Rais amchagua Abdala Mtonga kuwa Internal Auditor General

Rais amchagua Abdala Mtonga kuwa Internal Auditor General

I am confused...Unasema JK kafanya uamuzi sahihi kumchagua Abdallah maana jamaa ni mtu safi na hataki upuuzi lakini at the same time unasema ni mwoga kufanya maamuzi!!!!!! Leadership is about making decision na mtu mwoga kufanya maamuzi hafai kuwa kiongozi. Kama ni kweli Abdallah ni mwoga kufanya maamuzi basi ofisi hii haimfai hata kidogo hata kama angekuwa mwadilifu kama malaika maana kuna wakati itabidi afanye maamuzi mazito na hatayafanya maana ni mwoga. Watu waoga wa kufanya maamuzi huwa wanatakiwa wawe chini ya mtu fulani ili wao wawe wanapokea orders tu na kuzifanyia kazi ili likitokea tatizo aseme boss ndo aliniambia nifanye

Ngoja nitafuatilia maana mimi nilipata tetesi kwamba kamteua Aziz Kifile ambaye ni msaidizi wa Mhasibu mkuu wa serikali pale wizara ya fedha na inasemekana ni mwislamu safi.
 
Yanisikitisha kuwa Kikwete amekumbuka shuka kumekucha. Kuwepo kwa kitengo hiki ilikuwa na sharti la wfadhiri mwaka jana yeye akakataa kuiweka kwa kisingizio kuwa mswada ulikuwa na mapungufu matokeo yake donors wakakataa kuchangia kwenye busket fund. Ndo maana mwaka huu miradi mingi haijatekelezeka na bajeti ina nakshi kubwa ambayo haizibiki.
 
Kuna watu wanapaswa waaishie kwenye ngazi flan za uongozi, hii inatokana na uwezo wao mdogo wa kubeba majukum, kama mtu ni mwoga basi ubora wake unaoonekana kwa sasa ni kwa sababu anariport kwa mtu. Aishie hapo tu. Atafutwe mtu mwingine mwenye kifua cha kufanya maamuzi mazito.
 
Kama Jakaya anataka kufanya replacement kwenye hiyo nafasi anatakiwa kutambua kwamba
so far hicho ndio kitengo pekee cha serikali ambacho wananchi wanaimani nacho, akiamua kukivuruga,
atafupisha siku zake magogoni

Mkuu replacement gani tena? Kitengo hicho hakikuwepo ndio kwanza kinaanzishwa!! Hakikuwepo wananchi wanaimani nacho? Wawe na imani na kitu ambacho hakikuwepo, makubwa!! Hii si ofisi ya Controller and Auditor General (CAG) ni ofisi mpya ya Internal Auditor General (IAG)!! WanaJF tuwe tunakuwa pamoja ili kuchangia kitu tunachokijua!!
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete amemeteua Bw. Mohammed A. Mtonga (52) kuwa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali (Internal Auditor General).

Bw. Mtonga ni msomi mwenye Shahada ya Uzamili katika masuala ya Fedha (MSc in Corporate Finance) toka Chuo Kikuu cha Salford nchini uingereza.

Aidha Bw. Mtonga anayo Shahada ya Uhasibu ya CPA (T) inayotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) na Stashada ya Juu ya Uhasibu (Advanced Diploma in Professional Accountancy) toka Chuo cha Jamii Nyegezi ambacho kwa sasa ni Chuo Kikuu cha Mt. Augustine cha Mwanza.

Kabla ya uteuzi huu, Bw. Mtonga amekuwa na utumishi wa miaka 32 katika Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Heasabu ambapo amewahi kushika nyadhifa mbalimbali.

Nyadhifa alizowahi kushika Bw. Mtonga ni pamoja na Afisa Masuuli na Mkaguzi wa Hesabu wa Kanda. Pia amewahi kuwa Mkaguzi wa Hesabu Mkazi katika mkoa wa Lindi, Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Makao Makuu ya Jeshi (Ngome).

