Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyote

Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyote

Mh.Rais ndio mwajiri ndio kila kitu Rais acha kusikia wezi hao wanajilipa mishahara ya ajabu Kwa Kazi gani?Wewe ndio kila kitu hata Leo ukisema unataka kichwa cha MTU Fulani utaletewa Mh.Punguza hiyo mishahara wametuibia vya kutosha.

Hizo kauli za Rais ndo kila kitu zitawatokea puani siku moja.
 
pasco bana,eti analinganisha mishahara ya huko marekani na japani na hapa tanzania!!!!!pasco just be honest,milioni 40 kwa mwezi unazitumiaje?yani kwa vyakula hvi tunavyokula ubwabwa,nyama,maharage umalize milioni 30 kwa mwezi?na usisahau hao watu wanalipiwa nyumba,mafuta full tank...acha utani pasco!!!!!!!mimi nimesoma kama hao na nina uwezo,kama vipi magufuli anipe hiyo kazi kwa milioni tano tu kwa mwezi...ebo!!!!wahongaji kama wewe pasco ndio mnatakaga mihela mingi...
Sponsors wa watu mjini, zile swaga "ma new ride zinaenda kwishaaaaaa
 
Mkuu watanzania wengi wana akili nzito sana sana!! Lishe duni.... Elimu mbovu na mazingira mbovu yametafuna kabisa uwezo wa kufikiri wengi wapo kama wafu tu!! MTU akisikia NHC anafikiri mishahara yao inategemea kodi kama ile ya Rais na mawaziri!!
Hahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa tabu kweli kweli
 
We need a fair and just remuneration!

Haiwezekani kwa ela ya kodi mtu alipwe 40m na mwingine alipwe 200,000 Tshs!

Hauwezekani!!!!

Ni kweli lazima kuwe na moderation na Magufuli ndio anafanya hiyo kazi. Wakati wa Nyerere alijitahidi kuweka huu uwiano lakini walipokuja walafi wakaanza kujilimbikia mapato wenyewe na jamaa zao na marafiki zao na wapenzi wao. Itakuwaje kima cha juu milioni 60 wakati kima cha chini ni 120,000 na maprofesa waliowafundisha chuoni wanapata 1,500.000
 
Mkuu Mzalendo Halisi, usemayo ni kweli kuwa we need a fair and just renumeration, kiukweli na ki haki kima cha chini ambacho ni just na fair ni TZS 1,000,000/= lakini kutokana na umasikini wa nchi, hatuna uwezo huo, hivyo usiyahukumu mashirika yenye uwezo, for the expenses ya umasikini wetu wa nchi!.

Wanaolipwa pesa za kodi, yaani Government scale ni watumishi wa serikali tuu, top salaries yao ni mshahara wa rais. Hawa wanaolipana milioni 40 ni mashirika ya umma, they make those money, wana produce hivyo ni haki yao, kula wanachovuna. Kwenye mashirika haya exception ni TRA ambao wao hawapoduce bali wanakusanya, nao wanalipana vizuri ili kuepuka vishawishi vya kupokea rushwa njaa. Hawa wakubwa wa serikali wasiopokea mishahara minono kama ma CEO wa mashirika, ndio matajiri wakubwa kuliko hao ma CEO, source za utajiri wao ni "vijisenti" kwenye cut za "the grand corruption" wakiongozwa na top wao!.

Watu wanaofuga kuku wa nyama na mayai, huwezi kuwazuia kula kuku wao na kula mayai, na badala yake uwalazimishe kushindia mihongo na kisamvu, tembele au sukuma wiki, eti tuu kwa sababu, wengine hawawezi kula kuku na mayai!.
Hii mishahara ya Magufuli, itashusha productivity!.

Pasco
Shirika la umma sio private company; ni mali ya serikali; ni uwekezaji wa serikali; halina haki ya kujimegea wanachozalisha wapendavyo; wanawajibu kwa umma kwa sababu ni mali ya watanzania wote lazima wanachofanya kizingatie maslahi mapana ya wanahisa wao kupitia Hazina; sio kutapanya wapendavyo wakawasahau wenye mtaji; ebho!
 
Hoja yako ni nzuri sana inajaribu kucheck and balance
lakini wakati huo huo inampunguzia Mh.Rais sauti kama
Amiri Jeshi mkuu kwa kuwa chochote anachokisema
kijeshi ni amri.
Mpaka hapa tulipofikia ni dhahili wengi wetu tutakubaliana
kwa 100% chochote anachokisema Mh.Rais kwa kuwa
hakuna kiongozi yeyote tokea uhuru aliyethubutu
kukemea serikali hasa kwenye mapato na matumizi ya serikali.

Kasi iliyopo na matatizo ya watanzania kwa sasa tumeanza
kujifunza vitu vingi sana na kurejea historia juu ya taifa letu na
kutupelekea kumuona Mh.Rais kama mkombozi wa kweli.

Utu na umoja wetu ulikwishaanza kupuuzwa,kudhauliwa
na kunyanyapaliwa na mabepari wachache ambao wengine
taifa liliwatengeneza wenyewe lakini wakasahau walikotoka
na kuanza kufuja na kutapanya mali ya umma.

Baadhi yetu tumesahau uchaguzi ulikwisha na kinachokiwa ni kufanza
kazi,lakini hapa tunaanza kuhoji kazi inayofanywa na kuingiza haki
za mambo ya uchaguzi na utendaji wa serikali hii si sawa.

Ni wakati wa si kujihoji tu bali tuangalie matatizo yetu yanasababishwa na
nini na kwanini ni sisi tu mbona wengine wanasonga mbele?.

Na kama tatizo ni mishahara mikubwa mikubwa lakini hakuna kazi yoyote
inayofanyika nini kifanyike na kwanini tufanye hivyo kwa faida ya nani?

Ningemshauri tu Mkuu Pasco,"kuwa kabla ya kuhoji uhalali wa mkuu wa nchi
kuingilia bajeti ya serikali yake hasa kwenye matumizi/mishahara, ni vyema
akamshauri/kumuuliza nini hasa madhumuni ya kupunguza mishahara
na kwanini iwe sasa,kwa faida ya nani na ili iweje"?.
 
Kwa elimu ipi au uzoefu upi tukupe milioni 40?
Kazi ni moja tu ya kumfanya malaika aishi kama shetani
 
Pasco,uliyoeleza ni mambo ya msingi sana,lkn kwa mujibu wa katiba yetu tuliyonayo mi naona Rais yuko juu ya sheria

Kwnza cjui km tuna mahakama ya katiba!!!!,kwa udhaifu wa katiba Magufuli anaweza kusema lolote na ucwe na mahali pa kumhoji zaidi ya mtandaoni km hapa,tena ukifanyamchezo wakukamate.

Unafikiri leo hata akapunguza hyo mishahara mikubwa nani atamuuliza c mtaishia kumshitaki mwanasheria mkuu wa serikali,mahakama zenyewe c huru raisi ndio anateua jaji mkuu itakuwaje huru?

Kwa ujumla Magufuli anaweza asiwe dkteta,ila amegundua udhaifu wa katiba so ndo anapita huko kujiongezea umaarufu,coz hamtamwambia kitu,kumbuka Kauli yake"mm nimesema mi c ndio Rais?"anahoji,bila shaka hata ww ungesema ndiooooo!!!!!
 
Mtu akijiona anastahili m40 mshahara kwa mwezi, atoke kwenye mashirika ya umma akaombe kazi kwa Bakhresa, mengi au aende huko Toyota, fb, google na kwingineko atapata hiyo pesa na kuzidi, atuachie mashirika ya Umma. watu wanalipwa mapesa lukuki na wizi, ufisadi na rushwa hawaachi na wengine hata kazi zao hazionekani wanafanya nini kwenye hayo mashirika. waje wazalendo watakaokubali kufanya kazi kwa ujira wa TGS.
 
Nilijua kwamba labda umekuja na kifungu cha sheria kinachosema

" Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania hana mamlaka ya.... "

Teh teh, umeenda kanisan?

najua ule mchepuko umepigwa panga ila sio mbaya sana, vumilia tu

 
Haya Mashirika ya umma kama yanazlisha wasianze kujigawia "jikoni" wapeleke kwenye common basket then tugawane wote tulichokipata.

Uchumi wa Nchi ukiruhusu wote tutapata mishahara ya peponi ila kwa sasa tujibane kwa kidogo tulicho nancho.

Sio undugu jirani yako analipwa laki na nusu anashindwa hata kulips kodi na wewe unalipwa mil 40 na marupurupu juu unashindwa hata pa kuyapeleka.

Kulipana 40M na wengine laki na nusu sio equity.
 
Leo umetoa thread yenye akili sana ni matumaini yangu kuwa mzee wa majipu ataufanyia kazi ushauri huu, alaaniwe mtu yeyote atakayepinga ushauri huu, amen
Ni kweli thread yenye akili, na hii sio ya kwanza kutolewa na mleta uzi.
Tatizo lililopo ukawa na ccm mnachagua ipi mzuri na ipi sio nzuri. Ikiwa upande wako ni nzuri na isipokuwa upande wako sio nzuri. Inasikitisha sanataifa imefika wakati watu wanaendeshwa na hisia tena za kisiasa. Sio wewe tu, ni watanzania wengi tena wale wanaoitwa taifa la leo na hata la kesho.
 
