Raila Odinga anaamini Rais Magufuli hashauriwi vizuri

JipuKubwa

JF-Expert Member
Jun 1, 2013
2,311
2,324

Wanajukwaa, yule rafiki mkubwa wa Magu katika ukanda huu wa Afrika mashariki bwana Raila Odinga amekiri kwamba huenda rais Magufuli hapewi ushauri mzuri na amewaasa viongozi wengine wampe ushauri kwani ni msikivu.

Hayo yamejiri wakati akihojiwa na kituo cha habari, japo haikuwekwa wazi ni katika jambo gani ndugu Raila ameona rais hashauriwi vizuri.

WanaJF vipi maoni yenu kuhusu ushauri wa Raila Odinga?

=====

Virusi vya corona: Kiongozi wa upinzani wa Kenya Raila Odinga amesema Rais Magufuli ''anashauriwa vibaya''

9 Mei 2020
Akijibu kauli za Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga, Mbunge wa Tanzania kutoka chama tawala cha CCM Job Lusinde Kibabaje amesema mfumo ambao Magufuli anautumia katika kukabiliana na Covid -19 ni mfumo umewasaidia sana Watanzania tofauti na Afrika Kusini, Uganda Kenya na Rwanda. ‘’Pengine wanashindwa tu kumuelewa’’, alisema katika mahojiano na BBC.

‘’Rais mfumo alioutumia kwa kukataa kuwaweka watu Lockdown, sisi Watanzania tunafahamiana, kuna watu wengi wanakula chakula cha leo wakitoka...leo ukiwafungia ndani wanaweza kupata matatizo makubwa’’ amesema .
‘’Mi natakaka tu kumuambia mwanasiasa mkongwe Raila kuwa Magufuli anawafahamu Watanzania zaidi na rais ana uchungu zaidi na Watanzania kuhusu uchungu wowote’’alisema Mbunge Kibabaja.

Raila amesema viongozi wa kanda wamekua wakitaka kushauriana na rais John Pombe Magufuli, bila mafanikio.
 
Shida ni kwamba hata akishauriwa hakubali yeye kila Ushauri anasema unatoka kwa mabeberu
 
Wanajukwaa,yule rafiki mkubwa wa Magu katika ukanda huu wa Afrika mashariki bwana Raila Odinga amekiri kwamba huenda rais Magufuli hapewi ushauri mzuri na amewaasa viongozi wengine wampe ushauri kwani ni msikivu. Hayo yamejiri wakati akihojiwa na kituo cha habari, japo haikuwekwa wazi ni katika jambo gani ndugu Raila ameona rais hashauriwi vizuri.

WanaJF vipi maoni yenu kuhusu ushauri wa Raila Odinga?
Kenya wapambane na hali zao!
 
Sarah kimani amekuwa Raila? Au anatafuta bwana Tanzania maana kenya nzala tupu
 
Back
Top Bottom