Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyote

Nchi yetu ni nchi inayofuata katiba na inaendeshwa kwa misingi ya sheria, "the rule of law" kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni, hakuna aliye juu ya sheria, hata rais hayuko juu ya sheria, hivyo kuna baadhi ya kauli za rais wetu, kiukweli ni kauli za kibabe tuu, vitisho na kidikiteta, lakini tukija kwenye utekelezaji wa kauli hizi, zitatekelezwa kwa kuzingatia sheria taratibu na kanuni, hivyo hazitatekelezwa kama rais alivyotamka, au kama anavyotaka kuwaaminisha Watanzania.

Mkuu Pasco nimekunuu hapo juu. Kama kweli hii nchi ingekuwa inafuata "the rule of law"...Yaliyotendeka Zanzibar yasingetokea.
 
Pasco na wana bodi wengine humu ndani swali ni hili: Je hawa wanaolipwa mishahara minono ya kuanzia milioni 10 kwa mwezi wanaongeza "value" gani kwa mashirika wanayoyaongoza? Wanasaidia nini zaidi? Haya mashirika mengi kama sio yote yamekuwa mzigo kwa serikali kutokana na madeni, ubadhirifu, mikataba mibovu, yet ma Executive wao wanalipwa mishahara ya kimarekani. I say get rid of them lete watu wanye track record ya kutoa positive results then tuongee compensation.
 
Comrade Pasco mbona mfano wako umelinganisha na kampuni binafsi kama Microsoft.. Kwani hiyo ya serikali.. Kwani umesikia Magufuli anataka mishahara ya kampuni ya Bakharesa ipungue

Mkuu kwani unafikiri hilo halijui, analijua sana!! Sitaki kusema mengi ila nina swali dogo kwa Pasco: Hivi huyu JPJM aliwahi kukukwaza wapi kimaisha? Comments zako nyingi kuhusu kiumbe huyu si za kistaarabu hata kidogo, kuna wakati uliwahi kumsema jambo fulani ambalo siwezi kulirudia hapa, binafsi nilishikwa na bumbuwazi kwa kauli yako hiyo.

Nataka nikupe ushauri wa bure, ni hivi PASCO: May you please try 2 tone down your .... rhetoric levered against a selfless and honest man, unaweza kutumia a diplomatic language watu wakakuelewa - baada ya ushauri huo mfupi I hope next time you won't let your resentment 2ward Dk.Magufuli cloud your.....
 
Wanabodi,

Kufuatia kazi nzuri inayofanywa na rais wetu, Dr. John Pombe Magufuli, ya utumbuaji majipu ya rushwa, ufisadi na uzembe, imefikia wakati baadhi yetu kumuona Rais Magufuli kama Mkombozi, kama Masiya, kama Malaika, kama Nabii, na bado kidogo tuu kuna wenzetu, wanaweza kumuona kama ni Mungu Mtu, hivyo wanataka kumuabudu, hivyo ukisema chochote against Magufuli, kwa waabudu hawa, utaonekana kama umekufuru!, hivyo watakushukia kwa nguvu zote, hili likitokea kwenye uzi huu, mjue nililijua.

Ukweli Dr. John Pombe Magufuli ni rais wetu, yeye sio bosi wetu, bali ni mtumishi wetu, sisi wananchi ndio mabosi wake, sisi ndio tumemuajiri hiyo kazi ya urais kwa kura zetu, sisi ndio tunaemlipa mshahara wake kwa kodi zetu, hivyo sisi ndio waajiri wake, na ndio tunaemlisha na kumvisha na kumfanya aishi, yuko pale ikulu kwa ajili yetu sio kwa ajili yake!, tena yeye ni binadamu, sio Mungu, sio nabii na sio malaika, hivyo kama binadamu pia anaweza kufanya makosa kama binadamu mwingine yoyote, hivyo kumkosoa kwa nia njema (in good faith), ni kitu kitu, na ukosoaji huo, unakuwa ni constructive criticism unakosoa kuwa kitu hiki ni wrong, pia unaweka ushauri wa the right thing to do!.

