Raia Mwema: CCM Haijui Ifanye nini na Lowassa

Raia Mwema: CCM Haijui Ifanye nini na Lowassa

Lau Lowassa angekuwa mkatoriki asingesulubiwa hivi.
 
Lau Lowassa angekuwa mkatoriki asingesulubiwa hivi.

mkuu lowasa angekuwa dini yoyote ile kwenye taasisi ya urais hafai kamwe. hayo yanasemwa huku mitaani na waumini wa dini zote,wafuasi wa vyama vyote mpaka wa ccm. napia na watu wa rika zote. wanadai kumweka lowasa ikulu ni kuruhusu kina chenge na marafiki zao kuendelea kuliibia taifa hili.
 
Mkuu Laki Si Pesa,waliamua lini mkuu?Kikao kilifanyika lini na mahali gani?Hebu tukumbushe kidogo!
mpe angalizo tu asipochaguliwa huyo mume wake je laki-nipesa atajificha wapi?
 
Kamati kuu ya CCM
1. JK Kikwete
2. Dr Sheni
3. Philip Mangula
4. Mizengo Linda
5. Seif Ali Iddi
6. Anna Makinda
7. Pandu Kificho
8. Vuai Ali Vuai
9. Combred Kinana
10. Nape Mnauye
11. Mohammed Seif Khatibu
12. Zakhia Mechi
13. Asha Rose Migiro
14. Sophia Simba
15. Sadipha Abdallah
16, Jenister Mhagama
17. William Lukuvi
18. Steven Wasira
19. Emmanuel Mchimbi
20. Pindi Mchana
21. Jerry Slaa
22. Adam Kimbisa
23. Vuai Nahodha
24. Hussein Mwinyi
25. Maua Daftari
26. Samia Suluhu
27. Salimu Ahmed Salim
28. Makame Mbarawa


Hiyo ndio List ya kamati kuu ya CCM. Je nani mwenye ujasiri wa kumpitisha Lowassa kugombea urais, kati ya hapo nani yupo tayari kuwasaliti Watanzania?
Tuachane na Mafisadi. Tanzania kwanza

cc Pasco Ritz FaizaFoxy ocampo four Lizaboni n.k

Kamati hii kuna watu hawawezi kumtupa Lowassa
JK Kikwete
Seif Ali Iddi
Anna Makinda
Pandu Kificho
Vuai Ali Vuai
Combred Kinana
Mohammed Seif Khatibu
Zakhia Megjhi
Asha Rose Migiro
Sophia Simba
Jenister Mhagama
William Lukuvi
Steven Wasira
Emmanuel Mchimbi
Jerry Slaa
Vuai Nahodha
Hussein Mwinyi
Maua Daftari
Samia Suluhu
Makame Mbarawa

Hiyo ndio List ya kamati kuu ya CCM. Yenye uswahiba na kuweza kumpitisha Lowassa kugombea urais, kati ya hapo nani ambaye hayupo tayari?
 
Last edited by a moderator:
Lowasa ni sehemu ya matatizo ya nchi hii hivyo kumchagua ni kutia chumvi kwenye kidonda.


Hahahaaaaa ati wanasema ni maumivu yanakuwa makali lakini kidonda kinapona haraka
 
Tulipokuwa tunasema 5 years ago mlikuwa mnakataa leo kabakisha miezi mitatu mnaanza kukubali, poleni.

Hiyo ni sifa kubwa sana kwa Kikwete.

Sasa wanaoona Urais ni mwepesi kuupata wacha waingie kwenye kinyang'anyiro waelewe huo urahisi wake.
 
Watanzania kukubali kumpitisha Lowassa kugombea urais na kumchagua ni kurudia maamuzi yasiyo na faida yaliyofanywa miaka 2000 iliyopita pale Wayahudi walipoamua kumsulubisha Yesu mwenye haki na kumwachia huru Baraba aliyekuwa amefungwa gerezani kwa ujambazi.

Yuko kifungoni kutokana na ufisadi alioufanya ikiwemo Richmond lakini wakati huo huo wako wagombea wengine wenye sifa ambao kwa kutokuwapendekeza ni sawa na kuwasulubisha.

Watanzania tusikubali kumwachia huru Baraba nchi na badala yake tuonyeshe ukomavu kwa kumpa haki yake ya kuendelea na adhabu ya kifungo ili yule mwenye haki apate kuwaongoza Watanzania. Yesu wa kuweza kuongoza kizazi hiki wapo wengi na inaonekana hatutaki kuwaangalia hao bali tunakodolea watu waliovunja rekodi za wizi na kuchangia kuongeza umaskini wa walalahoi.

