Rais Jakaya Kikwete anafaa kuongoza Tanzania! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Jakaya Kikwete anafaa kuongoza Tanzania!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MPadmire, Jan 13, 2010.

 1. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #1
  Jan 13, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,631
  Likes Received: 904
  Trophy Points: 280
  Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania, anafaa kuiongoza Tanzania.

  Rais ana dhamira ya kweli ya kuleta maisha bora kwa kila mtanzania. Maisha bora yatachelewa lakini yatapatikana.

  Rais Jakaya Kikwete ameruhusu uhuru wa vyombo vya habari. Amewaruhusu watu wakosoe viongozi na wakosoaji wako huru kabisa.

  Hii dhana ya kuwa huru kukosoa serikali inawaogopesha viongozi, hata kama ni marafiki zake Jk. Kwa hiyo JK ameruhusu UMMA kuwasulubu mafisadi.

  JK ameruhusu mafisadi kusemwa hadharani na wananchi wanawajua na hivyo 2010 mafisadi hawataambulia kitu.

  Na baada ya uchaguzi wa 2010 mafisadi wote wataondolewa kiaina, na viongozi wataogopa kufanya ufisadi. Kwa hiyo JK anajua hilo, na ni mbinu nzuri sana.

  Heko JK, utashinda tena 2010 na utafanikiwa.
   
 2. Jenerali QoyoJB

  Jenerali QoyoJB JF-Expert Member

  #2
  Jan 13, 2010
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 307
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Anafaa lakini mawaziri wengine asirudi nao awamu ya pili. Wanamwangusha mno, wote wangekuwa kama pinda na magufuli au Aggrey mwanri japo nao wana makosa tungepiga hatua. Kina Kapuya wapumzike kwa heshima jamani toka enzi hizo wapo tu mpaka wafie huko? JK achukue wat kama kina mama Kilango, Ole sendeka, Makwembe kwenye serikali yake mambo yatakuwa motomoto kama phalsafa yake ya kasi, ari mpya.
   
 3. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #3
  Jan 13, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180

  kweli unamaanisha??
   
 4. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #4
  Jan 13, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  kwani hao mawaziri wasio faa nani aliwaweka madarakani ? Sofia Simba, Adam Malima, Ngeleja, kAwambwa Shukuru, Chiligati, Mkuchika....orodha ya mawaziri vimeo inaendelea.
  tumekua tukilalama na mawaziri vimeo kipindi chote cha utawala wake, amekuwa akiziba masikio yake, alilazimishwa kuwaondoa Mafisadi kutokana na kuanguka kwa Lowasa , karamagi na Msabaha kutokana na kupokea hongo ya mradi wa kufua umeme maarufu kama kashfa ya Richmond.

  JK hafiti katika viwango vya marais wa kututoa hapa, hana uthubutu , hana jipya, anaiga mitindo ya utawala ya watawala walioshindwa, ameshidwa kujitenga na makundi ya wala rushwa , kashindwa kutenda yale matarajio ya WATANZANIA masikini waliompa kura.
  mnaendelea kutuaminisha kuwa tayari JK ameishashinda uchaguzi 2010, naamini bado , kunajaribu kubwa anapaswa kupambana nalo na kwa ustadi bila hivyo yeye na CCM yake itakwenda alijojo.

  natamani kuona JKakiondolewa madarakani kwa sanduku la kura hii 2010, kama mikakati itakaa vyema hapana shaka huu ni mwaka wa mwisho kwamafisadi kuneemeka , maandishi yapo UKUTANI, ukitaka yasome kama hutaki yapotezee.
   
 5. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #5
  Jan 14, 2010
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145


  Nimekwazika na hilo neno Mkwere katika thread yako; naona umelitumia Jina hilo kimakosa, ni kama vile unamkashifu. Ni vema ukabadilisha na ikasomeka Mtukufu Rais JK anafaa kuongoza Tanzania?

  Ni ushauri tu.
   