Nchi yetu ni nchi inayofuata katiba na inaendeshwa kwa misingi ya sheria, "the rule of law" kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni, hakuna aliye juu ya sheria, hata rais hayuko juu ya sheria, hivyo kuna baadhi ya kauli za rais wetu, kiukweli ni kauli za kibabe tuu, vitisho na kidikiteta, lakini tukija kwenye utekelezaji wa kauli hizi, zitatekelezwa kwa kuzingatia sheria taratibu na kanuni, hivyo hazitatekelezwa kama rais alivyotamka, au kama anavyotaka kuwaaminisha Watanzania.

Moja ya kauli hizi za vitisho na kidikiteta, ni kauli ya rais Magufuli, aliyoitoa akizungumza na wananchi wa home base yake kule Chato, kuwa atapunguza mishahara ya wale wanaopata mishahara minono na kuwaongezea wanaopata mishahara midogo. Miongoni mwa maneno aliyoyasema ambayo mimi nayaita ni kauli za vitisho na kidikiteta ni pale aliposema alipotolea mfano Mtanzania mmoja analipwa Shilingi milioni 40 kwa mwezi, huku Mtanzania mwingine akilipwa Shilingi 150,000, na kusema wanaishi kama peponi!. Amesema "nitahakikisha hakuna Mtanzania analipwa mshahara wa zaidi ya shilingi milioni 15!, mimi nimesema, mimi sio ndio rais!, nikisema nitafanya, nitafanya, kama kuna asiyetamka mshahara huo wa milioni 15, afungashe aende zake, kuna Watanzania wengi wenye uwezo, nawanaohitaji hizo kazi"!.

Kauli hii, ya rais imeshangiliwa sana na kuwapa wasiwasi wenye mishahaa minono, huku wakiwapa matumaini makubwa wenye mishahara duni, hii imewapa kitu kinachoitwa "Great Expectation" kuwa the gap kati ya wenye nacho na wasiona nacho, itapungua, matokeo yake, isipokuja kupungua, hawa wenye great expectations wataishia kupata a great despair.

Rais wa nchi ndie mtu mwenye mamlaka kuu kuliko mtu mwingine yoyote, lakini mamlaka hiyo, inatawaliwa na sheria, taratibu na kanuni, ambapo kiukweli, rais wa nchi, hana mamlaka yoyote kisheria, kikanuni au kiutaratibu, kupanga mshahara wa mtu, wala hana uwezo wowote kisheria kupunguza mshahara wa mtu yoyote, hivyo kauli ya Magufuli kuwa atapunguza mishahara, ni kauli ya kibabe tuu na kidikiteta, rais hana uwezo huo wala hana mamlaka hayo!. Ufike wakati viongozi wa kisiasa wasiachwe kutoa kauli za matumaini hewa, wakati hawana uwezo huo kisheria!. Nadhani hata Magufuli alipotoa kauli hiyo, aliitumia ile hulka yake ya "udikiteta" akijijua yeye ndio rais, hivyo yeye ndio kila kitu, akisema, amesema, kiukweli, ukweli halisi, rais sio kila kitu, rais yuko chini ya katiba, yuko chini ya sheria, na anabanwa na sheria, taatibu na kanuni!.

Niliwahi kuwa mtumishi wa umma, kanuni za utumishi wa umma, zinatambua kitu kinachoitwa "a legitimate expectation", yaani kama umeajiriwa kwa mshahara fulani, na ukawa unalipwa ujira huo, then hakuna mamlaka yoyote inayoweza kuupunguza ujira huo!. Hivyo hata rais hana mamlaka ya kupunguza mishahara yoyote inayolipwa kisheria, zile kauli za asietaka na aende, ni vitisho tuu na udikiteta!.

