Jaji Chande amesema hayo wakati Dkt. Samia Suluhu Hassan, akipokea Ripoti ya Tume ya Rais ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani Yaliyotokea Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2025, tarehe 23 Aprili, 2026, Dar es Salaam
"...Madhara ya kiuchumi. Madhara makubwa ya kiuchumi yaliyotokea ni yale yanahusu mali za watu binafsi na mali za serikali kuharibiwa. Tume imebaini kutoka vyanzo mbalimbali kuwa mali iliyoharibiwa ina thamani ya shilingi bilioni 125.
Kati ya mali hizo, mali za sekta binafsi ambazo ni watu binafsi, vituo vya mafuta, CCM na benki, zina thamani ya shilingi bilioni 89 sawa na 71.2%. Na mali za umma ambazo ni mali za serikali na taasisi kama zile shule, TRA, mahakama, polisi, DART, TANROADS, TANESCO, TTCL, zina thamani ya shilingi bilioni 36 sawa na 28.8%.
Lakini sekta binafsi ndio imepata madhara makubwa kuliko sekta ya umma. Ushahidi na waathirika wengi waliopoteza mali binafsi unaonyesha machungu waliopata na wanaendelea kuwa nayo. Mfano mmoja ni mstaafu..."