Rais anisukuma nipigane vita

Rais anisukuma nipigane vita

Kupigana na nchemba ni sawa na kupigana na kichaa ambaye hata mirembe bado hajaenda kupimwa. Wapo wengi wa aina ya nchemba hasa kwenye ccm.
 

Mkuu Kenwood, kifo cha mwanangu ni sababu hasa iliyonifanya nipigane hii vita, na kiukweli kama mwanangu kifo kisingemfika nisingekuwa na sababu yoyote ya kupambana na Mwigulu kwakuwa angeendelea kuwa kiongozi wangu ndani ya chama.
Ila napenda uelewe wajumbe wote tuliokuwa katika ukumbi wa Chuo tulikuwa tumeenda kusikiliza na sio kupanga jambo lolote maana taarifa za awali tuliambiwa kuna mbinu tunakuja kupewa na sio kupanga.

Hauja eleza mwanao alienda vipi wakati mlikwisha onywa au ulidharau. mi naona hii ni hadithi 2 hamna la maana na kama kweli unaogopa nini? nenda kafungue kesi au katoe ushahidi polisi vinginevyo kaa kimya
 
Hauja eleza mwanao alienda vipi wakati mlikwisha onywa au ulidharau. mi naona hii ni hadithi 2 hamna la maana na kama kweli unaogopa nini? nenda kafungue kesi au katoe ushahidi polisi vinginevyo kaa kimya

Sawasawa labisa, huyu anatupotezea muda tu hapa.
 
Hizi ni ngonjera za kipuuzi sana. Kwa nini mnahangaika na mariwaya wakati mwenyekiti wenu anasema kuwa anayo CD inayoonesha waripuaji wa bomu pale Soweto?

CD anayo, kuunda tume ya kimahakama mmegoma, subirini mahakama yenu 2015, hiyo CD itawahukumu vizuri sana kwetu sisi wenye nchi! Tatizo lenu mnasahau cheo nidhamana tu, kesho si nyinyi, vipi Nchimbi sasa hivi? kile cheo chake kilicho mlewesha hadi akaona kifo cha binadamu wenzie kama kafa kuku tu? siku inakuja wala haiko mbali hizo mnazo ziita ngojera zitakapo kuwa kweli!
 
Natumai Sikuku ya X-mas ilienda vizuri na leo hii tupo pamoja katika kusukuma gurudumu hilii zito la maendeleo ya Taifa letu wakati tunahesabu siku chache zipite tuuzike mwaka 2013 na Mungu akipenda tuuanze mwaka 2014.

Wana Jf siku mbili zilizopita Mh. Mwigulu Nchemba alileta post yake ya utetezi humu ndani na mimi niliichachinga kwa kueleza maumivu yaliyo ndani ya moyo wangu. Na baadhi ya wana Jf walinishauri nianzishe Thread japo halikuwa wazo langu mwanzo.

Mnamo mwezi wa sita mwaka 2013 kulikuwa na uchaguzi mdogo wa madiwani katika baadhi ya mikoa ya Tanzania, Arusha ilikuwa mojawapo ya mikoa hiyo huku ikiwa na kata zipatazo 4 zikirudiwa uchaguzi. Nakumbuka vyama vinne vilijitokeza katika kusimamisha wagombea ila chama cha CCM na CHADEMA ndivyo vilikuwa vikishindana. Kipindi hicho nilikuwa mwanachama wa Cmm na nikimfanyia kampeni kwa karibu mgombea udiwani kwa tiketi ya ccm wa Kata ya Elerai Ndg. Emanuel Laizer.

Wakati kampeni zinaendelea na tunakaribia kufikia mwisho tulipata ujumbe kuwa kuna Mjumbe toka makao makuu ya chama atakuja akiambatana na mawaziri ili kuongeza nguvu na atakapofika tutatakiwa tufanye kikao cha siri ambapo katika kikao hicho tutapewa mbinu na mipango mbalimbali ya kukabiliana na Chadema. Na wajumbe watakao ruhusiwa kuuudhuria kikao hicho ni wale viongozi wa mitaa na watu wanao aminika na chama tu.

Tarehe13/06/2013 siku ya alhamisi saa moja jioni tulikutana katika eneo la chuo kimoja cha ufundi (Help to Selph Help Project )kilichopo Sakina kuelekea Olmatejo, kulikuwa na ulinzi mkali ndani na nje ya chuo hicho na magari yapatao sita hivi aina ya Toyota vx na V8 yakiwa yamepaki chuoni hapo, huku taa za chuo hicho zikiwa zimezimwa zoto isipokuwa taa za chumba cha mikutano tu. Tulipewa tangazo kuwa tunatakiwa tuzime simu zetu na tuzikabizi kwa bwana mmoja ambae alikuwa mlangoni (nafikiri waliogopa kurekodiwa au kupigwa picha) kabla ya kuingia ukumbini.

Tulipo kuwa ukumbini aliingia Mwigulu Nchemba na kuanza kutupa moyo na maelekezo ya mbinu mbalimbali za kikampeni, na muda uliposogea majira ya saa 10:00 usiku ndio akaanza kutoa kauli zilizotuacha na maswali mengi kichwani., namnukuu "Kesho tarehe 14 tutafunga kampeni zetu zote na tuna sababu ya kufanya hivyo, kwa sababu tunazo taarifa kuwa Chadema watafunga kampeni zao tarehe 15 siku moja kabla ya uchaguzi ndio maana tumeamua kufanya hivyo. Pili kila mmoja anatakiwa aimize jamiii yake na rafiki zake kwamba siku ya tarehe 15 wasisubutu kwenda kwenye mkutano wa Chadema na yeyote aliopo hapa asisubutu kwenda na atakae enda kitakacho mkuta tusilaumiane" mwisho wa kunukuu.

Kiukweli sina ushaidi wa picha wala rekodi yoyote inayoonyesha mwigulu akiyasema hayo ila nina wajumbe wanne waliokubali kutoa ushaidi pindi kesi itakapoenda mahakamani.

Kwa kuwa Raisi amemfuta kazi aliyekuwa Waziri wa mambo ya Ndani Mh. Nchimbi, ambae alikuwa mtu wa kaaribu sana na Mwigulu Nchemba ndio sababu hasa iliyonifanya kupigana vita hii na wale waliosababisha na namna yoyote kifo cha mwanangu.

NB:
Mh. Raisi nakuomba uunde tume huru ya kijaji ili mimi muhathirika mkuu na wajumbe waliokuwa katika kikao hicho cha Mwigulu Nchemba tuweze kutoa ushaidi utakaoweza kuisaidia tume hiyo kufanya kazi yake kwa uraisi. Nakuomba sasa Mh. Raisi usikie kilio chetu.

Hivi huyu Nchemba kwanini anatesa watanzania?,Bw Nchemba unasemwa sana mkuu jirekebishe nenda jimboni kwako.
 
Back
Top Bottom