Rais anisukuma nipigane vita

Eddo Sambai

JF-Expert Member
Aug 1, 2013
1,815
0
Natumai Sikuku ya X-mas ilienda vizuri na leo hii tupo pamoja katika kusukuma gurudumu hilii zito la maendeleo ya Taifa letu wakati tunahesabu siku chache zipite tuuzike mwaka 2013 na Mungu akipenda tuuanze mwaka 2014.

Wana Jf siku mbili zilizopita Mh. Mwigulu Nchemba alileta post yake ya utetezi humu ndani na mimi niliichachinga kwa kueleza maumivu yaliyo ndani ya moyo wangu. Na baadhi ya wana Jf walinishauri nianzishe Thread japo halikuwa wazo langu mwanzo.

Mnamo mwezi wa sita mwaka 2013 kulikuwa na uchaguzi mdogo wa madiwani katika baadhi ya mikoa ya Tanzania, Arusha ilikuwa mojawapo ya mikoa hiyo huku ikiwa na kata zipatazo 4 zikirudiwa uchaguzi. Nakumbuka vyama vinne vilijitokeza katika kusimamisha wagombea ila chama cha CCM na CHADEMA ndivyo vilikuwa vikishindana. Kipindi hicho nilikuwa mwanachama wa Cmm na nikimfanyia kampeni kwa karibu mgombea udiwani kwa tiketi ya ccm wa Kata ya Elerai Ndg. Emanuel Laizer.

Wakati kampeni zinaendelea na tunakaribia kufikia mwisho tulipata ujumbe kuwa kuna Mjumbe toka makao makuu ya chama atakuja akiambatana na mawaziri ili kuongeza nguvu na atakapofika tutatakiwa tufanye kikao cha siri ambapo katika kikao hicho tutapewa mbinu na mipango mbalimbali ya kukabiliana na Chadema. Na wajumbe watakao ruhusiwa kuuudhuria kikao hicho ni wale viongozi wa mitaa na watu wanao aminika na chama tu.

Tarehe13/06/2013 siku ya alhamisi saa moja jioni tulikutana katika eneo la chuo kimoja cha ufundi (Help to Selph Help Project )kilichopo Sakina kuelekea Olmatejo, kulikuwa na ulinzi mkali ndani na nje ya chuo hicho na magari yapatao sita hivi aina ya Toyota vx na V8 yakiwa yamepaki chuoni hapo, huku taa za chuo hicho zikiwa zimezimwa zoto isipokuwa taa za chumba cha mikutano tu. Tulipewa tangazo kuwa tunatakiwa tuzime simu zetu na tuzikabizi kwa bwana mmoja ambae alikuwa mlangoni (nafikiri waliogopa kurekodiwa au kupigwa picha) kabla ya kuingia ukumbini.

Tulipo kuwa ukumbini aliingia Mwigulu Nchemba na kuanza kutupa moyo na maelekezo ya mbinu mbalimbali za kikampeni, na muda uliposogea majira ya saa 10:00 usiku ndio akaanza kutoa kauli zilizotuacha na maswali mengi kichwani., namnukuu "Kesho tarehe 14 tutafunga kampeni zetu zote na tuna sababu ya kufanya hivyo, kwa sababu tunazo taarifa kuwa Chadema watafunga kampeni zao tarehe 15 siku moja kabla ya uchaguzi ndio maana tumeamua kufanya hivyo. Pili kila mmoja anatakiwa aimize jamiii yake na rafiki zake kwamba siku ya tarehe 15 wasisubutu kwenda kwenye mkutano wa Chadema na yeyote aliopo hapa asisubutu kwenda na atakae enda kitakacho mkuta tusilaumiane" mwisho wa kunukuu.

Kiukweli sina ushaidi wa picha wala rekodi yoyote inayoonyesha mwigulu akiyasema hayo ila nina wajumbe wanne waliokubali kutoa ushaidi pindi kesi itakapoenda mahakamani.

Kwa kuwa Raisi amemfuta kazi aliyekuwa Waziri wa mambo ya Ndani Mh. Nchimbi, ambae alikuwa mtu wa kaaribu sana na Mwigulu Nchemba ndio sababu hasa iliyonifanya kupigana vita hii na wale waliosababisha na namna yoyote kifo cha mwanangu.

NB:
Mh. Raisi nakuomba uunde tume huru ya kijaji ili mimi muhathirika mkuu na wajumbe waliokuwa katika kikao hicho cha Mwigulu Nchemba tuweze kutoa ushaidi utakaoweza kuisaidia tume hiyo kufanya kazi yake kwa uraisi. Nakuomba sasa Mh. Raisi usikie kilio chetu.
 
Mutakyamirwa

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
4,943
1,500
Mkuu,

Simamia ukweli haki itendeke kwa Nchemba. Tanzania haiwezi kuendeshwa kinyama namna hiyo. Ninachokijua, hata kama haki haitapatikana mahakama, hukumu itokayo juu itatosha kwa ilo Li-Savimbi.
 
Eddo Sambai

JF-Expert Member
Aug 1, 2013
1,815
0
Mkuu,

Simamia ukweli haki itendeke kwa Nchemba. Tanzania haiwezi kuendeshwa kinyama namna hiyo. Ninachokijua, hata kama haki haitapatikana mahakama, hukumu itokayo juu itatosha kwa ilo Li-Savimbi.