Kiukweli hii mishahara ambayo rais Magufuli ameiita ni mishahara ya peponi, kweli ni mishahara mikubwa, ila kwenye corporate world, ni mishahara ya kawaida kabisa, hata nchini Marekani, ma CEO wa makampuni makubwa, kama GM, GE, Microsoft, etc, wanalipwa mishahara mikubwa kuliko Obama. Hata Japan, rais wa TOYOTA analipwa mshahara mkubwa kuliko Waziri Mkuu wa Japan, hali ndio hivyo duniani kote, ila pia hii mishahara mikubwa ya Tanzania, sio kukubwa kivile kimataifa, ila ni kweli mishahara ya kima cha chini Tanzania, ni midogo kabisa ya level ya inhumane kutokana na umasikini wa taifa uliotopea, sasa umasikini huu, usitufanye kuwaadhibu wele wenye eheueni nao lazima waishi kwenye lindi la umasikini, badala ya kugawana utajiri, sisi tunagawana umasikini!.

Lengo la Magufuli kupunguza mishahara minono ni lengo jema kwa lengo la kufanya kitu kinachoitwa "standardization and harmonization" kwa ku "bridge the gap" kati ya the highest paid na the lowest paid, lakini harmonization haifanywi kwa kuwapunguzia wenye vipato vya juu, bali hufanyika kwa kuwapigisha "mark time", kuwasimamisha hapo walipo, na kuwainua wengine hadi wawakaribie!. Kwenye kanuni za utumishi, hakuna kitu kinachoitwa kupunguza mishahara!.

Kwa vile hiyo mishahara imepangwa kwenye strructures za mashirika hayo, kitu ambacho Magufuli anaweza kufanya, ni kwanza kuvunja hizo structures kuwaandikia barua za kuwaachisha kazi wafanyakazi wote wanaolipwa viwango vikubwa na kuwalipa haki zao zote, kisha kuvunja stucture na kutoa structure mpya yenye hizo salary scale za Magufuli, na kuwataka wale wote wenye nia ya kuendelea na scale hizo mpya za Magufuli, waombe kazi upya na kuajirriwa upya kwa scale mpya za Magufuli.

Sasa mtu aliyekuwa analipwa milioni 40 akiishandikiwa kustaafishwa, atachukuya barua yake ya kustaafu atalamna mafao yake na "golden handshake yake", kisha ataendelea kula pensheni yake ya 60% ya milioni 40 hivyo kuvuta milioni yake 24 kila mwezi, na kuachana na hiyo milioni 15 ya Magufuli, unless kama huu udikiteta wa Magufuli utaingizwa hadi kwenye mifuko ya pensheni, kwa kuiamuru mifuko hiyo kutoa pensheni ya ceiling ya mshahara wa milioni 15 tuu kwa kila pensioner hata kama ameastaafu na mshahara wa milioni 40!.

Namalizia kwa kumpongeza rais wetu, kwa kuwa na nia njema na Watanzania, ila namtahadharisha sana kuchunga kauli zake, haswa hizi kauli za kidikiteta na vitisho kwa lengo la kuleta matumaini chanya, kabla ya kauli hizo, ni vema aki consult wataalamu na washauri, kuhusu uwezekano wa kuwezekanika, ndipo atoe matumaini hayo, vinginevyo ni kuwapa Watanzania matumaini hewa!.

Nawatakia Jumapili Njema.

Pasco.
Kwa wageni na maandishi ya Pasco wa jf, unaweza kupitia nyuzi hizi ili uweze kujua huwa ninamsimamo gani kumhusu Magufuli.
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?.
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata .

Japo ni Dikiteta, Rais Magufuli ni Simple, Genuine & Down To E
JF Modes, Magufuli ni Rais Wetu, Asiabudiwe, Asiogopwe, Bali
Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria ...
If you can't beat them, join them! He is the worst dictator.
Katazo la Rais Kusafiri Nje ya Nchi bila Vibali: Je, Halikiuki Haki za Binaadamu...
Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 ni John Pombe Magufuli
Magufuli Kama Nyerere:Ni Mtu wa Watu, Hapapasi, Hamung'unyi
Yajue Makundi 10 Top Ten wa CCM, Ambamo Watatoa Top 5,

Kama Magufuli Anaangalia Clouds TV na Kuipongeza, Kunatum
ENL, CHADEMA na UKAWA, Tuyakubali Matokeo!,

Ushauri wa Bure Kwa Lowassa: Kwa Vile ni Magufuli, Kubali M
Ushauri wa Bure kwa Lowassa: Hata kama ni kweli uliibiwa kur

Ulisha sema Magufuli ni Dikteta, naomba usome maana na nia hasa ya udikteta halisi kwanza, kisha utakubali kuwa uwezo wa kufanya hayo anao na ni wanamchi wanampa hata kubadili katiba akitaka kama ndio inamzuia, maana tunamwelewa sisi waajili wake kwamba ndio kazi haswa tuliyo mwajilia afanye.
 