Hivi tunahitaji ushahidi gani kuthihirisha kuwa EL hatatufaa kwa urais ilhali ameweka bayana kuwa bado anasaka utajiri. Hivi mtu tajiri kama Lowassa akisaka utajiri au kama bado anasaka utajiri maskini atakuwa wapi kama siyo shimoni. Mdomo huyanena yaujazayo moyo wa mtu hivyo tuwe na akili ya kuchambua maneno ya EL then tukafanye maamuzi ya kuwanusuru Watz.

Kwa sasa hivi wenye viwanja katika miji hawana amani kwani yule mtwaa viwanja vya mijini anautaka urais na hivyo viwanja vyao kuwa katika hatihati. Huyo ndiye Baraba mnyang'anyi anayetaka kuwa rais kwa udi na uvumba.
 
Kwa CCM Lowassa ni mtu wa kutatiza; wakimkubali wataonekana wamemuogopa wakimkata wataonekana wanamuonea...
Heri kwa CCM mara mia kumuonea kuliko Wakimkubali....kama ni lawama CCm ishapokea lawama za Wanaccm wengi tu...japo ndani ya pazia kama Raia wangeambiwa matendo ya maovu yake yake, kuwa fulani kabla ya kusomea taarifa ya madudu yake aliyoyatenda kinyume na kuinanga CCM, alishikwa na shinikizo la ghafra ...wako wengi tu wenye sura za kondoo kumbe ndani chui...
 
Mkuu siku ya kupiga kura usimpe el ndiyo dawa
 
Nasikia eti nawe ni mjumbe Wa NEC ya CCM!!!

Nimecheka Sana maana huu ni mzaha mkubwa kwa wanaCCM!!!!
Kidogoooo ubutue kombolela...siku nyingine usiludie mkuu ahahaaa
 
Hiyo ni sifa kubwa sana kwa Kikwete.

Sasa wanaoona Urais ni mwepesi kuupata wacha waingie kwenye kinyang'anyiro waelewe huo urahisi wake.
kuna mtu anashindwa kupanda ndege na kufunga mkanda?wote wameona kama jk kaweza basi hata kigwangala anaweza,utitiri wa watangaza nia ni tusi kubwa kwa kikwete.
 
Hoja haina tija coz lowasa mwenyewe hajapitishwa na CCM, ww unaongelea mambo ya kupiga kura
 
Generali Ulimwengu, tunajua msimamo wake, na ni team ya nani..sina haja ya kumwongelea...

Lowassa wa leo alipelekwa kwa Pilato ( JK wa leo ) na wafilisti kwa hasira na kelele, wanaipaaza sauti juu, asulubiwe, asulubiwe...Pilato akasema, mm sioni hatia ya mtu huyu...hana kosa...!!!

Naamini, JK ndilo linalomuuma moyoni, anajua fika, kwa damu na jasho, Lowassa hana hatia, na amempiga tafu kuliko mwana CCM yeyote, hili linamuuma sana JK, na katoa kauli ya wazi, kuwa CCM iache kudhania ikimchagua mgombea atakuwa Rais, hizo nyakati zimepitwa na wakati...lazima CCM imchague mtu anaeuzika ndani na nje ya CCM...na lazima CCM ikubali nyakati zimebadilika...!!!

Hii kauli ni shangwe kwa team Lowassa...inaonyesha JK kasoma upepo wa Lowassa ni mkubwa kuliko kawaida, na moyoni kabisa ndani kwake JK anaona Lowassa hana HATIA...so kuliko CCM ife, heri Lowassa apewe tiketi ya CCM kugombea Urais...!!! ana nguvu kubwa sana...

Na ukifuatilia matukio ya hivi karibuni, baada ya Lowassa kuweka wazi hatoki CCM, yeye ni kada mwaminifu tokea 1977, UKAWA wameyumba sana, na kuanza kutoa matamko ya UOGA NA MARUERUE, KUWEWESEKA, NA KUSEMA CJUI NN na NN...sbb WALITEGEMEA LOWASSA ATOKE CCM aende kwao UKAWA...sasa ngoma imebuma...!!!

So far, the CCM ball is 75% on Lowassa's side... i bet, mtaona NEC itakavyomchagua kwa nguvu ya AJABU...tuwe na subira, tusiandikie mate, wino upo
Ustaarabu ujenga ...matumizi ya lugha za kashifa kwa wengine sio kitu chema...cool mode..ufinyu wa fikra sasa unaweza kusomeka japo watu wakaona mjadala.
 
kuna mtu anashindwa kupanda ndege na kufunga mkanda?wote wameona kama jk kaweza basi hata kigwangala anaweza,utitiri wa watangaza nia ni tusi kubwa kwa kikwete.

