Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 52,685
- 119,325
Wanabodi,
Kufuatia kazi nzuri inayofanywa na rais wetu, Dr. John Pombe Magufuli, ya utumbuaji majipu ya rushwa, ufisadi na uzembe, imefikia wakati baadhi yetu kumuona Rais Magufuli kama Mkombozi, kama Masiya, kama Malaika, kama Nabii, na bado kidogo tuu kuna wenzetu, wanaweza kumuona kama ni mungu mtu, hivyo wanataka kumuabudu, hivyo ukisema chochote against rais Magufuli, kwa waabudu hawa, utaonekana kama umekufuru mungu!, hivyo watakushukia kwa nguvu zote, hili likitokea kwenye uzi huu, mjue nililijua kabla. Wako wenzetu humu wameisha anza kumuabudia rais Magufuli na kumuita ni Alfa na Omega.
Mkuu Mzee Mwanakijiji, Rais Magufuli Sio Alfa na Omega. Rais Sio ...
Kati ya Rais wa Nchi na Wananchi, Who is The Boss, and the Real Boss?.
Ukifungua katiba ya JMT, inaanza na maneno "We the people...", hivyo ingawa Dr. John Pombe Magufuli ni rais wetu, yeye sio bosi wetu, yeye ni bosi wa viongozi, watumishi wa umma na wateule wake, kwetu sisi wananchi wa kawaida, rais wa nchi sio bosi wetu bali ni mtumishi wetu, sisi wananchi (we the people), ndio mabosi wake, sisi ndio tumemuajiri hiyo kazi ya urais kwa kura zetu, sisi ndio tunaemlipa mshahara wake kwa kodi zetu, hivyo sisi ndio waajiri wake, na ndio tunaemlisha na kumvisha na kumhudumia kwa kila kitu, tena mshahara wake haukatwi kodi ili kumfanya aishi kwa starehe, yuko pale ikulu yetu kwa ajili yetu sisi we the people na sio kwa ajili yake!, tena yeye ni binadamu, sio Mungu, sio nabii na sio malaika, hivyo rais Magufuli kama binadamu, kikukweli kabisa, ni rais bora kupata kutokea kwa nchi yetu Tanzania, ila kwa vile ni binadamu na sio malaika, rais pia anaweza kufanya makosa kama binadamu mwingine yoyote, hivyo kumkosoa rais kwa nia njema (in good faith), ni kitu kizuri kitakacho mjenga, na ukosoaji huo, unakuwa ni constructive criticism unakosoa kuwa kitu hiki ni wrong, pia unaweka ushauri wa the right thing to do!.
Nchi yetu ni nchi inayofuata katiba na inaendeshwa kwa misingi ya sheria, "the rule of law" kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni, hakuna aliye juu ya katiba na sheria, hata rais hayuko juu ya katiba na sheria, hivyo kuna baadhi ya kauli za rais wetu, Mhe. Dr. John Pombe Magufuli, kiukweli ni kauli zinazoashiria kuwa yuko juu ya katiba, baadhi ya kauli hizo ni za kibabe, vitisho na kidikiteta, lakini tukija kwenye utekelezaji wa kauli hizi, zitatekelezwa kwa kuzingatia sheria taratibu na kanuni, hivyo hazitatekelezwa kama rais alivyotamka, au kama anavyotaka kuwaaminisha Watanzania.
Moja ya kauli hizi za rais Magufuli, ni aliyoitoa akizungumza na wananchi wa home base yake kule Chato, kuwa atapunguza mishahara ya wale wanaopata mishahara minono na kuwaongezea wanaopata mishahara midogo. Miongoni mwa maneno aliyoyasema ambayo mimi nayaita ni kauli za vitisho ni pale aliposema alipotolea mfano Mtanzania mmoja analipwa Shilingi milioni 40 kwa mwezi, huku Mtanzania mwingine akilipwa Shilingi 150,000, na kusema wanaishi kama peponi!. Amesema "nitahakikisha hakuna Mtanzania analipwa mshahara wa zaidi ya shilingi milioni 15!, mimi nimesema, mimi sio ndio rais!, nikisema nitafanya, nitafanya, kama kuna asiyetamka mshahara huo wa milioni 15, afungashe aende zake, kuna Watanzania wengi wenye uwezo, nawanaohitaji hizo kazi"!.
Kauli hii, ya rais imeshangiliwa sana na kuwapa wasiwasi wenye mishahaa minono, huku wakiwapa matumaini makubwa wenye mishahara duni, hii imewapa kitu kinachoitwa "Great Expectation" kuwa the gap kati ya wenye nacho na wasiona nacho, itapungua, matokeo yake, isipokuja kupungua, hawa wenye great expectations wataishia kupata a great despair.
Rais wa nchi ndie mtu mwenye mamlaka kuu kuliko mtu mwingine yoyote, lakini mamlaka hiyo, inatawaliwa na sheria, taratibu na kanuni, ambapo kiukweli, rais wa nchi, anayo mamlaka ya kisheria, kikanuni au kiutaratibu, kupanga mshahara wa mtumishi yoyote, lakini hana mamlaka wala uwezo wowote kisheria. kikanuni na kiutaratibu, kupunguza mshahara wa mtumishi yoyote, hivyo kauli ya Magufuli kuwa atapunguza mishahara, ni kauli ya ubabe tuu wa rais hana uwezo huo aliodhani anao, wa kupunguza mshahara wa mtu!.
