Rais Jakaya Kikwete anafaa kuongoza Tanzania!

Mie namsihi kabla hajajitokeza rasmi kuwania uongozi kwa awamu nyingine, atuahidi na atuwekee wazi mikakati ya kutekeleza kuwa atajitenga na mafisadi, majambazi na wauza unga katika kampeni zake zijazo. Katika zile kampeni zake za 2005, yule jambazi maarufu wa Arusha aitwaye Justin Nyari alikuwa akitamba waziwazi kabla hata kampeni hazijaanza rasmi kuwa marafiki zake JK na Lowasa watakuwa rais na waziri mkuu respectively. Na hata alipokutwa na hatia ya ujambazi wa kutumia silaha na kufungwa miaka 30 jela, alilalama kuwa kafungwa kwa sababu za kisiasa, na atakapokuja rais mpya angemtoa. Na kweli, baada ya kikwete kuingia madarakani alimteua jaji mpya Othman Chande ambaye alisikiliza rufaa ya Nyari na kumwachia huru!

Tunahitaji rais ambaye hana uhusiano hata wa kuhisiwa au wa kusingiziwa, na wahalifu. Hatutegemei mhalifu ajisifu kuwa ana uswahiba na rais, halafu huyo rais anyamaze tu kama vile ni sawa!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom