Rais atakaefuata baada Rais Samia ni Mwigulu Lameck Nchemba

Rais atakaefuata baada Rais Samia ni Mwigulu Lameck Nchemba

Natabiri hapa waziwazi leo tarehe 16/7/2023 Raisi atakaefuata baada mama samia ni Mwigulu Lameck Nchemba

[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
Nitakuwa mtu wa kwanza kuhamia Burundi. Hakuna mtu hapo. Na kama amekutuma uje umpigie promo, basibmwambie wazi kabisa watu wanasema eti wewe huna hata sifa ya kuwa balozi wa nyumba 10.

Ni vile tu kuna makosa ya kiufundi yalifanyika hapo kabla, na hivyo kujikuta hapo alipo.
 
Nitakuwa mtu wa kwanza kuhamia Burundi. Hakuna mtu hapo. Na kama amekutuma uje umpigie promo, mwambie wazi kabisa wewe huna sifa ya kuwa hata balozi wa nyumba 10.

Amefika kimakosa sana hapo alipo.
Hata enzi za jiwe mlisema hivi hivi
 
Kwa bahati mbaya watu wenye akili kama hawa, ni vigumu sana kwao kupewa nafasi nyeti ya kuongoza raia wenzake. Huyu jamaa yuko vizuri sana kichwani na ana kipawa cha uongozi.

Na ingetokea tukapata Rais kama huyu, ndani ya miaka michache tu tungegeuka na kuwa donor country! Ila siyo mtu kama mwigulu.
 
Mwigulu ana haiba ya urais ila kiukweli haiwezekani yeye kuwa Rais. Kashonyesha sana tamaa ya kukitaka kiti.... na kauli zake za kukera wapiga kura zinamharibia. Pia aina yake ya siasa ni ya hovyo. Kuna wakati alimvalisha mbuzi tshirt ya CHADEMA hadharani. Lile tukio lilikuwa la kipumbavu mno. Hata Magu mwenyewe hakuwa nasiasa za kipuuzi wakati akiwa waziri.
Toka lini nchi hii Rais akachagiwa na wananchi? Akishapitishwa na CCM agombee biashara imeisha
 
Natabiri hapa waziwazi leo tarehe 16/7/2023 Raisi atakaefuata baada mama samia ni Mwigulu Lameck Nchemba

[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
Mungu ndio hutoa uhai, labda kama una mawasiliano naye. Tunajua huo ndio mpango wenu TISS. Lakini sio kwa njia halali ya box la kura.
 
Nani aliamini Magufuli atakua raisi

Niaminini mimi raisi ajae ndio uyo
Magufuli alikuwa rais kwakuwa ccm ilikuwa imezidiwa ushawishi na wapinzani, na yeye pekee ndio alikuwa na afadhali huko CCM. Hii ndio iliyopelekea yeye na CCM yake kuhakikisha wanauhujumu upinzani ili ccm iliyochoka kushindana ipumue. Kama CCM watampitisha Mwigulu sio kwa ajili ya uwezo wake wa uongozi, ila ni kwakuwa ni mkatili kama Magufuli, hivyo ataudhibiti upinzani kwa ulevi wa madaraka.
 
Law of noncontradiction inakataa huwezi kuwa A wakati huo huo ukawa B.

Kama ni muanglikana basi sio mkatoliki ispokuwa ni mkristu.

Hivyo, Law of identity inaelekeza tumtambue kwa ukristu wake na sio vinginevyo.
Mkuu, pana 'Anglican Catholic Church' ujue.
 
  • Thanks
Reactions: 30P
Back
Top Bottom