Comrade Pasco mbona mfano wako umelinganisha na kampuni binafsi kama Microsoft.. Kwani hiyo ya serikali.. Kwani umesikia Magufuli anataka mishahara ya kampuni ya Bakharesa ipungue

Mimi nilipoanza kumsoma tu huyu Jamaa nikajua amekurupuka kama kafumaniwa, amekimbia kuanzisha mjadala, lakini hakumuelewa Magufuli. Sio yeye tu, wapo wengi wamekaririshwa kila anachokifanya Magufuli, kwao ni vitisho na udikteta, tatizo lipo hapa!
 
Pasco shikamoo kaka..kweli Mh Raisi ana nia njema lakini hawezi kubadilisha mambo kwa kuongea tu pasipo kufuata sheria.Mh Magu is a scorpion.ni wagumu sana kushauriwa lakini ni viongozi wazuri sana .
 
UKAWA kazi mnayo
Kusema kwamba nchi imempata dictactor ni wazo lako... kwamba rais hana haki ya kupunguza mishahara ya viongozi wa mashirika ya umma na wakala za serikali .. ina nitatiza maana ni sheria gani iliyowapa haki ya kujilipa zaidi ya uwiano kati ya kipato cha chini na cha juu.?? Kama rais ndiye aliyemteua mtu ambaye sasa anayo haki ya kujilipa Million 40 kwa mwezi kwa sababu tu ya upigaji wa hesabu za account za serikali kuwekwa kwenye benki binafsi za biashara na serikali isipate hiyo riba bali riba ikaenda kwenye kampuni binafsi nadhani tunaimba "wimbo wa maslahi ya umma" lakini tunaucheza wimbo huo kibepari/ kibinafsi"...
 
Just a reminder, kwa katiba hii nakuhakikishia yeye ndiyo the big Boss.
Mfano akatekeleza utampeleka wapi mahakamani!? Maana ukileta kivimbisha misuli utapigwa chini na wengine wanaitamani hiyo 15m ujue. Niajabu na kweli Mashirika mengi ya uma yamekuwa yakijiendesha kwa hasara huku watu wakipokea vinua mgongo vya wale wanaofanya vitu vinavyoonekana.40m ujue ni kinua mgongo hicho kwa mtu anayestaafu kwa kulitumikia taifa 30yrs kwa uaminifu, wakati mtu anayeua shirika la uma akiipata kwa mwezi mmmh.
Mimi nadhani ikiwa huyo Mkurugenzi amefanikiwa kurifanya shirika,taasisi,etc lijiendeshe kwa faida kubwa basi ni haki yake kulipwa vizuri.
Nia ya JPM ni njema ingawa itambidi kubadili baadhi ya kanuni,sheria na taratibu kupitia vyombo husika.
 
Nilijua kwamba labda umekuja na kifungu cha sheria kinachosema

" Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania hana mamlaka ya.... "

Teh teh, umeenda kanisan?

najua ule mchepuko umepigwa panga ila sio mbaya sana, vumilia tu

Kama bwana Pasco anataka kupima kina cha maji kwa mguu basi kama nimtumishi wa uma basi akwee pipa kwa fedha ya serikali kwenda nje bila ruhusa ya JPM maana katazo haliko ktk sheria,kanuni na taratibu.teh the teh
 