 6. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #6
  Jan 14, 2010
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Pia nimeendelea kukwazika kwa wewe kuendelea kutumia neno Mtukufu wakati ukujua dhahiri kuwa sio yeye, wewe au mimi tunaoweza kuwa watukufu, ila Muumba! Angekuwa mtukufu, kazi yake na wateule wake pia wangekuwa watukufu, na kila kitu kingekuwa kitakatifu.
   
 7. K

  Kabonde JF-Expert Member

  #7
  Jan 14, 2010
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Kweli kabisa hata mimi nimekwazika sana unamwita Mkwere Mtukufu wakati anashindwa kuwafikisha mahakamani mafisadi.
   
 8. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #8
  Jan 14, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Kikwete hawezi kuitwa mtakatifu maana hana utakatifu hata chembe, mtakatifu gani huyo ?
   
 9. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #9
  Jan 14, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ni kweli ana dhamira, lakini hana uwezo
   
 10. M

  Mkandara Verified User

  #10
  Jan 14, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Wanabodi,
  Kwanza naomba radhi kwa kutokuwepo kijiweni kwa muda mrefu sana na hakika nimeutumia muda huo kuyafahamu mengi sana yanayohusu Utawala mzima wa Kikwete..
  Yamkiniki, mengi yamezungumzwa lakini moja kubwa ambalko siku zote sikuweza kulifanyia utafiti ni uwezo wetu sisi wenyewe kuongozwa!... Watanzania ni kigezo kikubwa cha mafanikio yote iwe Umaskini, Ufisadi, uzembe na kila baya ambalo tunaliona kwa viongozi wetu..Umaskini wetu umetokana na sisi wenyewe...yaani WATU.

  Mikakati mingi ambayo Mzee Mwanakijiji ameweza kuiorodhesha kama kazi aloshindwa Kikwete nimekuja gundua kwamba ilianza kazi mara moja baada tu ya kuchukua kiti cha IKULU lakini ndipo Watanzania walipofanya choo cha shimo, bila aibu watu wanaitumia nafasui hiyo kujitajirisha na kufungua miaya ya uzalishaji binafsi... yaani ni kazi yetu siku zote ni Kunyea pale panapotupa riziki.

  Ifikie wakati sisi wananchi tuzipokee lawama na mara nyingi kujitazama sisi wenyewe kama kweli tunawezwa kuongozwa..Ni rahuisi kuongoza kondoo zizini kuliko kuongoza wadanganyika..acha mbali hata kuwashauri tu ni kazi kubwa ambayo sijui wala siwezi kuipa mfano.

  Kwa mfano, serikali ilitoa msamaha wa ushuru kwa Watanzania wanaotaka kuwekeza nchini badala yake sisi wenyewe tul;ianza kuitumia nafasi hiyo kuingiza mtaji na vitendea kazi (Capital goods) lakinimatokeo ya msamaha huo ilikuwa wazalendo wenyewe tukiuza vibali na nafuu hizo kwa wahindi na wazungu wawekezaji, mali ikiagizwa na kuuzwa madukani pasipo kufungua miradi iliyokusudiwa.. matokeo yake serikali imesimamisha misamaha hiyo... lawama kwa Kikwete..

  Kikwete alitoa fedha yale mabillioni ya Kikwete, hao hao viongozi wetu wa mashirika na jumuiya zetu wakayachota na kuanzisha biashara zao, wengine wakienda China na India ikafika waakati rais wetu akasimamisha zoezi hilo..Yaani ni mikakati isiyokuwa na kipimo ambayo imeanzishwa na kushindikana kufanya kazi kutokana na wananchi wenyewe kukosa Uzalendo..
  familia zinavunjika kwa mirathi, baba anamzima mwanae fedha, ndugu anamlima nduguye kwa fedha kiasi kwamba kwa mtu yeyote anayesoma habari hii anambie ni familia ngapi tanzania zinaweza kushirikiana pasipo kionyongo ama kutafuta kuibiana...Sisi sote humu tumeshindwa kupiga hatua moja mbele kwa sababu sote hatuna watu wa kuwaamini. leo hii Mkandara hapa nitaonekana sijafanya lolote wala sifanyi kitu kwa familia yangu, lakini ukweli ni kwamba haihesabiki ni kiasi gani cha fedha nilizokwisha poteza pamoja na kutokuwepo kwa mafanikio yoyote..watu wanahesabu wafanikio yangu kutokiana na maisha ya ndugu zangu ambao ndio wamefuja mali ama mtaji mdogo niliokuwa nao..Leo hii sote maskini na tunalia njaa..Lawama kwa Mkandara! - ebooooooo