Ni sifa kubwa sana kwa Kikwete na inaonesha wazi kabisa ni vipi demokrasia imekuwa kwa kasi zaidi wakati wake.
 
DN,
Umenichefua!
Uamuzi wa Lowassa kujiuzulu Uwaziri Mkuu kutokana na kuhusishwa kwake na kuingilia mchakato wa kashfa ya kampuni ya kufua umeme ya Richmond kinyume cha sheria kumeacha ladha chungu kwenye ndimi za wapenzi na mashabiki wake ndani ya CCM (bungeni na nje ya Bunge). Lowassa – kwa maoni ya baadhi ya watu – hakupaswa kujiuzulu Uwaziri Mkuu kwani angeweza kutumia nafasi aliyopewa na Spika Samuel Sitta kujibu hoja kwa hoja madai yaliyotolewa na Kamati Teule ya Bunge. Hakufanya hivyo. Badala yake aliamua kuuzira Uwaziri Mkuu katika ile hotuba yake ya “Tatizo ni Uwaziri Mkuu”.

Lowassa alifanya mojawapo ya makosa ambayo naamini atakuwa anayajutia hadi leo hii na labda kwa maisha yake yote. Ulikuwa ni uamuzi wa woga na hasira – kitu ambacho baadhi yetu kinatufanya tusiwe mashabiki wa aina ya uongozi wake. Badala ya kujibu hoja na kuonesha uongozi kwa kufafanua ni kwa namna gani kina Harrison Mwakyembe na kamati yake teule walifanya makosa Lowassa aliamua kujiuzulu. Alisema kuna jambo (kina Mwakyembe) wanalitaka na atakuwa tayari kuwapatia.

Kujiuzuru ni sifa ya Kiongozi. Kwa hili nampongeza Lowassa kwa uamuzi wake wa heshima. Tanzania leo tumefikia hatua wananchi tunalalamika hadi Rahis anatusaidia kulalamika lakini watendaji wake wana amua kuziba pamba masikio!!

Wewe huoni mataifa mengine wanacho fanya? Bado wewe unashabikia watu kutokuwajibika aidha iwe kwa makosa yao au ya walioko chini yao?? Come ooooon DN!!?

Sitamwanini Lowassa na wala sitarajii kumpa hata kura yangu awe yeye mwenyewe FISADI au mtu yeyote wa CCM lakini kwa hili nampongeza Lowassa au kwa ufisadi wake that is the big NO! CCM hawa aminiki tena, Kikwete aliwatenda wengi 2005, matumaini kibao utekelezaji mdomoni tu na tangu nimeanza kuzijua siasa za Tanzania ndani ya CCM, sioni yeyote wa kufanya mabadiliko makubwa yanayotegemea kwa maslahi ya Taifa.

Sifa ya CCM ni UFISADI, Kulindana, Rushwa (kumbuka Takrima), Chama mwanzo mwisho. Taifa kwao mwiko!
 
Kamati kuu ya CCM
1. JK Kikwete
2. Dr Sheni
3. Philip Mangula
4. Mizengo Linda
5. Seif Ali Iddi
6. Anna Makinda
7. Pandu Kificho
8. Vuai Ali Vuai
9. Combred Kinana
10. Nape Mnauye
11. Mohammed Seif Khatibu
12. Zakhia Mechi
13. Asha Rose Migiro
14. Sophia Simba
15. Sadipha Abdallah

16, Jenister Mhagama
17. William Lukuvi
18. Steven Wasira
19. Emmanuel Mchimbi
20. Pindi Mchana
21. Jerry Slaa
22. Adam Kimbisa
23. Vuai Nahodha
24. Hussein Mwiny
i

25. Maua Daftari
26. Samia Suluhu
27. Salimu Ahmed Salim
28. Makame Mbarawa



Hiyo ndio List ya kamati kuu ya CCM. Je nani mwenye ujasiri wa kumpitisha Lowassa kugombea urais, kati ya hapo nani yupo tayari kuwasaliti Watanzania?
Tuachane na Mafisadi. Tanzania kwanza

cc Pasco Ritz FaizaFoxy ocampo four Lizaboni n.k

hahahahahhah
 
Sijawahi kuona makala ya kikanjanja kama hii.
Problem ya raia mwema ni mtiririko wa makala negative dhidi ya
ya lowassa tangu mwaka jana, so hapa hakuna jipya.

Umeonae? Hawa jamaa ni wanafiki balaa.
 
Back
Top Bottom