Wanabodi,
Kwanza naomba radhi kwa kutokuwepo kijiweni kwa muda mrefu sana na hakika nimeutumia muda huo kuyafahamu mengi sana yanayohusu Utawala mzima wa Kikwete..
Yamkiniki, mengi yamezungumzwa lakini moja kubwa ambalko siku zote sikuweza kulifanyia utafiti ni uwezo wetu sisi wenyewe kuongozwa!... Watanzania ni kigezo kikubwa cha mafanikio yote iwe Umaskini, Ufisadi, uzembe na kila baya ambalo tunaliona kwa viongozi wetu..Umaskini wetu umetokana na sisi wenyewe...yaani WATU.
Mikakati mingi ambayo Mzee Mwanakijiji ameweza kuiorodhesha kama kazi aloshindwa Kikwete nimekuja gundua kwamba ilianza kazi mara moja baada tu ya kuchukua kiti cha IKULU lakini ndipo Watanzania walipofanya choo cha shimo, bila aibu watu wanaitumia nafasui hiyo kujitajirisha na kufungua miaya ya uzalishaji binafsi... yaani ni kazi yetu siku zote ni Kunyea pale panapotupa riziki.
Ifikie wakati sisi wananchi tuzipokee lawama na mara nyingi kujitazama sisi wenyewe kama kweli tunawezwa kuongozwa..Ni rahuisi kuongoza kondoo zizini kuliko kuongoza wadanganyika..acha mbali hata kuwashauri tu ni kazi kubwa ambayo sijui wala siwezi kuipa mfano.
Kwa mfano, serikali ilitoa msamaha wa ushuru kwa Watanzania wanaotaka kuwekeza nchini badala yake sisi wenyewe tul;ianza kuitumia nafasi hiyo kuingiza mtaji na vitendea kazi (Capital goods) lakinimatokeo ya msamaha huo ilikuwa wazalendo wenyewe tukiuza vibali na nafuu hizo kwa wahindi na wazungu wawekezaji, mali ikiagizwa na kuuzwa madukani pasipo kufungua miradi iliyokusudiwa.. matokeo yake serikali imesimamisha misamaha hiyo... lawama kwa Kikwete..
Kikwete alitoa fedha yale mabillioni ya Kikwete, hao hao viongozi wetu wa mashirika na jumuiya zetu wakayachota na kuanzisha biashara zao, wengine wakienda China na India ikafika waakati rais wetu akasimamisha zoezi hilo..Yaani ni mikakati isiyokuwa na kipimo ambayo imeanzishwa na kushindikana kufanya kazi kutokana na wananchi wenyewe kukosa Uzalendo..
familia zinavunjika kwa mirathi, baba anamzima mwanae fedha, ndugu anamlima nduguye kwa fedha kiasi kwamba kwa mtu yeyote anayesoma habari hii anambie ni familia ngapi tanzania zinaweza kushirikiana pasipo kionyongo ama kutafuta kuibiana...Sisi sote humu tumeshindwa kupiga hatua moja mbele kwa sababu sote hatuna watu wa kuwaamini. leo hii Mkandara hapa nitaonekana sijafanya lolote wala sifanyi kitu kwa familia yangu, lakini ukweli ni kwamba haihesabiki ni kiasi gani cha fedha nilizokwisha poteza pamoja na kutokuwepo kwa mafanikio yoyote..watu wanahesabu wafanikio yangu kutokiana na maisha ya ndugu zangu ambao ndio wamefuja mali ama mtaji mdogo niliokuwa nao..Leo hii sote maskini na tunalia njaa..Lawama kwa Mkandara! - ebooooooo
Nawaombeni nyote tujitazame kwanza sisi.. Sisi Wadanganyika tuna tatizo kubwa la Uaminifu, ni wezi mafisadi na washenzi wakubwa ambao hatuhitaji kusaidiwa wala kuongozwa isipokuwa kwa bakora..Na sote humu tunalaumiwa na familia zetu, marafiki wetu na kadhalika lakini jaribu kusaidia ndio utafahamu uchungu wa kupoteza nguvu yako ulokusanya ktk kipindi kigumu cha maisha..
Watu wanafikiri huko Ulaya fedha inaokotwa! watu mnazoa tu mifedha ktk snow wasifikirie nguvu na kazi ngumu iliyowapata mnapojituma huko makazini..na bahati mbaya ukimwamini mtu anakutoka tena mkali unapoulizia maendeleo yake mwenyewe..Nina hakika kwa nyote mnaomlaumu Kikwete, mnashindwa kuzitazama nafsi zenu wenyewe...na hakika wengi wetu tunalaumiwa kama anavyolaumiwa Kikwete pasipo kujitambua kwamba tatizo linaanza kwao, Huna wa kumwamini na huwezi kuongoza nchi ama familia pasipo kuwa na watu..
Haya ndio maisha yetu wakuu zangu, Kila Mtanzania ni striker! anataka kufunga goli hata goal keeper hatuna formation wala formula..kila mtu anasubiri ukosee akufunge goli,(akuingize mjini) iwe mtaani ama serikalini na hakika usitegemee pasi ama umoja wa Watanzania... ukweli ni kwamba kila mtu sasa hivi anabeba msalaba wake..na hakuna kiongoziatakayeweza kuibadilisha hali hii na akapendwa na wananchi..trust me!
Kilichobakia ni sisi wenyewe kubadilika kurudisha Uzalendo, upendo na udugu uliopotea baada ya Ubepari kushika nafsi zetu..UZALENDO iwe mbiu ya kila mmoja wenu kabla ya kulaumu maanake sidhani kama kuna mtu humu anaweza kunambia anaweza kumwekea imani kila Mtanzania..The slogan inayotamba tanzania leo ni Trust NO ONE! na it's true ukijaribu kunyoosha mkono watu watakulaza nje!
kwa herini!