Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Rais ndiyo Nembo

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,597
215,272
"Mtu anasimama analalamika eti sina mahusiano mazuri na Nchi za Ulaya kwani ni lazima mtu kwenda huko Ulaya, hata sasa kuna mkutano wa umoja wa mataifa nimesema siendi nitatuma Mabalozi wetu wakatuwakilishe huko na ndiomaana tukawaweka huko watuwakilishe"

"Ningekuwa sina mahusiano mazuri je ningechaguliwa kuwa mwenyekiti wa SADC, mimi nitabakia hapa hapa kuwapambania Watanzania wanyonge walionipigia kura sio lazima kwenda huko Ulaya " Dkt. Magufuli CHATO

1600150441261.png

Wewe ndiye Rais wetu, uliechaguliwa kwa matokeo ya uchaguzi. Tulitegemea utakua unaiwakilisha nchi katika mikutano ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na pia Umoja wa Afrika. Matokeo yake uliwatuma wateule na wasaidizi wako. Tunahitaji Rais atakaetuwakilisha kwenye mikutano. Hatukuchagua mwari wa kukaa ndani.
 
Kwa hiyo akiwawakilisha ndo mtapata maendeleao? Acheni Raisi afanye kazi za watanzania! Wanaopishana kila siku kwenye ndege wanapata nini! Hivi nyie watu hamjui raisi akisafili anatumia bilioni ngapi? Msione madaraja ya bil 700 kwenye maji yanajengwa hela zinatoka huko huko mh anapobana matumizi ya safari
 
Uenyekiti wa jumuia ya sadc si wa kuchaguliwa, ni wa zamu. Ukikufikia unapokea kijiti. Mwakilishi hana maamuzi mpaka awasiliane na aliemtuma. Mikutano ina ngazi za wahusika. Kukacha kwenda na kutuma wajumbe kuna tatizo, na hasa yanapokuwa ni mazoea.
 
Kuna tofauti kubwa sana ya Cheo cha Rais na hao wawakailishi unao wahubiri hapa ,katika kutia uzito (msisitizo) wa jambo flani hasa ukizingatia kuwa sisi ni Nchi Masikini sana.
Masikini wewe na familia yako na sioni namna ikitoboa maana unaendekeza dezo na kuombaomba, fikiria kwa akili kubwa how wao wamekuwa matajiri nasisi tishindwe nini.

Mosi lazima ujifunze kujitgemea
Others you name it.
 
Kwa hiyo akiwawakilisha ndo mtapata maendeleao? Acheni Raisi afanye kazi za watanzania! Wanaopishana kila siku kwenye ndege wanapata nini! Hivi nyie watu hamjui raisi akisafili anatumia bilioni ngapi? Msione madaraja ya bil 700 kwenye maji yanajengwa hela zinatoka huko huko mh anapobana matumizi ya safari

Kwani huu Msafara wake wa hapa hapa Nchini na Helkopter juu unajua anatumia kiasi gani Mkuu !?
 
Masikini wewe na familia yako na sioni namna ikitoboa maana unaendekeza dezo na kuombaomba, fikiria kwa akili kubwa how wao wamekuwa matajiri nasisi tishindwe nini.

Mosi lazima ujifunze kujitgemea
Others you name it.

Mkuu haunijui sikujui hivyo hauwezi kunisemea chochote juu ya Maisha yangu ,Great thinker hajadili Watu hapa unatakiwa kujadili Hoja iliyo Mezani.
 
Hapana ,ni Faida kushirikiana na wengine ukizingatia haishi mwenyewe hapa Duniani na hawezi kufanya kila kitu peke yake.
Kuna nchi ngapi nje, akizitembelea zote nilini atawatembelea watanzania walio mchagua na angeeleza nini wananchi wakati huu wa uchaguzi.

Kuna mgombea hafahamu hata majina ya vijiji na shida zao.
 
Back
Top Bottom