Raha ya Chakula cha mwenzi kiwe wazi

ladyfurahia

JF-Expert Member
May 10, 2011
14,753
9,568
Habarini wadau wangu wa ukweliiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!!!!
Ndo nimeingia na mada tamutamu leo ninawafunda wadada/wamama/waadogo zangu na wenzangu ambao kwa namna moja ama nyingine wamejisahau kutimiliza wajibu wao ndani ya nyumba zao wamekuwa wavivu kupitiiliza .

Mashosti hebu tuwekane sawa hivi mnatambua wajibu wenu kama wanawake katika nyumba zenu? Leo nawapa somo maridhawa kuhusu HOTPOT hiki chombo kinasaidia sana kuhifadhi chakula kisipoe ila umuhimu wake ni mkubwa sana, ila kina maeneo yake ya kukitumia sio kila mahali unakitumia tuuuuuuuuuuu bila mpangilio wake.

Mabestito jamani unapoandaa chakula chako kwa mwenzi wako jaribu kuweka manjonjo mezani kwa mpangilio unaotakiwa kwani kwenye kitchen parti hamkufundwa, Majuzi kati nilimtembelea shosti wangu maeneo Fulani hivi sitaki kutapika sana ila naleta somo hapa tujifunze wote , shostiii bila hiyana si akaleta chakula mezani tena ndani ya hotpot

Nambie hilo hotpot lenyewe wala hajalifuta vizuri kwa kitambaa kabeba kaweka mezani so shem kaja kwa meza kula mwenzangu yeye yuko amekochi anasmatika na mawasapu wala hana habari mezani pakoje, mm nikawa nachora mwenndo mzima, unavyoendelea ; heheheheiya abadani akamwita wife , bibie shostito akaenda sasa shem akamwangalia juu mpaka chini akanyanyuka na kuondoka,

Nikamfuata bidada nikamwambia shosti hujui kosa lako hapo? Bidada anashangaa na ndo kwanza anachatika hajali nikamwambia shosti utavunja ndoa yako kwa upumbavu wako, umeshindwaje kumtengea mumeo bakuli mezani kwa uzuri na ubora,

Umeweka poti liko chafu unadhani nani anaweza kula hicho chakula hata kama ni kitamu heheheheheiyaaaa akaniangalia kasha akafyonya fyoooo akaondoka , nikamwambia bidada shauriro nakupa somo unanitolea nje yasisikukute kama mtia maini ndani ya bilauri utavuruga nikajiondokea mie

Lengo la stori hiyo mabestito ni kuwaasa na kuwaonya jamani mabesttito raha ya chakula cha mwenzi wako lazima kiwe wazi kwanini nasemea hivi namaanisha kuwa unapoandaa chakula kiandae katika usafi na ubora uliototukuka sio sasambu sasambu mpaka kero kwa mwenzi wako

Hatukatai kuweka kwenye HOTPOT weka ili kisipoe ila unakitenga mezani weka kwenye bakuli kikiwa wazi cheupeeeeeee na chenye harufu murua ili kumvuta mwenzi wako awe na hamu na shauku ya kula sio kumfanya mwenzi wako aone kinyaa halafu wewe uwe unasmatika ukiachwa utasema mama paroko sikukupa somo wakati uzembe ni wako mwenyewe

shauriroooooooooooooo nimeshakutwangia utajiju ukiharibikiwa huko usije sema hakutufunda bure kumbe ni wewe mwenyewe kwa uzembe na uvivu na kujifanya kuwa upo kwenye maendeleo na utawandazi utakutandaza ukose raha inahuuuuuuuu heheheheiyaaaa

Shostito elewa kuwa raha ya chakula lazima kiwe wazi kikifunikwa hakionekani, kifunue weka kwenye bakuli kitalika kwa furaha mpaka mwenyewe utaona sasa mm nimepika,

habari ndo hiyo nawapa heheheheheeiyaaaaa. Nimeshawasomesha mwenye kujifunza achukue na asiyetaka aache kwani utakuwa na mamaporoko huko ukiburunda hahahahahahahahahyheeheheiyaaaaaaaaaaaa shosti Valentina upo oo haahahaha



Wasalamu
Ladyf
 
Kikifunikwa napo kina raha yake bwana, cha msingi ni kuzingatia usafi, alafu unamnawisha then mnasali kisha unafunua anakutana na harufu taaamu, then unampakulia vizuuri maana unajua size yake, then mnakaa mnakula.

Kama unataka kionekane basi kuna bakuli nzurii ambazo ni transparent na zina mifuniko transparent pia. Chakula kinaonekana muruaaa.

 
Makaw tena siku hizi naona hayana soko.
10f7a0654f36ae80890562313dbc7897.jpg
 
Kikifunikwa napo kina raha yake bwana, cha msingi ni kuzingatia usafi, alafu unamnawisha then mnasali kisha unafunua anakutana na harufu taaamu, then unampakulia vizuuri maana unajua size yake, then mnakaa mnakula.

Kama unataka kionekane basi kuna bakuli nzurii ambazo ni transparent na zina mifuniko transparent pia. Chakula kinaonekana muruaaa.


hatari sana! tena kuna za rangi ya pink pink hv
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom