Rais anisukuma nipigane vita

Rais anisukuma nipigane vita

Mwigulu Nchemba anawanyima sana usingizi CHADEMA. Nawahakikishia kuwa he is our next Minister for Home Affairs. Hapo ndipo mtakapokoma na kusaga meno

samahani hivi mada inahusu chadema au inamhusu nchemba?
 
Hizi ni ngonjera za kipuuzi sana. Kwa nini mnahangaika na mariwaya wakati mwenyekiti wenu anasema kuwa anayo CD inayoonesha waripuaji wa bomu pale Soweto?

...tuliza akili wewe,usiende kama msukule wa jana, huyu mwana ccm mwenzenu alikuwa kwenye vikao vyenu vye kigaidi anao ushahidi wake anataka kuuweka bayana kwa vyombo vinavyo aminika na sio polisi wauaji wasio na dira ya kazi, mbowe nae ana ushahidi tumewaambia mpaka bungeni undeni tume ya kimahakama n=mnagwaya nini...???
 
Hizi ni ngonjera za kipuuzi sana. Kwa nini mnahangaika na mariwaya wakati mwenyekiti wenu anasema kuwa anayo CD inayoonesha waripuaji wa bomu pale Soweto?

siku nkikujua wewe! yani sikupendi kama mavi.
 
Mwanao anaitwa nani, kafa wapi na kwenye mazingira yepi. Maana kama kwenye maandano jina litapatikana na shughuli halisi za baba yake zitajulikana hili hata polisi wakuchukulie serious, let alone raisi wako. Siku hizi kuna tabia za watu kuja na hadithi za uongo sana humu ndani.

Hivi mtu mwenye nia mbaya hatataka kweli kujiweka katika mazingira tata na kauli zake kwa watu asiowajua kiundani, halafu inakupa kweli chama cha siasa chochote kitafute kura za ushindi kwa kupiga watu mabomu.
 
Natumai Sikuku ya X-mas ilienda vizuri na leo hii tupo pamoja katika kusukuma gurudumu hilii zito la maendeleo ya Taifa letu wakati tunahesabu siku chache zipite tuuzike mwaka 2013 na Mungu akipenda tuuanze mwaka 2014.

Wana Jf siku mbili zilizopita Mh. Mwigulu Nchemba alileta post yake ya utetezi humu ndani na mimi niliichachinga kwa kueleza maumivu yaliyo ndani ya moyo wangu. Na baadhi ya wana Jf walinishauri nianzishe Thread japo halikuwa wazo langu mwanzo.

Mnamo mwezi wa sita mwaka 2013 kulikuwa na uchaguzi mdogo wa madiwani katika baadhi ya mikoa ya Tanzania, Arusha ilikuwa mojawapo ya mikoa hiyo huku ikiwa na kata zipatazo 4 zikirudiwa uchaguzi. Nakumbuka vyama vinne vilijitokeza katika kusimamisha wagombea ila chama cha CCM na CHADEMA ndivyo vilikuwa vikishindana. Kipindi hicho nilikuwa mwanachama wa Cmm na nikimfanyia kampeni kwa karibu mgombea udiwani kwa tiketi ya ccm wa Kata ya Elerai Ndg. Emanuel Laizer.

Wakati kampeni zinaendelea na tunakaribia kufikia mwisho tulipata ujumbe kuwa kuna Mjumbe toka makao makuu ya chama atakuja akiambatana na mawaziri ili kuongeza nguvu na atakapofika tutatakiwa tufanye kikao cha siri ambapo katika kikao hicho tutapewa mbinu na mipango mbalimbali ya kukabiliana na Chadema. Na wajumbe watakao ruhusiwa kuuudhuria kikao hicho ni wale viongozi wa mitaa na watu wanao aminika na chama tu.

Tarehe13/06/2013 siku ya alhamisi saa moja jioni tulikutana katika eneo la chuo kimoja cha ufundi (Help to Selph Help Project )kilichopo Sakina kuelekea Olmatejo, kulikuwa na ulinzi mkali ndani na nje ya chuo hicho na magari yapatao sita hivi aina ya Toyota vx na V8 yakiwa yamepaki chuoni hapo, huku taa za chuo hicho zikiwa zimezimwa zoto isipokuwa taa za chumba cha mikutano tu. Tulipewa tangazo kuwa tunatakiwa tuzime simu zetu na tuzikabizi kwa bwana mmoja ambae alikuwa mlangoni (nafikiri waliogopa kurekodiwa au kupigwa picha) kabla ya kuingia ukumbini.