Ufike wakati viongozi wa kisiasa wasiachwe kutoa kauli za kisiasa za kujenga matumaini hewa, wakati hawana uwezo huo kisheria!. Nadhani hata rais Magufuli alipotoa kauli hiyo, aliitumia ile hulka yake ya "udikiteta" akijijua yeye ndio rais, hivyo yeye ndio kila kitu, akisema, amesema, kiukweli, ukweli halisi, rais sio kila kitu, katiba ndio kila kitu, rais yuko chini ya katiba, yuko chini ya sheria, na anabanwa na sheria, taratibu na kanuni!.
Niliwahi kuwa mtumishi wa umma, kanuni za utumishi wa umma, zinatambua kitu kinachoitwa "a legitimate expectation", yaani kama umeajiriwa kwa mshahara fulani, na ukawa unalipwa ujira huo, then hakuna mamlaka yoyote inayoweza kuupunguza ujira huo!. Hivyo hata rais hana mamlaka ya kupunguza mishahara yoyote inayolipwa kisheria, zile kauli za asietaka na aende, ni vitisho tuu na udikiteta!.
Kiukweli hii mishahara ambayo rais Magufuli ameiita ni mishahara ya peponi, kweli ni mishahara mikubwa, ila kwenye corporate world, ni mishahara ya kawaida kabisa, hata nchini Marekani, ma CEO wa makampuni makubwa, kama GM, GE, Microsoft, etc, wanalipwa mishahara mikubwa kuliko rais Obama. Hata Japan, rais wa TOYOTA analipwa mshahara mkubwa kuliko Waziri Mkuu wa Japan, hali ndio hivyo duniani kote, ila pia hii mishahara mikubwa ya Tanzania, sio mikubwa kivile kimataifa, ila ni kweli mishahara ya kima cha chini Tanzania, ni midogo kabisa ya level ya inhumane kutokana na umasikini wa taifa uliotopea, sasa umasikini huu, usitufanye kuwaadhibu wale wote wenye eheueni nao lazima waishi kwenye lindi la umasikini, badala ya kugawana utajiri, sisi tunagawana umasikini!.
Lengo la rais Magufuli kupunguza mishahara minono ni lengo jema kwa lengo la kufanya kitu kinachoitwa "standardization and harmonization" kwa ku "bridge the gap" kati ya the highest paid na the lowest paid, lakini harmonization haifanywi kwa kuwapunguzia wenye vipato vya juu, bali hufanyika kwa kuwapigisha "mark time", kuwasimamisha hapo walipo, na kuwainua wengine hadi wawakaribie!. Kwenye kanuni za utumishi, hakuna kitu kinachoitwa kupunguza mishahara!.
Kwa vile hiyo mishahara imepangwa kwenye strructures za mashirika hayo, kitu ambacho rais Magufuli anaweza kufanya, ni kwanza kuvunja hizo structures kuwaandikia barua za kusudio la kuwaachisha kazi wafanyakazi wote wa umma wanaolipwa viwango vya mishahara zaidi ya milioni 15 na kuwalipa haki zao zote, kisha kuvunja stucture na kutoa structure mpya yenye hizo salary scale za Magufuli, na kuwataka wale wote wenye nia ya kuendelea kazi kwa viwango vipya na scale hizo mpya za Magufuli, waombe kazi upya na kuajiriwa upya kwa scale mpya za Magufuli.
Sasa mtu aliyekuwa analipwa milioni 40 akiishandikiwa kustaafishwa, atachukuya barua yake ya kustaafu atalamba mafao yake na "golden handshake yake", kisha ataendelea kula pensheni yake ya 60% ya milioni 40 hivyo kuvuta milioni yake 24 kila mwezi, na kuachana na hiyo milioni 15 ya Magufuli, unless kama huu udikiteta wa Magufuli utaingizwa hadi kwenye mifuko ya pensheni, kwa kuiamuru mifuko hiyo kutoa pensheni ya ceiling ya mshahara wa milioni 15 tuu kwa kila pensioner hata kama ameastaafu na mshahara wa milioni 40!.
Namalizia kwa kumpongeza rais wetu, kwa kuwa na nia njema na Watanzania, ila namuomba sana rais Magufuli asitoe sugar coating statements zenye kuleta matumaini makubwa kama mabomba nchi nzima, kutoa maziwa na asali kwa lengo la kuleta matumaini chanya, kabla ya kauli hizo, ni vema aki consult wataalamu na washauri, kuhusu uwezekano wa kuwezekanika, ndipo atoe matumaini hayo, vinginevyo ni kuwapa Watanzania matumaini hewa!.
Nawatakia Jumapili Njema.
Pasco.
Update
Wandugu, rais Magufuli nimevulia kofia!, kumbe ni kweli amechinja mishahara hadi mshahara wa Gavana amefyeka!. Siku aliposema atapunguza mishahara isizidi TZS milioni 15, mimi ni miongoni mwa ma Tomaso wa humu, tulibisha na kubeza kuwa rais hawezi kupunguza mshahara wa mtu, kwa sababu hana mamlaka hayo.
Leo akihutubia jumuiya ya Chuo Kikuu, amethibitisha amefyeka mishahara ya peponi, na hakuna aliyeacha kazi kwa kupinga mishahara mipya ukiwemo mshahara wa Gavana ambao nao ameupiga panga, tena almanusura angeutaja, wastaarabu wakampooza kuwa ni kumdhalilisha gavana kusema anavuta ngapi, ila mshahara wake ameendelea kuutaja kuwa kuwa anavuta just TZS 9,500,000!.
Kuanzia sasa, namuaminia rais Magufuli, chochote atakachosema atafanya, kiukweli atafanya regardless katiba, sheria, taratibu na kanuni zinasemaje, the end justify the means, amesema, ametenda na ameweza.
Hongera rais Magufuli.
Paskali