Nimeona mtoa hoja hapo amejichanganya vya kutosha kama vile hajui anachoongea.
1. Anafananisha uchumi wa Tanzania na Marekani (yaani nchi ya kwanza duniani kwa utajiri na ya mwisho kwa umaskini) Hata tofauti haoni? Hata hivyo sishangai kwa utamaduni uliokuwepo huko Tanzania kulinganisha kila kitu na Marekani.....mbona haulinganishi uwajibikaji uliopo hapa na huko Tanzania kuona kama kweli wanaolipwa hicho kima wanastahili?
2. Magufuli (mimi sio mshabiki wake) amesema wafanyakazi wa serikali na mashirika yake (parastatal organization-kama vile NSSF, PPF, TAWIRI, TANAPA,NHC, N.K, N.K) kuwa mishahara yao itapunguzwa na wasiotaka waondoke- rais kama kiongozi wa nchi ndiyo mkubwa wa serikali yaani kwa maana nyingine ni zaidi ya CEO wa serikali mwenye maamuzi ya mwisho ambayo hayawezi kuingiliwa na aina yoyote ya board of directors au yoyote yule. Hivyo uamuzi wa mwisho ni wake kwa mujibu wa katiba, hivyo akisema anapunguza mishahara yupo sawa, akisema anapunguza wafanyakazi hakuna wa kumwingilia au kumzuia.
3. Mwandishi anafaninisha serikali na viongozi wa makampuni ya GE, GC,Walmart, GM, Microsoft na mengineyo ya hapa Marekani. KAKA UNAKOSEA SANA UTACHEKWA KAMA HUJACHEKWA BADO. Haya makampuni hayahusiki na serikali na wala serikali haina aina yoyote ya hisa kwenye kampuni hizi hata zile zinazotengeneza vifaa vya kijeshi kama Lockheed Martin, GD au Northrup Grumman, haya yanalipa kodi kama kawaida, uhusiano wake na serikali ya hapa ni pale yanapotaka kuuza silaha nchi za nje zinatakiwa ziwe na kibali cha serikali. Sasa kama ni mashirika binafsi wana haki ya kupanga kumlipa kiasi chochote mkubwa wake wa kampuni bila kuulizwa na serikali ili mradi wanalipa kodi stahiki.Mashirika ya serikali kama EPA na mengineyo mengi ya hapa yanatumika mishahara ya scale ya serikali ambayo ni mdogo sana kulinganisha na mashirika binafsi madogo kama ya radio na TV's za States tofauti.
4. Mengi ya mashirika makubwa kama TOYOTA, MACY's, Marriot,Microsoft n.k na mengineyo uliyoyataja ni ya kifamilia, hivyo hata CEO's wake wanayamiliki wenyewe hivyo usitegemee walipwe fedha kiduchu....unategemea ujilipe kidogo kwa mali yako? Au unaangalia na ku-project faida utakayoipata ndiyo ujipangie mshahara wako? Ma-CEO wa makampuni binafsi hawaongozwi na boards au hata kama boards zipo zinakuwa na ndugu watupu wengi wakiwa share holders.
5. Makampuni katika nchi tajiri yanatumia mfumo wa hisa ambazo zinagawanwa kwa kadiri ya faida iliyopatikana, hivyo mengi yanatengeneza faida ya kutisha hivyo migawanyo yao ya fedha inakuwa mikubwa
6 Kwa serikali na nchi yetu tunategemea zaidi kwenye faida ambayo inazalishwa kwa kuzungushwa kwa fedha aidha za serikali au za wafanyakazi siyo mtaji uliopatikana kama inavyokuwa kwa makampuni binafsi.......SASA KWA NINI TUWAZAWADIE WAFANYAKAZI AMBAO HAWAKUTOA JUHUDI ZAO KATIKA KUTAFUTA MITAJI NA HAWAKUANZISHA MAKAMPUNI YAO WENYEWE BALI TUNAWALIPA MALIPO MAKUBWA KWA KAZI AMBAZO WAO NI WAAJIRI WA SERIKALI KAMA WENGINE?