Tulipo kuwa ukumbini aliingia Mwigulu Nchemba na kuanza kutupa moyo na maelekezo ya mbinu mbalimbali za kikampeni, na muda uliposogea majira ya saa 10:00 usiku ndio akaanza kutoa kauli zilizotuacha na maswali mengi kichwani., namnukuu "Kesho tarehe 14 tutafunga kampeni zetu zote na tuna sababu ya kufanya hivyo, kwa sababu tunazo taarifa kuwa Chadema watafunga kampeni zao tarehe 15 siku moja kabla ya uchaguzi ndio maana tumeamua kufanya hivyo. Pili kila mmoja anatakiwa aimize jamiii yake na rafiki zake kwamba siku ya tarehe 15 wasisubutu kwenda kwenye mkutano wa Chadema na yeyote aliopo hapa asisubutu kwenda na atakae enda kitakacho mkuta tusilaumiane" mwisho wa kunukuu.

Kiukweli sina ushaidi wa picha wala rekodi yoyote inayoonyesha mwigulu akiyasema hayo ila nina wajumbe wanne waliokubali kutoa ushaidi pindi kesi itakapoenda mahakamani.

Kwa kuwa Raisi amemfuta kazi aliyekuwa Waziri wa mambo ya Ndani Mh. Nchimbi, ambae alikuwa mtu wa kaaribu sana na Mwigulu Nchemba ndio sababu hasa iliyonifanya kupigana vita hii na wale waliosababisha na namna yoyote kifo cha mwanangu.

NB:
Mh. Raisi nakuomba uunde tume huru ya kijaji ili mimi muhathirika mkuu na wajumbe waliokuwa katika kikao hicho cha Mwigulu Nchemba tuweze kutoa ushaidi utakaoweza kuisaidia tume hiyo kufanya kazi yake kwa uraisi. Nakuomba sasa Mh. Raisi usikie kilio chetu.

MKUU WA KAYA,

Pole sana na namuomba Mungu akupe Moyo wa Subira wewe na familia yako

Nitakuunga mkono kwenye mapambano haya ya kutafuta haki.

Usichoke wala kuogopa hadi ukweli ujulikane

Hatuwezi kujenga demokrasia kwa kudhulumu nafsi za binadamu wenzetu bila sababu.

Jitokeze hadharani bila kujificha na tutakuunga mkono katika kutafuta haki
 
Last edited by a moderator:
Mwigulu na wenzako mnaoshirikiana nao kukihujumu chama kilicho mioyoni mwa waTanzania wengi wapenda mabadiliko(CHADEMA) hakika hamuezi kuzima huu moto wa CHADEMA km ni mbinu ya kuua ndiyo mnayoona ni kutudhoofisha hakika mtatuuwa wengi hatuwezu ogopa vitisho vyenu.
 
Mwigulu ni muuaji kama serikali nzima ya ccm ilivyo ya kiuaji, wanachotakiwa kujua ni kwamba hakuna watawala waliotumia risasi kwa wananchi wao na wakashinda, wananchi wakikukataa huwezi kuwabadilisha kwa risasi, wewe ndio unayehitajika kubadilika kwa yale madhila uwafanyiayo.

Utauwa watanzania wote Mwigulu? mtang'oa kucha na macho watanzania wote? tumewakataa na tunawakataa Ccm mnaosababisha umaskini katika nchi yenye kila rasilimali.
mlaaniwe ccm.
 
Mwigulu Nchemba anawanyima sana usingizi CHADEMA. Nawahakikishia kuwa he is our next Minister for Home Affairs. Hapo ndipo mtakapokoma na kusaga meno

may be kwa familia yako,yaan unashabikia jitu gaidi?? Naona unaishi kwa kutegemea mgongo wa shetani wako dog Nchemba!
 
Heee! we kwani huna familia unakua kama unamegwa..yule awe MHA basi ww na Rais wako mtakua na cha kujibu 2015 kule ICC
 
Mwigulu Nchemba anawanyima sana usingizi CHADEMA. Nawahakikishia kuwa he is our next Minister for Home Affairs. Hapo ndipo mtakapokoma na kusaga meno

Mbona hiyo nafasi ameshaanza kuitumikia siku nyiiingi, ukiwa kiongozi ndani ya ccm unaweza ukawa ndo Jaji mkuu, makamu wa raisi, Katibu mkuu kiongozi, IGP, Mkurugenzi wa usalama wa Taifa e.t.c, Kwa hilo la Nchemba hata sishangai kwani hata asipoapishwa rasmi ataendelea tu na kazi zake sambamba na akina Nchimbi, Lukuvi na Wassira.
 
Mkuu, roho mbaya anayo Mbowe na Slaa ambao wametelekeza familia zao kwa tamaa zao za kimwili

Hivi wewe una ndugu au una nafsi wewe? Mbona mnatetea ujinga? Kama mtu anauwa watu wewe unajifanya uko upande wake unaakili kweli wewe? Tufanye siasa lakini upuuzi tuanchane nao, is only in Tanzania unapoweza kujoke na uhai wa mtu! Acha ukichaa!
 
