Nadhani kuna kitu watu wengi hamkifahamu kuhusiana na huyu marehemu, mwamba kabisa, jemedari wa demokrasia, hasa kwa nyakati hizi za mwisho wa uhai wake,
Raila wa mwaka 2007, 2013, 2018 na 2022 si huyu aliyekua amebaki sasa, kadri siku zilivyokua zikienda alikua akiendelea kupoteza ushawishi, na sababu kuu ilikua vijana wa sasa yaani Gen Z walikua wameshamshtukia na kupoteza matumaini nae kwakua mpaka wanaandamana mwaka jana 2024 alikua akiwasupport na kama hamfahamu basi niwajuze kua Raila ndiye mtu aliyesimamisha yale maandamano ya kumtoa Ruto madarakani baada ya Ruto kumpigia magoti, baada ya kufanikiwa katika hilo ndiyo wakatengeneza hii broad-based government (serikali ya nusu mkate) iliyopo sasa, baada ya Raila kuungana na Ruto hapo ndiyo Gen Z wakajua rangi halisi ya jamaa yaani mzee wa nusu mkate,
Chanzo kikubwa cha Rigathi kuwa impeached ni Raila, sababu Rigathi aliapa hawezi kufanya kazi na Raila kwa kua anajua jamaa yuko kimaslahi hivyo Ruto na Raila wakampiga chini, sasa siasa zikahama, kutoka kwa Raila kuwa mpinzani wa serikali na sasa kutengeneza mpinzani mpya Rigathi, silaha kubwa na pekee Ruto aliyokua anaitegemea 2027 kushinda uraisi hasa ukizingatia hakubaliki kwa Gen Z ni walau Raila ( kwakua Gen Z wanamchukia kwa kuungana na Ruto lakini ndani ya mioyo yao wanamuona hero, kwakua demokrasia waliyonayo sasa iliasisiwa na Raila), maana ana wapiga kura wengi sana nyuma yake ambao wanamfia kokote atapoenda,
Ruto alizunguka Africa nzima akimnadi Raila kwenye kiti cha AU, ili tu asigombee 2027 lakini amwachie mtaji wa watu wengi wa chama chake cha ODM wa kumsupport,
Kati ya watu wanaolia sana kimoyo moyo, nadhani Ruto ni number moja,
Raila kaacha vijana wapinzani wanaokubalika haswa mfano ni Senator wa Nairobi Edwin Sifuna, na Mbunge wa Embakasi Babu Owino, huyu Babu Owino ndiyo kipenzi cha Gen Z kwa sasa Kenya, ni vile tu bado ni kijana mdogo just 36yrs,
Kifo cha Raila ni pigo kubwa sana kwa Ruto, japo pia ni rahisi sasa kwa Ruto kuwashawishi wale ma-CS aliowateua kutoka kwa Raila(ODM) waungane nae moja kwa moja kupitia mgongo wa Kenya Kwanza Coalition,
Naumuona Ruto mwenye njia iliyojaa miiba na misumari ya kila aina 2027, japo kwa siasa za Africa anaweza kushinda tu, lakini possibly zitamwagika damu nyingi sana, ni nani atakaewatuliza vijana hawa wenye gadhabu...?
Mimi na wewe hatujui, tumwachie Mwenyezi Mungu maana yeye ndiye ajuaye nini kinachofuata baada ya kukitoa kilichopo
Naomba kuwasilisha🙏