RAIA MWEMA: CHADEMA kwafukuta

RAIA MWEMA: CHADEMA kwafukuta

Ccm wamebaki na propaganda baada ya kuona wananchi kila pembe ya nchi wanalia uchumi umesambaratika sasa ndio hivyo wanakuja na hizi takataka ili kupotezea.

Hili gazeti la raia mwema baada ya kutaka kufirisika serikali ikawapa pesa ili waendelee kuwepo sokoni wawatumie kwa propaganda zao na tunalijua hilo.

Baada ya kuja kwa mitandao ya kijamii vyombo vingi vya habari vimekuwa mahututi na hasa baada ya dikteta Magufuli kuvilazimisha vimsujudie.
 
..Katiba Mpya ni kwa ajili ya Watanzania wote, sio sahihi kuikwamisha kutokana na mapungufu ktk Katiba ya Chadema.
Watanzania wote? Mbona sisi wengine wengi tu hatuitaki
 
..Binafsi sioni tatizo au ajabu kwa Mbowe na Lissu na wengine ndani ya Chadema kuwa na mitizamo tofauti kuhusu hoja mbalimbali.

..Tuwatie moyo Chadema ktk kujenga utamaduni wa kupambanisha hoja ndani ya chama chao.

..
Walau, japo indirectly, unakiri kwamba lipo tatizo la kutokuvumilia mawazo mbadala.

Mbowe lazima abadilike, haiwezekani kila mwenye mawazo tofauti aonekane msaliti.
 
Hilo gazeti halitokaa liandike habari njema za chadema hata siku moja, atakayeiona habari njema kwenye hilo gazeti kuanzia leo anitafute.
 
Walau, japo indirectly, unakiri kwamba lipo tatizo la kutokuvumilia mawazo mbadala.

Mbowe lazima abadilike, haiwezekani kila mwenye mawazo tofauti aonekane msaliti.
Abadilike ili chadema iwe kama cuf na Nccr mageuzi??? Hiyo hatutaruhusu upimbi huo hata siku moja

Sent from my DRA-LX5 using JamiiForums mobile app
 
Hilo gazeti halitokaa liandike habari njema za chadema hata siku moja, atakayeiona habari njema kwenye hilo gazeti kuanzia leo anitafute.
Chadema kuna habari gani njema? Au zile za Mimi mbowe sijalamba asali?
 
Raia Mwema wako sahihi!

Samia ameweka mazingira mazuri ya biashara na uchumi unafanya vizuri.
Kabla hajaingia madarakani benki zilikuwa zinapata faida kiduchu na zingine kufirisika kabisa!

Mwaka 2020 benki zote kwa jumla zilipata faida ya bilioni 200+ tu. Mwaka 2022 benki zote kwa jumla zimepata faida ya bilioni 1200+

Haya ni mafanikio makubwa mno ya sera za uchumi za Mh Samia!
Sera za uchumi zinazopondisha bei za bidhaa hasa chakula kwa watu wa kawaida hazifai. Maisha yanakuwa magumu kila uchao, machawa tu ndio mnafurahia
 
Walau, japo indirectly, unakiri kwamba lipo tatizo la kutokuvumilia mawazo mbadala.

Mbowe lazima abadilike, haiwezekani kila mwenye mawazo tofauti aonekane msaliti.

..nakiri kuwepo kwa mitizamo au approach tofauti kuhusu suala la Katiba Mpya.

..Na sidhani kama hilo ni tatizo kwa Chadema, au ni jambo baya kuwepo ktk chama chochote.

..Kwa upande mwingine kuwa na mitizamo tofauti tofauti ni njia nzuri zaidi kwa chama kuelekea ktk MSIMAMO ulio bora na shirikishi.

..Nashauri tujenge utamaduni huo Bungeni, Serikalini, Vyuoni, etc.
 
Back
Top Bottom