Ndg mleta mada km ckosei Last wk ulisema leo tar 27 ungefungua KESI mahakamani khs issue hiyo vp umekuja hapa Jukwaani au ckukuelewa vzr! Pia ujue unavyoandika nusunusu hapa hao jamaa ulokuwa nao kwenye huo mpango! Wanakusoma kwahiyo amua 1 km kuFUNGUKA funguka bila kuacha kitu na km hujiamnia potezea!


Uko sahii mkuu na wala hukunielewa vibaya.
Nilipanga leo niingie mahakamani na ushaidi wa kutosha wa kumwingiza Mwigulu hatiani, Tatizo ushaidi wa kufungua kesi ya jinai ndio haujajitosheleza kwani ushaidi wa kimazingira upo ila kisheria unaonekana kama ni ushaidi unaoongozwa na hisia kwa upande mkubwa.
Ila ukweli ni kwamba Mwigulu Nchemba is a One Director of Soweto Bom.

Na kudhibitisha hili haitafika Tarehe 15/01/2014 bila kujitokeza kwenye vyombo vya habari na kuweka haya yote hadharani, labda itokee niwe marehemu kama mwanangu.
 
...tuliza akili wewe,usiende kama msukule wa jana, huyu mwana ccm mwenzenu alikuwa kwenye vikao vyenu vye kigaidi anao ushahidi wake anataka kuuweka bayana kwa vyombo vinavyo aminika na sio polisi wauaji wasio na dira ya kazi, mbowe nae ana ushahidi tumewaambia mpaka bungeni undeni tume ya kimahakama n=mnagwaya nini...???

Mkuu tumpe pole ila ilibidi aitahadhalishe jamii, labda kwa kuwa alikuwa CCM hivyo ile roho ya ubinafsi ilikuwa kwake, lakini amebadirika baada ya kumpoteza mtoto wake!

Nawaasa jamii nzima, tusiwe wabinafsi, angeweza kuokoa maisha ya watu wengi zaidi including mtoto wake!
 
hujang'amua kitu katika hii kauli? "pili kila mmoja anatakiwa aimize jamiii yake na rafiki zake kwamba siku ya tarehe 15 wasisubutu kwenda kwenye mkutano wa Chadema na yeyote aliopo hapa asisubutu kwenda na atakae enda kitakacho mkuta tusilaumiane"

Hivyo vitisho vilivyotumika hapo ni wazi vinakiuka misingi ya kidemokrasia!
...
Na athari zozote zinazoweza kutokea kwa wahusika, ambao wamekengeuka hiyo kauli na wakapata loss isiyoeleweka eleweka chanzo chake.
Kwanini alietoa vitisho asiwajibishwe????
 
Mwigulu Nchemba tunaitaji majibu yako hapa...Damu za watoto zinakulilia.

Mkuu kiukweli siitaji majibu yoyote ya Mwigulu kwa kukuwa vyovyote vile atafanya siasa. Ninachoitaji hapa ni Raisi kuunda tume huru ya kijaji au kumteuwa waziri wa mambo ya ndani ambaye nitakuwa na imani naye ili niweze kujitokeza hadharani.
 
muendelezo wa hadithi za kuunga unga kama ulivyosema huna ushahidi, kwahiyo hatuwezi jadili jambo ambalo halina ushahidi
 
MKUU WA KAYA,

Pole sana na namuomba Mungu akupe Moyo wa Subira wewe na familia yako

Nitakuunga mkono kwenye mapambano haya ya kutafuta haki.

Usichoke wala kuogopa hadi ukweli ujulikane

Hatuwezi kujenga demokrasia kwa kudhulumu nafsi za binadamu wenzetu bila sababu.

Jitokeze hadharani bila kujificha na tutakuunga mkono katika kutafuta haki


Nashukuru mkuu,
I promis to be publicized before 15/01/2014
Na kwa hili Mwigulu hawezi kuchomoka wala kujitetea kwani ni kweli aliongea na kutoa viashiria vyote juu ya yale yaliyotokea soweto.

NB:
Ushaidi nilionao na ule Chadema wanaosema wanao ni tofauti kabisa na nitasimama juu ya kile nilichokiona na kukisikia na sio kuhisi au kuambiwa. Sitoogopa.
 
muendelezo wa hadithi za kuunga unga kama ulivyosema huna ushahidi, kwahiyo hatuwezi jadili jambo ambalo halina ushahidi
Kwa nini unajibu kwa kujifichaficha njoo kwa jina lako halisi.
 
Back
Top Bottom