Comrade Pasco mbona mfano wako umelinganisha na kampuni binafsi kama Microsoft.. Kwani hiyo ya serikali.. Kwani umesikia Magufuli anataka mishahara ya kampuni ya Bakharesa ipungue

Hata mimi nimemshangaa sana Pasco kwa mfano wake wa kulinganisha taasisi binafsi za Marekani/Japan na za umma Tanzania. Wala hakuwa na sababu ya kwenda mbali huko, hivi anajua Meneja potelea mbali Director au MD wa ACACIA (zamani Barrick) analipwa USD ngapi? Ofisi zao ziko pale Victoria, DSM angeenda tu pale akapata data.
 
Comrade Pasco mbona mfano wako umelinganisha na kampuni binafsi kama Microsoft.. Kwani hiyo ya serikali.. Kwani umesikia Magufuli anataka mishahara ya kampuni ya Bakharesa ipungue

Kwa kusaidia mjadala, hapa chini ni mishahara ya baadhi ya wakurugenzi wa mashirika ya umma nchini Uingereza ambao wanalipwa mishahara mikubwa kuliko waziri mkuu wao. Inasemekana kuna wafanyakazi wa serikali kama 250 wanalipwa zaidi ya waziri mkuu wao ambaye analipwa pounds 142,500 kwa mwaka. Hapa tunaongelea wafanyakazi wa serikali tu.

Baadhi ya hao wafanyakazi na mishahara yao ya mwaka:
1.Chief executive of the nuclear decommissioning Authority pounds 379,999 kwa mwaka
2. Former chief Executive of the Olympic delivery agency pounds 310,000 kwa mwaka.
3. Chief executive of the Civil Aviation Authority pounds 260,000 kwa mwaka
4. Chief Executive of the Technology Strategy board pounds 254,999 kwa mwaka
5. Chief executive of the higher Education Funding Council pounds 234,999 kwa mwaka.

kuna wengine kama 30 kwenye shirika lao la afya wanalipwa zaidi ya waziri mkuu. Mamlaka ya anga kuna wafanyakazi zaidi ya 10 wanalipwa zaidi ya PM.

Mshahara wa chini nchini uingereza iko kwenye pounds 15,000 kwa mwaka. Mishahara ya kati ambayo watu zaidi ya nusu ndio wanapata haifiki 25,000 kwa mwaka.

Mshahara wa waziri mkuu ni 142,500 pounds. Mawaziri wanalipwa pounds 134,565. Wabunge wanalipwa pounds 74,000.
 
Naona Magu atashindwa mapema sana, lengo lake sio baya lkn anaonakana Ana haraka sana ya mabadiliko. Anataka Tanzania tukilala tukiamka tuone Tumepiga hatua Mbele. Kama anavosema mwenyewe tumechelewa sana. Ni kweli tumechelewa lkn Ajue tu hata yeye hawezi kuifanya Tanzania ikawa Kama South kwa miaka5 Ni ngumu sana. Na athari yake Itakuwa ni kubwa kuliko faida.

Kauli hizi si njema kuzitumia kwenye jamii, niliandika hapa kuwa atajitengenezea maadui ndani yake. Kwakua anatumia hii nafasi Kama yeye. Anachotakiwa kufanya Mh. Rais Abadilishe mfumo mzima wa system ya Madaraka,vyeo, mishahara, likizo, Na uajiri. Haya yote yanafanywa si kwa ajili ya Magu tuu, yafanywe kwa ajili ya Taifa hili miaka 50 ijayo. Hapa naweza kusema badala ya kutumia kauli Kama hizi tutumie Katiba Na sheria kali ili kufikia Kama wenzetu.

Ninavoamini kwa Nchi hii inavoendeshwa kisiasa Ni shida hata kupatikana hiyo Katiba bora, hawa Waafrika kwa wenyewe tuu KUkaa wakatulia Na kuiandika na kuikubali Katiba hiyo hawatoweza hata siku moja mpk wasubiri wauwane kwanza Ndio watakuja kufanya hayo kwa sindikizo. Namshauri Mh.rais wetu, Yale maendeleo unayoyaona kwa mfano south Afrika sio mzulu aliyefanya yale mpk Nchi ikaonekana imefika pahali Pazuri Na system nzuri. Wazungu wapo pale, cha kufanya omba msaada wa wataalam wa israil, ama uk waje wakuwekee system itakayokua haifungamani Na siasa Zenu. Hili wengine watalisemea sana lakini faida yake itakua Ni kubwa kuliko athari yake.

Siliamini bunge letu kwa linavoendeshwa kisiasa Kama litatusaidia hata Na Mh. Aliliona hilo.
 
Back
Top Bottom