Asante mkuu kwa maneno yako yenye ujasiri, pia nataka nijadiliane na mwanasheria wangu niangalie kama nitaweza kuviandikia vyombo vya habari kama ITV, STAR TV, CHANEL 10 nk, ili nifanye press kala ya kulifikisha hili swala mahakamani.
 
Baba V

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
19,487
2,000
Siasa za bongo ni upu.uzi mtupu na kuuana kijinga.jinga!
Itakuaje nchi ya kidemokrasia watu wazuiliwe kuhudhuria mikutano ya wengine?

ALIKUWA ANAWATAHADHARISHA NA BOMU LA cHINA, SI UNAONA KILICHOFUATA BAADA YA PALE... YAANI NCHI HII KUNA WATU WANAJIONA NI MIUNGU AISEE..
 
Baba V

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
19,487
2,000
Asante mkuu kwa maneno yako yenye ujasiri, pia nataka nijadiliane na mwanasheria wangu niangalie kama nitaweza kuviandikia vyombo vya habari kama ITV, STAR TV, CHANEL 10 nk, ili nifanye press kala ya kulifikisha hili swala mahakamani.

Wakati huo unayafanya haya agana na nyonga kabisa maana hawachelewi kukupoteza wale, kama wanaona poa kuua watu makumi na mamia ya watu kwa mabomu hawashindwi kuku MVUNGI.
 
Buldoza

JF-Expert Member
May 2, 2013
2,306
2,000
Kwa yale yaliyotokea Arusha, Mwigulu Nchemba na Emmanuel Nchimbi, lazima damu za Wasio na hatia zitaendelea kuwalilia hadi vizazi vyenu. Auwae kwa Upanga.........
 
Eddo Sambai

JF-Expert Member
Aug 1, 2013
1,815
0
Wakati huo unayafanya haya agana na nyonga kabisa maana hawachelewi kukupoteza wale, kama wanaona poa kuua watu makumi na mamia ya watu kwa mabomu hawashindwi kuku MVUNGI.

Unayoyasema ni kweli maana ata juzi walikuja watu nyumbani kwangu usiku na kugongo mlango wakidai wao ni askari na nilipo wauliza kama ninyi ni Askari kwanini mruke ukuta na kuja kunigongea mlangoni wakanijibu kuwa hayo hayaniusu kinachotakiwa ni mimi nifungue mlango. Walipona nawasiliana na polisi wakatimua zao.
 
Buldoza

JF-Expert Member
May 2, 2013
2,306
2,000
Hivi inakuwaje Mwigulu anakuwa na roho mbaya hivi! Sababu tu ana sapoti ya Mkuu basi yeye anajiona anaweza kumuua mtu yeyote tu na akaendelea kutembea kifua mbele! Sasa Nchimbi aliyekuwa anashirikiana nae kafukuzwa kazi, tuone atatokea wapi? Huwezi kuwa mnyama kiasi hiko, kisa ni siasa tu. Mungu atakulaani wewe na vizazi vyako vyote. Damu iliyomwagika na machozi ya ndugu na jamaa wa marehemu yatakulilia milele.
 
Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,891
2,000
Hizi ni ngonjera za kipuuzi sana. Kwa nini mnahangaika na mariwaya wakati mwenyekiti wenu anasema kuwa anayo CD inayoonesha waripuaji wa bomu pale Soweto?
 
Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,891
2,000
Hivi inakuwaje Mwigulu anakuwa na roho mbaya hivi! Sababu tu ana sapoti ya Mkuu basi yeye anajiona anaweza kumuua mtu yeyote tu na akaendelea kutembea kifua mbele! Sasa Nchimbi aliyekuwa anashirikiana nae kafukuzwa kazi, tuone atatokea wapi? Huwezi kuwa mnyama kiasi hiko, kisa ni siasa tu. Mungu atakulaani wewe na vizazi vyako vyote. Damu iliyomwagika na machozi ya ndugu na jamaa wa marehemu yatakulilia milele.
Mkuu, roho mbaya anayo Mbowe na Slaa ambao wametelekeza familia zao kwa tamaa zao za kimwili
 
Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,891
2,000
Unayoyasema ni kweli maana ata juzi walikuja watu nyumbani kwangu usiku na kugongo mlango wakidai wao ni askari na nilipo wauliza kama ninyi ni Askari kwanini mruke ukuta na kuja kunigongea mlangoni wakanijibu kuwa hayo hayaniusu kinachotakiwa ni mimi nifungue mlango. Walipona nawasiliana na polisi wakatimua zao.
Yaani uzi mnaanzisha wenyewe halafu mnajijibu wenyewe. Bora watu wamesusa kuchangia uz huu
 
Rock City

JF-Expert Member
Feb 11, 2012
1,266
0
Mkuu chukua tahadhari kuu.

Narudia, chukua tahadhari na family yako. Haya mambo si lelemama hata kidogo.
 
Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,891
2,000
atakuja huyo mchemba aanze ngonjera zake,na kuanza kukanusha
Mwigulu Nchemba anawanyima sana usingizi CHADEMA. Nawahakikishia kuwa he is our next Minister for Home Affairs. Hapo ndipo mtakapokoma na kusaga meno
 
Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
43,803
2,000
Tatizo uzi kama huu hauwezi kudumu hapa.

Mods msifunge huu uzi kama mtuhimiwa amekerwa aende mahakamani.

Mwigulu mwenyewe ni mtu wa kutoa tuhuma hadharani hivyo mwacheni nae aumbuke.

Ni mtazamo wangu unaotokana na kuwepo hapa jukwaani kwa muda sasa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom