Rais Kikwete adanganywa tena

hii niliisikia dodoma wakati wa bunge kuwa
mzee kifimbo cheza a.k.a mkono adv. ndiye mhusika wa hii skendo!
nitarudi na data
 
nafikiri jk hana haja ya kuwa makini,anachosubiri ni kumaliza miaka yake minne aondoke.kufanya vizuri au kutofanya vizuri haimjalishi maana hana haja tena ya kura zenu. cha muhimu watazania tuwe makini na nchi yetu.tufanye kazi kwa bidii na kuiombea nchi yetu.
 
kwa kuwa rais na wasaidizi wote wana system ya walio desa -UDSM, walio tumia fatomu MIST, simbi - SUA, nyoka etc ndio hayo madhara yake yatamtafuna sana maana haingii akilini ikiwa kila siku anadanganywa halafu hao hao anawaacha wanaendelea kumdhalilisha na kujidhalilisha zaidi.
 
Walikua wanampima tu kama ameanza kuwa makini, kumbe ...........
 
Hawa watendaji mbona wanamdhalilisha hivi Rais wetu jamani ? Yaani wanamdanganya kama mtoto mdogo na yeye anaingia kichwa kichwa tu
 
muda wa kusoma Nyaraka atoe wapi , hahaaaaah , nakubembea aende nani, hahahaaaaah Kura zenu ndio zimetuletea Mtu huyu jamani najuta kuwa Mtanzania
bembea_1.jpg
 
Kwa hili nikiambiwa kuandamana nitaandamana ili kumshinikiza Rais awawajibishe hao waliomdanganya. Watu hawawezi kuchezea taasisi ya Urais huku tumekaa kimya na kuchekelea. Ikishindikana nitamtuma Mbunge wangu apeleke hoja Bungeni ili kuchunguza tatizo ni nini hadi Rais adanganywe mara kumi na tatu kwa muda wa miaka 6 na ni nani anahusika kumdanganya.
 
hakusoma kilichoandkwa.. Na sio amedanganywa by the way msimlaumu sana alkuwa kwenye maandalizi ya safari ya marekani.
 
KWELI HUYU Chifu Kikwete wa Tanzagizaajalifisadinia! HATA DOCTOR ANADANGANYWA! TUSILAUMU TU WATENDAJI WAKE NAYE PIA AWAJIBIKE.
 
Huyu ni Rais au Mtalii, Tanzania imekwisha jamaa hana muda hata wa kuulizia. Duh hii kali.
 
Hampendi Baba wa Taifa hayati Julius Nyerere -- mnakumbuka ile ishu ya chuo cha jeshi cha Monduli? Mmewahi kumsikia hata siku moja JK akimtaja Nyerere kama 'Baba wa Taifa'?
sikubaliani na wewe hata kidogo hapo kwenye red,huo ni uzushi tu,nimeshawahi kuona post humu jamvini(kama sio wewe itakuwa member mwingine) ikisema jk huwa hatamki Nyerere kuwa 'baba wa taifa', ilibidi niwe nafatilia hotuba zake na katika hotuba moja ya juzi juzi sikumbuki ilikuwa ni katika shughuli inayohusu nini ila kama sikosei ilikuwa pale polisi kilwa road nilimsikia akitamka 'baba wa taifa' kama mara mbili hivi, nikipata uhakika wa hiyo hotuba nitaiweka jamvini, na pia katika mkutano wa leone sullivan alitamka nyerere as 'father of the nation' je na hiyo haikubaliki kwa kuwa alitamka kwa kiingereza? jk ana matatizo,weakness na kitu kama uzembe au kutojali mambo fulani muhimu ambapo ni vigumu kuvumilika ila siko tayari kushabikia kitu ambacho si kweli kuhusu yeye na hasa nikiwa nina ushahidi wa kusikia au kuona. kutosoma nyaraka halafu anasaini kama mbumbumbu ni jambo la hatari sana na inaweza kuleta madhara makubwa kwa taifa naona hayuko makini sana na mambo ya ndani ya nchi but yuko busy na safari za nje na labda anataka kuvunja rekodi na kuingia kwenye guiness book kuwa rais aliyesafiri sana kuliko marais wote hapa duniani na kwa bidii aliyonayo ya kusafiri mpaka amalize awamu hii anaweza akafanikiwa.
 
ha ha ha ha, inanikumbusha episode ya Chief Mangungo; bora Chief hakujua kusoma na kuandika na huyu, Doctor! Ha ha ha ha ..........
 
Tuwe serious jamani, hili suala si kweli kuwa limechomekewa bali ni makusudio, la kama limechomekewa kweli bac tuambiwe ni nani aliyelichomeka kwa kuwa hiyo document iliyokuwa signed imepita kwa watu mpaka imemfikia huyo "Dokta' Vasco. So pinda hebu tuwekee hiyo document imeandaliwa na nani imepitia kwa nani kabla ya kufika kwa Mhishimiwa Kipenzi Chetu mpendwa wetu mwaminiwa, mstahiki Rahisi Dokta Profesa Amiri jeshi Luteni Kanali Mr. JK
 
Hivi kumbe tuna Rais Zezeta?

Inakuwaje Rais mzima unasaini kitu usichokijua? Jamani kuna hatari siku moja huyu mchovu atakuja kusaini nyaraka zinazosema kuanzia leo wananchi wa Tanzania watakuwa watumwa wa Marekani!

Hivi huwa ana haraka ya kwenda wapi kiasi anaona wanamchelewesha?

Yaani hili nalo anahitaji kupelekwa shule jamani?!!

HUYU NAYE NI AINA YA AKINA MANGUNGO WA MSOVERO!!!!
 
Pinda pia alimpa fursa mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere, kutoa kauli yake kuhusu suala hilo, ambaye alisema yeye asingependa kuliingilia suala hilo.
"Hili suala halina tatizo, ninyi na wananchi wote mtakavyoamua ndivyo iwe hivyohivyo," alisema Mama Maria
.
[/QUOTE]

Punda naye eti akataka amwingize mama Maria Nyerere kwenye mtego wake! Ka mama nako kalimjibu vizuri huyu zezeta mwingine!! Saaaaafi saaaana mama!!

Hivi wadau huyu PM mchovu mwenyewe hakulisoma hilo tangazo la Serikali kabla halijaenda kwa Rais? Kwa nini anataka kujitoa kwenye hili sakata?
 
Du kazi kweli kweli huyu jamaa anaweza hata kutuuza wazima wazima very interesting au ndo alikuwa anawahi safari ya USA!

Tulikwisha uzwa long time, kama unadhani uko huru kwenye nchi yako umejidanganya. Akiitwa USA nakimbia hata kama nchi iko gizani!
 
Back
Top Bottom