gfsonwin,hakuna mtu anaeweza kukupa furaha,furaha unayo mwenyewe.Hivyo ndoa haina furaha,lakini furaha ndo hisia ya juu kabisa inayomfanya mwanadamu kujisikia bora,mwenye afya na akiwa na furaha ataiona maana ya maisha.Namna ya kuipata furaha ni kujikubali kama ulivyo na kujitazama na kujipima kwa ubinadamu wako na sio kitu kingine cha nje yako.Ukishapata ridhiko la ndani utaanza kuhisi tofauti na utajiona si mwenye visirani tena.Hapo utaanza kuipata furaha.. . . . Raha ni kitu cha muda,kinakinaisha,hakuna tofauti kati ya raha na utamu.Unapopanda gari zuri au kulala kwenye kitanda kizuri unapata raha,lakini ukishazoea raha huisha. . . . Nikija kwenye swali lako,raha ya ndoa sio kitu kimoja ni vingi,baadhi umeviorodhesha hapo kwenye thread yako,ila navyo hukinai na kuna wakati mtu huiona ndoa haina maana.Yes,unaiona ndoa haina maana kwa sababu wengi kama sio wote tunawekeza kwenye vitu hivyo,tunadhani ndivyo vinamfanya mtu aifurahie ndoa.Badala ya kuwekeza kwenye raha,wekeza kwenye furaha na maswali yako yatapata majibu sahihi!