Uteuzi huu umeanza toka tarehe 06 Aprili, 2011.

source: Wavuti - Habari
 
Huyu ni dini gani?
 
Ni kweli Masjid lakini jamaa shule iko na uzoefu.Mpeni haki yake
 
Ni kweli Masjid lakini jamaa shule iko na uzoefu.Mpeni haki yake
ukisema nikweli masjid nisawa nakusema 'jamaa freshi sana sema tuu mmasai' huo ni mfano mzuri sana wa mawazo yakibaguzi. Inamaana watu wakiwa waislamu na wana qualifications zote zinazohitajika inakuwa poa JAPOKUWA ni waislamu!! Inasikitisha sana kuona kuwa Tanzania kweli kuna watu wanamawazo ya namna hii. Sijuii hii sumu inatokana na nini? Sinto toa ata onyo kwasababu madhara yake wote twayajua.
 
Hii ndio Tanzania yetu bwana, zamani tuliambiwa kama waislamu hawakusoma kazi kunywa kahawa na kashata tu! sasa amechaguliwa jamaa mwenye CPA, Masters na uzoefu wa kazi zaidi ya miaka 32...utasikia hoja nyingine kama JK ni mdini. Hii ndio Tanzania ambayo CDM wanataka waijejenge.

Miongoni mwa wachangiaji wakubwa na wanaombatiza JK kuwa ni mdini ni hawa makada wa CDM walioko hapa JF!!!

Kikwebo.
 
Mimi pia nahitaji hiyo sheria kwa kweli maana kama sielewi hivi, kwani Controller and Auditor General (CAG) pia anafanya audit kwa kuwa internal audit ni sehemu ya audit. Nahisi kama hatujuwi tunachofanya hapa sana sana tunazidi kumwongezea mzigo masikini mlipa kodi (nchi hii inaendeshwa kwa PAYE) pasipokuongeza efficiency yeyote kama tulivyofanya kwenye EWURA, SUMATRA na upuuzi mwingine unaofanana na huo.

Ni nani amesema kwamba tatizo letu ni kutokufanyika kwa audit? Hili si kweli kwani kila mwaka CAG anareport upotevu wa mabilioni na hakuna kinachofanyika, reports zake tunaishia kufungia vitumbua Kwamtogole.Tungekuwa serious kufanyia kazi reports na recommendations za CAG wala tusingehitaji ofisi mpya ya internal audit, huu ni upotevu wa pesa usio na sababu.

Kaka kazi za CAG na IAG hazifanani, zipo zinazofanana na nyingi hazifanani.Kumbukeni pia kwamba Tanzania iliridhia kufuata mtindo wa IFRS

(international Financial reporting standards), kwa sasa hesabu zetu Tanzania zinatayarishwa kwa kufuata muundo huu.Moja ya mahitaji ya miundo ya kimataifa ni pamoja na kuimarisha ukaguzi wa ndani(IA).
Kuteuliwa kwa IAG ni compliance with IFRS kwanza hii wamechelewa kwani TZ wholly adopted the reporting standards way back in july 2004
 
Kuna watu wanapaswa waaishie kwenye ngazi flan za uongozi, hii inatokana na uwezo wao mdogo wa kubeba majukum, kama mtu ni mwoga basi ubora wake unaoonekana kwa sasa ni kwa sababu anariport kwa mtu. Aishie hapo tu. Atafutwe mtu mwingine mwenye kifua cha kufanya maamuzi mazito.

Sasa kama kateua mwoga mwenzie itakuwaje?!!!!
 
Tehe wana undugu na mama, nasikia anatokea lindi
 
Mwislam Safi, ulamaa aneyejua kazi yake na misingi ya uislam, hongera JK kwa uteuzi huu.

Hahahaha...umeniacha hoi Gamba jipya..kwa mujibu wa mtoa mada ameweka bayana wasifu mojawapo wa mtu aliyeteuliwa kwamba ni muoga wa kufanya maamuzi, sasa hapo unampa hongera kwa lipi mkweree?...ovyooooo...!!
 
Back
Top Bottom