  Nawaombeni nyote tujitazame kwanza sisi.. Sisi Wadanganyika tuna tatizo kubwa la Uaminifu, ni wezi mafisadi na washenzi wakubwa ambao hatuhitaji kusaidiwa wala kuongozwa isipokuwa kwa bakora..Na sote humu tunalaumiwa na familia zetu, marafiki wetu na kadhalika lakini jaribu kusaidia ndio utafahamu uchungu wa kupoteza nguvu yako ulokusanya ktk kipindi kigumu cha maisha..
  Watu wanafikiri huko Ulaya fedha inaokotwa! watu mnazoa tu mifedha ktk snow wasifikirie nguvu na kazi ngumu iliyowapata mnapojituma huko makazini..na bahati mbaya ukimwamini mtu anakutoka tena mkali unapoulizia maendeleo yake mwenyewe..Nina hakika kwa nyote mnaomlaumu Kikwete, mnashindwa kuzitazama nafsi zenu wenyewe...na hakika wengi wetu tunalaumiwa kama anavyolaumiwa Kikwete pasipo kujitambua kwamba tatizo linaanza kwao, Huna wa kumwamini na huwezi kuongoza nchi ama familia pasipo kuwa na watu..
  Haya ndio maisha yetu wakuu zangu, Kila Mtanzania ni striker! anataka kufunga goli hata goal keeper hatuna formation wala formula..kila mtu anasubiri ukosee akufunge goli,(akuingize mjini) iwe mtaani ama serikalini na hakika usitegemee pasi ama umoja wa Watanzania... ukweli ni kwamba kila mtu sasa hivi anabeba msalaba wake..na hakuna kiongoziatakayeweza kuibadilisha hali hii na akapendwa na wananchi..trust me!

  Kilichobakia ni sisi wenyewe kubadilika kurudisha Uzalendo, upendo na udugu uliopotea baada ya Ubepari kushika nafsi zetu..UZALENDO iwe mbiu ya kila mmoja wenu kabla ya kulaumu maanake sidhani kama kuna mtu humu anaweza kunambia anaweza kumwekea imani kila Mtanzania..The slogan inayotamba tanzania leo ni Trust NO ONE! na it's true ukijaribu kunyoosha mkono watu watakulaza nje!

  kwa herini!
   
 11. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #11
  Jan 15, 2010
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280

  Tanzania imemshinda ...jaribu kumpa familia yako aiongoze..nadhani hatashindwa!!
   
 12. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #12
  Jan 15, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,631
  Likes Received: 904
  Trophy Points: 280
  Hello there,

  Asanteni kwa Michango yenu.

  Baadhi wamejibu kwa hasira na jazba kutokana na hali ilivyo Tanzania, naelewa. lakini tuwe wavumilivu na mambo mazuri hayataki haraka.

  Kulingana na hali halisi ya Tanzania asilimia kubwa ya wapiga kura wako vijijini, na sio waelewa kama nyinyi. Sasa msiwe na hasira tu, mmechukua hatua gani kuwafikia watu wa vijijini?

  Lakini hata hivyo Mh rais amejitahidi, usimbeze. Yeye kama Rais ana mapungufu, ni binadamu na ni kwa sababu ya uhuru wa vyombo vya habari ndo maana mmeyajua.

  asanteni
   
 13. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #13
  Jan 15, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,372
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  naunga mkono hoja....
   