HITIMISHO:
Wanaolipwa fedha nyingi na makampuni makubwa ...aidha wanayamiliki au ni mali ya familia zao, changamoto walizonazo ni kubwa ambazo ni pamoja na kutafuta fedha kwenye mabenki, kutafuta masoko na mambo mengine mengi ambayo unapaswa kuyafanya ukiwa na mali yako binafsi. Sasa hawa wenzetu mnaotaka walipwe sawa na makampuni binafsi ya nje, wanapata fedha serikalini au kwenye mifuko ya jamii huku serikali ikiwa guarantor, wanafanya kazi kwa kufuata plan ya serikali iliyowekwa na wataalam wa serikali, SASA TUWALIPE MAMILIONI HAYO KWA MWEZI SAWA NA MASHIRIKA BINAFSI KWA MIPANGO IPI? Magufuli yupo sawa kukata hiyo mishahara na asiyetaka aache kazi.
 
Naomba kuuliza Magufuli alisema atapunguza mishahara mwezi gani? Huu wa nne au wa tano? Ili ikifika huo mwezi aliosema tucheki kama kapunguza kweli au ilikuwa kauli ya kutaka sifa tu za kisiasa
 
Umeongea meeengi na mifano miiiiingi,
Hebu nikuulize, hiyo kampuni ya Microsoft ya Marekani au Toyota ya Japani ni kampuni za SERIKALI?
Ni watumishi wa Umma wale?

Tuanzie hapo kwanza hlf tutaendelea.
 
Wanabodi,

Kufuatia kazi nzuri inayofanywa na rais wetu, Dr. John Pombe Magufuli, ya utumbuaji majipu ya rushwa, ufisadi na uzembe, imefikia wakati baadhi yetu kumuona Rais Magufuli kama Mkombozi, kama Masiya, kama Malaika, kama Nabii, na bado kidogo tuu kuna wenzetu, wanaweza kumuona kama ni Mungu Mtu, hivyo wanataka kumuabudu, hivyo ukisema chochote against Magufuli, kwa waabudu hawa, utaonekana kama umekufuru!, hivyo watakushukia kwa nguvu zote, hili likitokea kwenye uzi huu, mjue nililijua.

Ukweli Dr. John Pombe Magufuli ni rais wetu, yeye sio bosi wetu, bali ni mtumishi wetu, sisi wananchi ndio mabosi wake, sisi ndio tumemuajiri hiyo kazi ya urais kwa kura zetu, sisi ndio tunaemlipa mshahara wake kwa kodi zetu, hivyo sisi ndio waajiri wake, na ndio tunaemlisha na kumvisha na kumfanya aishi, yuko pale ikulu kwa ajili yetu sio kwa ajili yake!, tena yeye ni binadamu, sio Mungu, sio nabii na sio malaika, hivyo kama binadamu pia anaweza kufanya makosa kama binadamu mwingine yoyote, hivyo kumkosoa kwa nia njema (in good faith), ni kitu kitu, na ukosoaji huo, unakuwa ni constructive criticism unakosoa kuwa kitu hiki ni wrong, pia unaweka ushauri wa the right thing to do!.

Nchi yetu ni nchi inayofuata katiba na inaendeshwa kwa misingi ya sheria, "the rule of law" kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni, hakuna aliye juu ya sheria, hata rais hayuko juu ya sheria, hivyo kuna baadhi ya kauli za rais wetu, kiukweli ni kauli za kibabe tuu, vitisho na kidikiteta, lakini tukija kwenye utekelezaji wa kauli hizi, zitatekelezwa kwa kuzingatia sheria taratibu na kanuni, hivyo hazitatekelezwa kama rais alivyotamka, au kama anavyotaka kuwaaminisha Watanzania.

Moja ya kauli hizi za vitisho na kidikiteta, ni kauli ya rais Magufuli, aliyoitoa akizungumza na wananchi wa home base yake kule Chato, kuwa atapunguza mishahara ya wale wanaopata mishahara minono na kuwaongezea wanaopata mishahara midogo. Miongoni mwa maneno aliyoyasema ambayo mimi nayaita ni kauli za vitisho na kidikiteta ni pale aliposema alipotolea mfano Mtanzania mmoja analipwa Shilingi milioni 40 kwa mwezi, huku Mtanzania mwingine akilipwa Shilingi 150,000, na kusema wanaishi kama peponi!. Amesema "nitahakikisha hakuna Mtanzania analipwa mshahara wa zaidi ya shilingi milioni 15!, mimi nimesema, mimi sio ndio rais!, nikisema nitafanya, nitafanya, kama kuna asiyetamka mshahara huo wa milioni 15, afungashe aende zake, kuna Watanzania wengi wenye uwezo, nawanaohitaji hizo kazi"!.

