Rais Kikwete amtaja mhusika wa Richmond

Rais Kikwete amtaja mhusika wa Richmond

kama kuna mambo Lowassa anayaogopa kama ukoma ni kuzungumzia kwa Kina Richmond,hilo ni donda ndugu lake,kwa sababu mie najua kwa sasa angefunguka vibaya,lakini we utaona hawezi kujibu kwa kina hilo,ukweli bwana ni kama mafuta ya taa na maji hujitenga
 
Safi sana mh.jk wakati huo wewe ulikuwa waziri wa wizara gani?inaonekana unafahamu tutajie na waliochukua fedha za escrow akaunt bank ya stanbic.
 
Usijifanye huelewi.waliotorokea UKAWA walishakataliwa na CCM

Wacha kudanganya watu wewe. Nani hakuona watu wakiimba Lowassa mpaka na rais mwenyewe. CCM hawakumkataa Bali walimkataishwa. Aliye mkataa ni kakundi tu ndani ya ccm.
 
Rais Jakaya Kikwete amesema anashangazwa na Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu kumtaka amtaje mhusika wa Richmond wakati mwenye Richmond yupo na anatembea naye mikoani.

Kikwete aliyasema hayo jana wakati akiwaaga wananchi wa Kigoma katika Uwanja wa Lake Tanganyika na kumtaka Lissu amtaje mwenye Richmond.
“Endapo Tundu Lissu atashindwa kumtaja mwenye Richmond, nitatoka hadharani na kumtaja mwenyewe,” alisema Kikwete.


Chanzo:
Mwananchi

Hili lafaa tuchukulie ni utani wa Kisiasa!
Ila kwa namna yoyote ile Kauli kama hii toka kwa Raisi wa Nchi anayemaliza muda wake ni yale yale marudio ya aliyoyasema Mkapa pale Jangwani dhidi ya Umma wa Tanzania walio nje ya Mfumo wa Chama Dola. Na ndiyo mfumo wa kulindana ulivyo unapokuwa nje ya mfumo wewe siyo mwenzetu.
 
EL hatajibu, yy jk anajua mhusika na kikatiba ana mamlaka makubwa tu s amtaje, au sitta na mwakyrmbe wasaidiane hata na slaa wamtaje na wampeleke mahakamani basi. Mchezo wa kitoto wanaocheza hautayumbisha upepo wa ukweli na kisiasa.
 
Kwa nini amtaje yeye wakati aliyestahili kumtaja ni Kikwete? Mwakyembe?

Kitu gani hukijaelewa hapo ndg yangu! Kama unafatilia Mwakyembe alimtaja Lowassa ndio muhusika wa Richmond na akatoa option mbili Lowassa kujizuru au kujadiliwa na bunge. Kama haitoshi JK pia kamtaja jana ingawa alimtaja kimafumbo, lakini tumemuelewa! Sasa ni zamu ya fisadi Lowassa kwa mdomo wake atuambie muhusika wa Richmond ni nani? Atuambie kwa ushahidi wa kuridhisha, Watanzania tunataka kujua kama sio yeye ni nani?
 
Mimi nafikiri kikwete tulimpa majukumu makubwa yaliyomzidi tusimlaumu sana hajui analotenda
 
Sasa yeye ni wa kushindana na Lissu kweli??...Lissu ambaye wala sio waziri
 
  • Thanks
Reactions: Awo
Kama rais ambaye ni amiri jeshi mkuu na kiongozi wa nchi anaogopa kutaja jina la huyo wanamwita fisadi,sidhani kama kuna mtu akuja kumshitaki.
 
Sasa ukijua lowassa anahusika na wizi kwenye deal ya richmond, kwanini ulishindwa kumuadabisha? Kwani ulishindwa kumuadabisha chenge. Kifupi ni kusema kwamba chama chenu kina operate kama gangsters, genge la
BINAFSI NASHANGAA.
Kuna haja gani ya kuunda mahakama nyingine kwani hizi zilizopo zimeshindwa kazi. haya izo zitakazoundwa zitakuwa na mahakimu toka nje ya nchi au hawa hawa
huu ni ubadhilifu mwingine na danganya toto ya kiccm kama walivyozoea!
jamaa akiingia ikulu atageuka. nani hamjui Magufuli na kauli zake za jazba.
yani unategemea aunde eti mahakama ya kumtuhumu bosi wa RIchmond aliempitisha 5 bora kule Dodoma. wapi?
kitakachotokea ni kuundwa tume itakayoleta mapendekezo ya kuwa na idara maalum katika mahakama hizi. Hapo atasema kaunda tayari.
sakata la Richmond litafukiwa kwa kuhakikisha mgao haupo ili kuwasahaulisha watu. zitakuja ajenda moto moto kufuta hoja. ni pamoja na kutoa unafuu flani wa bei ya bidhaa muhimu kwa kipindi flani
atakaeuliza kwa nn rais hujaunda mahakama kama ulivyoahidi. Magufuli mzuri wa kujibu..... atasema niliunda tume kushughulikia suala hili. ikanishauli hakuna haja bali kuwe na maboresho katika idara za mahakama iliopo ili kupunguza gharama za mahakama mpya. ss unataka nitumie kodi za wanachi wangu vibaya!!!! Je tangu niingie ikulu umesikia ufisadi? kama unamjua na ushadi unao nipe sasa hivi! mchezo kwishnea
hapo changa la macho tayari..
 
