Nimekumbuka hili shairi
Mgenisikuyakwanza, mpemchele na panza,
mtilie kifuani, mkaribishe mgeni,
Mgenisikuyapili, mpe maziwa na samli, mahaba
yakizidia, mzidie mgeni,
Mgeni siku ya tatu, jumbani hamuna kitu, mna
Kibaba tatu, pika ule na mgeni,
Mgeni siku ya nne, mpe jembe akalime, akirudi
muagane ,aende kwao mgeni,
Mgeni siku ya tano, mwembamba kama
sindano, hauishi musengenyano, asengenyao mgeni,
Mgeni siku ya sita, mkila mkajificha, mwingine
vipembeni, afichwae yeye mgeni,
Mgeni sikuya saba, simgeni ana baa, hata moto
mapaani, hutia yeye mgeni,
Mgeni siku ya nane ,njoo ndani tuonane,
atakapotokea nje, tuagane mgeni,
Mgeni siku ya kenda ,enenda mwana
kwenenda, usirudi nyuma, usirudi mgeni,
mgeni siku ya kumi, kwa mateke na mangumi,
hapana afukuzwaye ,ni yeye mgeni.ππππ
Tulitunze vema hili shairi