Odinga agoma kustaafu, asema kugombea tena 2027

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,566
KIONGOZI wa Chama cha Upinzani nchini Kenya, Raila Odinga amefichua kuwa bado hajajiandaa kujiondoa katika ulingo wa kisiasa na kwamba hatostaafu.

Raila mwenye umri wa miaka 78 alidokeza kujaribu bahati yake katika kiti cha urais kwa mara ya sita katika Uchaguzi Mkuu wa 2027.

"Siko tayari kuacha, na kwa hivyo mnapaswa kuwa tayari kuniunga mkono. Nilimsikia Ruto akisema kwamba ninaacha, na hivyo Kalonzo atachukua usukani, Kalonzo ni kitafunwa tu kwake," amesema Raila.

Akizungumza katika kisiwa cha Mfangano huko Homa Bay, Raila aliomba kuungwa mkono ili kuhakikisha muungano wa Azimio unaokabiliwa na kuzinduliwa upya, unasalia imara na kupata kiti cha juu.
 
Tatizo wajaluo na siasa zao za ukabila

Miaka yote hii hawajaanda mjaluo mwingine kugombea? Damu mbichi kijana badala ya Odinga

Odinga anakomaa sababu wajaluo hawajaandaa mbadala wake sasa afanyaje?

Hata kama ni ukabila mzee wa watu walitakiwa wawe wamemwandalia Mrithi

Ataendelea Sababu wajaluo hawajaanda wa kushika nafasi yake
 
Haki yake Kikatiba! Mrithi alikuwa mtoto wake Fidel! Unfortunately is no more!
 
Back
Top Bottom