Raila Odinga akiri kuugua homa kali

Kenyan

JF-Expert Member
Jun 7, 2012
414
313
Hatimaye Kiongozi wa Upinzani Raila Odinga amevunja ukimya baada ya kutojitokeza hadharani kushiriki maandamano.

Raila ameeleza kuwa alilazwa baada ya kuugua homa kali.

“Niko na homa mbaya sana ambayo ilinipiga na ikanilaza chini. Nimepata matibabu kutoka kwa daktari na sasa ninazidi kupata afueni na nitakuwa sawa." Odinga aliiambia NTV

Hatahivyo maswali yameibuka ni kwa nini vinara wengine wa Upinzani wakiwemo Martha Karua na Kalonzo Musyoka vilevile hawajajitokeza hadharani, suala ambako Odinga amefafanua akisema maandamano sio ya vinara wa Muungano wa Azimio tu bali ni ya raia wote wa Kenya kwa ujumla.

“Team yote ya Azimio iko sawa na wanaongoza maandamano kutoka maeneo tofauti tofauti. Si lazima waonekane wote kwa barabara.” alisema Odinga.

Aidha Raila ameepuzilia mbali tetesi kuwa amewasiliana na Rais Ruto kwa njia ya simu akisema kuwa Upinzani hauna Nia ya kushiriki mazungumzo na Serikali.

"Handshake ni porojo yao… ati watu wa Azimio wanatafuta handshake na nusu mkate. Hatutaki mkate yao ambayo imeoza."

Ijumaa ya Leo ni siku ya tatu ya maandamano japokuwa makali yake yameonekana kupungua tangu Jana kutokana na kutoonekana kwa Raila Odinga na vinara wenzake wa Upinzani.
 
Hatahivyo maswali yameibuka ni kwa nini vinara wengine wa Upinzani wakiwemo Martha Karua na Kalonzo Musyoka vilevile hawajajitokeza hadharani, suala ambako Odinga amefafanua akisema maandamano sio ya vinara wa Muungano wa Azimio tu bali ni ya raia wote wa Kenya kwa ujumla.
Wanasiasa bhana.....
 
“Team yote ya Azimio iko sawa na wanaongoza maandamano kutoka maeneo tofauti tofauti. Si lazima waonekane wote kwa barabara.” alisema Odinga.
Kwahio hata wakiandama nyumbani kwao sebuleni, jikoni na uwani ni sawa tu !!!. Au wote walipigwa na Homa kali ?
 
Martha Karua, Jeremiah Kioni, Kalonzo Musyoka, Eugine wamalwa, Opiya wandayi etc. waliongoza maandamano sehemu gani? zaidi ya Edwin Sifuna kujipachika dakika kadhaa kwenye kundi la waandamanaji hakuna kiongozi yeyote wa Azimio aliejitokeza katika maandamano. Raila apumzike
 
Wakenya wanajua sana siasa, za kujiamini sio wa bongo wakutishwa tu na ccm dola, na kujifungia ndani, na kubaki kwenye keybord zao, na ndo maana kenya wako juu sana.
 
Back
Top Bottom