Kauli hii, ya rais imeshangiliwa sana na kuwapa wasiwasi wenye mishahaa minono, huku wakiwapa matumaini makubwa wenye mishahara duni, hii imewapa kitu kinachoitwa "Great Expectation" kuwa the gap kati ya wenye nacho na wasiona nacho, itapungua, matokeo yake, isipokuja kupungua, hawa wenye great expectations wataishia kupata a great despair.

Rais wa nchi ndie mtu mwenye mamlaka kuu kuliko mtu mwingine yoyote, lakini mamlaka hiyo, inatawaliwa na sheria, taratibu na kanuni, ambapo kiukweli, rais wa nchi, hana mamlaka yoyote kisheria, kikanuni au kiutaratibu, kupanga mshahara wa mtu, wala hana uwezo wowote kisheria kupunguza mshahara wa mtu yoyote, hivyo kauli ya Magufuli kuwa atapunguza mishahara, ni kauli ya kibabe tuu na kidikiteta, rais hana uwezo huo wala hana mamlaka hayo!. Ufike wakati viongozi wa kisiasa wasiachwe kutoa kauli za matumaini hewa, wakati hawana uwezo huo kisheria!. Nadhani hata Magufuli alipotoa kauli hiyo, aliitumia ile hulka yake ya "udikiteta" akijijua yeye ndio rais, hivyo yeye ndio kila kitu, akisema, amesema, kiukweli, ukweli halisi, rais sio kila kitu, rais yuko chini ya katiba, yuko chini ya sheria, na anabanwa na sheria, taatibu na kanuni!.

Niliwahi kuwa mtumishi wa umma, kanuni za utumishi wa umma, zinatambua kitu kinachoitwa "a legitimate expectation", yaani kama umeajiriwa kwa mshahara fulani, na ukawa unalipwa ujira huo, then hakuna mamlaka yoyote inayoweza kuupunguza ujira huo!. Hivyo hata rais hana mamlaka ya kupunguza mishahara yoyote inayolipwa kisheria, zile kauli za asietaka na aende, ni vitisho tuu na udikiteta!.

Kiukweli hii mishahara ambayo rais Magufuli ameiita ni mishahara ya peponi, kweli ni mishahara mikubwa, ila kwenye corporate world, ni mishahara ya kawaida kabisa, hata nchini Marekani, ma CEO wa makampuni makubwa, kama GM, GE, Microsoft, etc, wanalipwa mishahara mikubwa kuliko Obama. Hata Japan, rais wa TOYOTA analipwa mshahara mkubwa kuliko Waziri Mkuu wa Japan, hali ndio hivyo duniani kote, ila pia hii mishahara mikubwa ya Tanzania, sio kukubwa kivile kimataifa, ila ni kweli mishahara ya kima cha chini Tanzania, ni midogo kabisa ya level ya inhumane kutokana na umasikini wa taifa uliotopea, sasa umasikini huu, usitufanye kuwaadhibu wele wenye eheueni nao lazima waishi kwenye lindi la umasikini, badala ya kugawana utajiri, sisi tunagawana umasikini!.

Lengo la Magufuli kupunguza mishahara minono ni lengo jema kwa lengo la kufanya kitu kinachoitwa "standardization and harmonization" kwa ku "bridge the gap" kati ya the highest paid na the lowest paid, lakini harmonization haifanywi kwa kuwapunguzia wenye vipato vya juu, bali hufanyika kwa kuwapigisha "mark time", kuwasimamisha hapo walipo, na kuwainua wengine hadi wawakaribie!. Kwenye kanuni za utumishi, hakuna kitu kinachoitwa kupunguza mishahara!.

