Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 15,310
- 9,737
Ndugu zangu Watanzania,
Nimeona nitumie jukwaa hili kwa upendo,Heshima na unyenyekevu mkubwa Sana kuishauri serikali yangu kuhakikisha kuwa katika mpango wake wa kila mwaka wa kununua chakula na kukitunza, ihakikishe kuwa mwaka huu inanunua Chakula cha kutosha na kukitunza kwa umakini mkubwa Sana hususani kwa watendaji watakao kuwa wamepewa dhamani hiyo.
Ifahamimike kuwa chakula hiki hutumika kusaidia maeneo yanayo kuwa na njaa Kali na Upungufu mkubwa wa chakula kwa kukiuza kwa Bei ambayo mwananchi anaweza kumudu Bei,chakula hiki huwa msaada mkubwa Sana kwa wananchi ukilinganisha na kile kinachokuwa kinauzwa sokoni na watu binafsi.
Pia serikali yetu kupitia viongozi wetu wakiwepo wale wa kisiasa wahakikishe kuwa wanatoa Elimu ya kutosha na kuwakumbusha wananchi kutunza chakula majumbani kulingana na ukubwa wa Wana Kaya au familia,kila mmoja wetu kwa kadri ya uwezo wake ahakikishe kuwa anatunza chakula.
Wananchi wakumbushwe ili wasiuze vyakula vyote na kubaki kuhenyeke na Bei kubwa ya vyakula miezi ya huko mbele, Ni wajibu na muhimu Sana kwa serikali yetu kuhakikisha kuwa inaweka msisitizo wa kutosha katika Jambo Hilo.
Ikumbukwe ya kuwa hakuna Jambo la hatari,baya na gumu katika kuongoza serikali kwa utulivu na Amani ikiwa njaa ya chakula imetamalaki katika mamilioni ya kaya au familia nchini.Ni ngumu Sana kumuongoza au kusikilizwa na mtu mwenye njaa tumboni mwake,huwezi ukasikilizwa Wala kueleweka mbele ya watu wenye njaa.
Ni Rahisi Sana mtu mwenye njaa kushawishika kufanya vurugu au uharifu au uasi dhidi ya nchi yake,Ni Rahisi kwa mtu mwenye njaa ya chakula kuingia katika mkumbo na mtego wa kuiboa nchi yake kwa mikono yake mwenyewe. Ni Rahisi kupandikizwa chuki au vinyongo kwa watu wenye njaa ya chakula ,Ni Rahisi kwa mtu mwenye njaa kujitoa ufahamu na kufanya tukio la Aina yoyote Ile kupata kitu Cha kuponya njaa yake.
Ndio maana kwa kulipenda Taifa langu,nchi yangu na serikali yangu nimeamua kutoa ushauri huu mapema wakati msimu wa mavuno ukiwa umewadia, Naiomba Sana serikali yangu kutunza chakula Cha kutosha.
Rais wangu Samia Suluhu Hassani nakushauri kwa unyenyekevu, upendo, hekima, busara na uzalendo mkubwa Sana kuhakikisha serikali yako inatunza chakula Cha kutosha. Tunza chakula Rais wangu. Tunza na hifadhi chakula Cha kutosha mama yangu ,weka na fuatilia fedha za kununua chakula kuhakikisha zinatimiza malengo ya serikali. Tumia hata vyombo vyako na wasaidizi wako waaminifu kuhakikisha chakula kinakuwepo Cha kutosha.
Rais wangu Tunza chakula kwa kuwa wapo wenye kipato Cha chini wasioweza kujitunzia chakula na njaa ikiingia wote watakutazama na kukulilia wewe na serikali yako ,kwa kuwa wewe ndiye Rais wao,mama Yao na kiongozi wao na mwenye serikali yao. Rais wangu watu wenye njaa hawatawaliki Wala kusikiliza ,Ni watu wenye maneno na malalamiko,watakulilia na kukulalamikia Sana. Wataona ni kama umewabeba mgongoni na kuwaacha jangwani pasipo na maji Wala chakula.
Rais wangu mh mama Samia suluhu Hassani naomba na kukuomba Sana upokee ushauri wangu na kuuzingatia Sana ,maana Naifahamu vyema Sana njaa na mawazo ya mwenye njaa,Napenda Uendeleee kuongoza Taifa letu kwa Hali ya utulivu na Amani kubwa Sana pasipo malalamiko Wala maneno kutoka kwa wananchi wako, ndio maana napenda kutoa ushauri wangu katika hili. Nakuomba Sana mh Rais utunze chakula Cha kutosha kwa kuwa chakula ndio usalama wa Taifa,ndio utulivu wa serikali,ndio amani ya nchi,ndio mshikamano wetu na ndio Matumaini ya wengi.
Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
0742-676627