 14. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #14
  Jan 15, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Huwezi kusema anafaa wakati hakuna comparison..kufaa ni relative term anafaa ukilinganisha na nani? JK vs. XXXX

  Tusubiri wanachama wa CCM waamue kama ndio chaguo lao tuwalinganishe na kina baregu, lipumba etc.. ndio tutatoa constructive comment
   
 15. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #15
  Jan 15, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,372
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  uhuru kwenye mateso.....................hana uwezo wa kuwa na maamuzi kama rais...........ni mbabaishaji..........anawaogopa mafisadi.............anashinda nje kuombaomba wakati tuna rasirimali lukuki..........alikili kuwa tz ni yenye neema kwa hiyo inawezekana sasa anatuyeyusha..........shuleni hakuna walimu,vitabu madawati alafu uchuli unatangwa kuwa unakua kwa kasi ya ajabu..........
  Hafai bora hata tusiwe na rais kwani siopni kazi yake....
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  Jan 15, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  kama haya yote unayoyasema yanatoka moyoni, unaamini kabisa kuwa uhuru tulionao sasa ni zawadi ya Kikwete, inabidi umtengenezee madhabahu na umtolee sadaka pamoja na kumfukuzia uvumba!
   
 17. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #17
  Jan 15, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,372
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  ahahaaaa.........maneno mengine yanaumiza kweli.....
   
 18. N

  Nanu JF-Expert Member

  #18
  Jan 15, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  JK to me has done his part and he deserve his final term. He has done a lot but we still have a lot not done and no any president will do all of them in his two terms or even if he stays for 2 decades like JKN. JK has done a lot and it is only intentional blind who will be against it. Lets give him support by electing the good legislators(MPs).
   
 19. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #19
  Jan 15, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  1. Kwa sababu ameruhusu mafisadi kusemwa hadharani ndiyo unaona anafaa? kuruhusu kumsema mtu nayo unaita perfomance?

  2. Hata ukiwa wewe ukiteuliwa na hicho Chama chenu kuwa mgombea wa urais, utapita kwa kishindo.

  toa hoja za msingi.... nakusubiri
   
 20. Kionambele

  Kionambele JF-Expert Member

  #20
  Jan 15, 2010
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 242
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  JK kwa kweli ni bonge la President sema tu kakuta nchi ilishaoza. Lazima tuliangalie hili pale mwaka 2005 JK alikuwa kama kondoo katikati ya mbwa mwitu na isingekuwa rahisi kuonyesha moto wake pale, wangemzima na tungepata Rais kama EL kwa mfano. Nchi ingekuwaje?

  Kwanza EL au jamaa zake wengine wangechukua nchi JF members tungesakwa vibaya mno na kupotezwa. Magazeti yangebaki yaleyale ya kifashisti. Watanzania wasingeona bahari tena maana beach zote zingefungwa kupisha nyumba za kina EL na mtandao wake, si unakumbuka alivyotaka kuifisadi coco beach.

  Hata ingekuwa nani uwekwe kwenye nafasi ya JK kama kweli unajua system inavyofanya kazi usingeweza kufanya bora zaidi ya JK. Huu ni wakati mgumu kuliko hata nyakati za vita vya kagera.( Kama una ufahamu wa kutosha).

  JK anahitaji support ya watanzania na ndio maana yuko tayari kushirikisha wazalendo katika shughuli za kiserikali bila kuangalia tofauti za kiitikadi kwa mfano Zito Kabwe na wengineo.

  Watanzania tunajitahidi sana kumvunja moyo JK ili mwaka 2010 awaachie mafisadi warudi tena na safari hii watatuonyesha cha mtema kuni. Kazi aliyoianzisha JK tumsapoti aimalizie miaka hii mitano ijayo. Hakuna mtu sasa hivi anaweza kuwa mgombea bora kuliko JK.

  Kila majira na Nabii wake. Kuna wakati wa Musa, Kuna wakati wa Ibrahimu, Kuna wakati wa Yesu na hapa Tanzania tusiharibu mambo huu ni wakati wa Jakaya Mrisho Kikwete. Wanaompinga ni mafisadi kwa sababu amewabwaga chini. Hakuangalia uso wa Lowasa wala Mramba wala Yona wala Mgonja wala nani.

  Kabla ya kumkataa Kikwete tukumbuke kuwa mkataa pema, Pabaya panamwita.
   
Loading...