Kwa vile hiyo mishahara imepangwa kwenye strructures za mashirika hayo, kitu ambacho Magufuli anaweza kufanya, ni kwanza kuvunja hizo structures kuwaandikia barua za kuwaachisha kazi wafanyakazi wote wanaolipwa viwango vikubwa na kuwalipa haki zao zote, kisha kuvunja stucture na kutoa structure mpya yenye hizo salary scale za Magufuli, na kuwataka wale wote wenye nia ya kuendelea na scale hizo mpya za Magufuli, waombe kazi upya na kuajirriwa upya kwa scale mpya za Magufuli.

Sasa mtu aliyekuwa analipwa milioni 40 akiishandikiwa kustaafishwa, atachukuya barua yake ya kustaafu atalamna mafao yake na "golden handshake yake", kisha ataendelea kula pensheni yake ya 60% ya milioni 40 hivyo kuvuta milioni yake 24 kila mwezi, na kuachana na hiyo milioni 15 ya Magufuli, unless kama huu udikiteta wa Magufuli utaingizwa hadi kwenye mifuko ya pensheni, kwa kuiamuru mifuko hiyo kutoa pensheni ya ceiling ya mshahara wa milioni 15 tuu kwa kila pensioner hata kama ameastaafu na mshahara wa milioni 40!.

Namalizia kwa kumpongeza rais wetu, kwa kuwa na nia njema na Watanzania, ila namtahadharisha sana kuchunga kauli zake, haswa hizi kauli za kidikiteta na vitisho kwa lengo la kuleta matumaini chanya, kabla ya kauli hizo, ni vema aki consult wataalamu na washauri, kuhusu uwezekano wa kuwezekanika, ndipo atoe matumaini hayo, vinginevyo ni kuwapa Watanzania matumaini hewa!.

Nawatakia Jumapili Njema.

Pasco.
Kwa wageni na maandishi ya Pasco wa jf, unaweza kupitia nyuzi hizi ili uweze kujua huwa ninamsimamo gani kumhusu Magufuli.
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?.
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata .

Japo ni Dikiteta, Rais Magufuli ni Simple, Genuine & Down To E
JF Modes, Magufuli ni Rais Wetu, Asiabudiwe, Asiogopwe, Bali
Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria ...
If you can't beat them, join them! He is the worst dictator.
Katazo la Rais Kusafiri Nje ya Nchi bila Vibali: Je, Halikiuki Haki za Binaadamu...
Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 ni John Pombe Magufuli
Magufuli Kama Nyerere:Ni Mtu wa Watu, Hapapasi, Hamung'unyi
Yajue Makundi 10 Top Ten wa CCM, Ambamo Watatoa Top 5,

Kama Magufuli Anaangalia Clouds TV na Kuipongeza, Kunatum
ENL, CHADEMA na UKAWA, Tuyakubali Matokeo!,

Ushauri wa Bure Kwa Lowassa: Kwa Vile ni Magufuli, Kubali M
Ushauri wa Bure kwa Lowassa: Hata kama ni kweli uliibiwa kur

Mimi sina uhakika km jamaa anaelewa anachokifanya serikali yake haueleweki....
 
Pasco is back!Umemwaga madini tupu!Kwanza mimi naona ni mambo ya ajabu mtu kila siku anasema mimi ndo rais! mimi ndo rais! hiyo kauli inakera sana. Anamwambia nani asiyejua? Au kuna watu huwa anawaogopa kuwa wana nguvu kuliko yeye hivyo anatanguliza hiyo title?
 
majipu ipo siku yatajopasua yenyewe,maana yashaanza kutoboka..
Magufuli piga kazi,punguza mshahara kwa wanaolipwa mamilioni.
hiyo itsaidia kupunguza wachela pool mtaani.
hizi kelele unazozisikia usiziogope kwani ni maumivu ya jipu kupona.
endelea kuyatumbua.hadi yaishe yote.
upo kwa ajili ya watanzania na watanzania wapo nyuma yako.
usiogope sauti ya mpiga kelele wakati akikamuliwa jipi,kwani ndip kuanza kupona huko.
 
Back
Top Bottom