Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,262
Kwenye mahojiano Jumatatu, Bw Odinga alishangaa ni kwanini Jubilee ina wasiwasi kuhusu suala hilo, ilhali matangazo halisi yatatolewa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC).
"Sioni ni kwa nini wenzetu (Jubilee) wana wasiwasi. Lengo letu ni kuhakikisha kuwa tunalinda na kuthibitisha hesabu za kura zinazotolewa na IEBC. Hatuna njama zozote", akasema Bw Odinga akihojiwa na Radio Jambo.
Wakati huo huo, Bw Odinga aliilaumu Serikali kwa kuingilia urafiki wake na Rais John Magufuli wa Tanzania, akisema yeye ni rafiki wa Marais wengine barani Afrika
Marafiki wengine
"Rais Yoweri Museveni wa Uganda ni rafiki yangu wa muda mrefu, hata kuliko Bw Magufuli. Marais wengine kama Alassane Ouatara (Ivory Coast) na Jacob Zuma (Afrika Kusini) kati ya wengine ni marafiki wangu pia. Mbona wanawashwa na urafiki wangu na Bw Magufuli?" akashangaa
Urafiki wa wawili hao ulionekana wazi Bw Magufuli alipohudhuria mazishi ya mwanawe Raila, Fidel Castro, mnamo 2015
Bw Odinga ndiye aliyekuwa kiongozi wa kwanza wa kimataifa kuzuru Tanzania kumpongeza Bw Magufuli baada ya kushinda urais Novemba 2015.
Kwenye mahojiano hayo, Bw Odinga pia alilalamika kuhusu uamuzi wa Mahakama Kuu kuiruhusu kampuni ya Al-Ghurair kuchapisha karatasi za urais akisema mahakama ilifikia uamuzi huo baada ya kutishwa na Serikali
Alidai kuwa kesi yao ilikuwa na ushahidi wa kutosha kuwa kampuni hiyo ina uhusiano na watu wenye ushawishi Serikalini.
"Hata hivyo tuliamua kuheshimu uamuzi wake ili tusivuruge maandalizi ya uchaguzi mkuu wa Agosti 8", alisema Odinga.
Chanzo: TaifaLeo