Kitu gani hukijaelewa hapo ndg yangu! Kama unafatilia Mwakyembe alimtaja Lowassa ndio muhusika wa Richmond na akatoa option mbili Lowassa kujizuru au kujadiliwa na bunge. Kama haitoshi JK pia kamtaja jana ingawa alimtaja kimafumbo, lakini tumemuelewa! Sasa ni zamu ya fisadi Lowassa kwa mdomo wake atuambie muhusika wa Richmond ni nani? Atuambie kwa ushahidi wa kuridhisha, Watanzania tunataka kujua kama sio yeye ni nani?

Sheria haisemi hivyo ndugu yangu. Kwamba polisi wakikutuhumu umefanya kosa lakini wakakosa uthibitisho au vigezo basi wewe ndio uwatajie wao polisi mhusika halisi, sio hivyo kaka.

Yaani kama wewe uhusiki basi ni jukumu la wao polisi kumtafuta mhusika halisi, sio jukumu lako wewe tena.
 
Uswahiba wa JK na fisadi Lowassa ndio umemfanya fisadi Lowassa aendelee kudunda, lakini JK anamaliza muda wake na tumeambiwa kesi ya fisadi Lowassa haina mwisho siku yoyote itaunguruma! Kwahiyo raia tukae mkao wa kula, Magufuli akiingia Ikulu lazima tuanze Lowassa.
Hapa Unataka kusema nini mkuu?kwamba wanaccm hamuwezi kutenganisha maslahi binafsi na maslahi ya nchi?
 
Lowasa anapaswa kulaumiwa kwa kila jambo lililotokea ndani ya utawala wa JK kwasasabu yeye ndiye aliyekuwa mshawishi mkuu wa kumpeleke jk ikulu. Hivyo basi inamuwia vigumu JK kumsulubu swahiba wake wa miaka lukuki.
Mkuu nchi itaongozwa kiswahiba hadi lini??ila ilimuwia rahisi kuunda tume na kuwasafisha watuhumiwa wote wa escrow na wengine kujiuzulu bila hatua nyingine kufuatia....ama hakika huu pia ni msiba kitaifa na ndio maana tunasema adui namba moja wa maendeleo yetu ni huo mfumo wenu wa utawala.
 
Rais gani huyu jamani?asie na nguvu asie na amri?wa nini lakini huyu baba?kashaharibu nchi ila bado aibu hana anaongea kimbea mbea?Kikwete nenda salama ila usiendelee kutuchanganya
 
Alishawahi kusema hajui owners wa Richmond na wahusika hawajui

As a commander in chief, aliaminika, sasa leo anakuja kisiasa zaidi

This kasshfa is not over

Aliwahi pia kusema Kilichompata Lowasa kuhusu Richmond ni ajali ya kisiasa, sasa inamaana huyu rais anasema uongo chini ya kiapo? Achunguzwe
 
Kama rais ambaye ni amiri jeshi mkuu na kiongozi wa nchi anaogopa kutaja jina la huyo wanamwita fisadi,sidhani kama kuna mtu akuja kumshitaki.

Ivi unajua kama rais ni taasisi nyeti kuliko nyeti tulizonazo sasa kama taasisi ya rais ikae ianze kujibishana mipasho sasa hiyo itakuwa ikulu au uharo ukimya wa kikwete sio kama dhaifu bali maadili ya kazi inabidi afanye hivyo. We subiri akitoka madarakani akiwa raia mwema muone moto wake ila msije kufukuzana tu uanachama
 
mwenzke kashamtaja, kasema hakn alichofny jk hakujua, sasa na yeye kutaja tu, tena kwa mafumbo ni uwoga wa hali ya juu, yeye kama raisi ilibid atoe amri kesi ifunguliwe mtu afungwe, lakini kupiga domo kwa watu ni udhaifu wa juu kwa amri jeshi, kuna kitu si bure
 
Back
Top Bottom