Rafiki yetu Cheda: Alivyopotezwa na itikadi kali ya Dini

Rafiki yetu Cheda: Alivyopotezwa na itikadi kali ya Dini

Ashampoo burning

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2023
Posts
1,296
Reaction score
3,929
Rafiki Yetu Cheda: Alivyopotezwa na Itikadi Kali ya Dini”

Utangulizi wa Kijiweni:
Basi ndugu yangu msomaji, leo ngoja nikupe story nzito ya maisha halisi ya jamaa yetu tuliyesoma naye Minaki—jina lake Francis, ila sisi tulimzoea kumuita Cheda. Hii sio hadithi ya kufikirika, ni ukweli wa kusikitisha kuhusu kijana mzuri kabisa aliyepotezwa na mikono ya itikadi kali ya kidini. Story yenyewe inaanzia Minaki, inapitia IFM hadi kwenye maficho ya ugaidi, Morogoro na hata inaishia kwenye uvumi wa Al-Shabaab. Karibu usome...
---

Minaki 2013: Mwanzo wa Safari

Tulikuwa kundi dogo la marafiki waliokuwa wameshikana sana—mimi, Cheda na wengine kibao. Tulimaliza Minaki Boys High School mwaka 2013 tukiwa na ndoto nyingi na matumaini makubwa. Mungu alijalia tukafaulu vizuri. Baada ya matokeo, mimi na Cheda tukapangiwa IFM pale Dar. Cheda alikuwa na bahati maana kaka yake mkubwa, Sedoyeka, alikuwa lecturer IFM, na baadaye akaja kuwa Mkuu wa Chuo Arusha, halafu akateuliwa kuwa boss wa Wizara ya Utalii—sasa hivi ni Profesa Sedoyeka.

Cheda alikuwa akiishi kwa kaka yake huyo. Lakini ile uhuru wa chuo na maisha ya Dar, ikamfundua. Tabia za kuvuta bangi alizojifunzia Minaki zikamkolea. Akawa anazidi kuingia ndani kwenye giza la matumizi ya madawa na marafiki wa ajabuajabu.

---
2014–2015: Kupotea kwa Cheda

Ilipofika katikati ya 2014, Cheda akawa haonekani tena chuoni. Mara unasikia yuko Mbagala, mara unasikia Arusha, lakini hakukuwa na uthibitisho. Ilikuwa kama amemezwa na hewa. Mwaka 2015, nikiwa Posta, alinipigia akanitumia ujumbe aniombe hela ya haraka, nikamtumia kama rafiki. Tukaweka miadi tukutane Survey karibu na Mlimani City, kwa rafiki yetu Sam aliyekuwa akisoma Ardhi University.

Siku hiyo tukamshuhudia mtu mwingine kabisa. Cheda aliyefika alikuwa amevaa balagha na kikofia cha kiislam, akiwa kabadilika kabisa. Huyu si yule mtoto wa Maua Seminary, yule mkristu aliyekuwa na tabasamu muda wote. Tukamuuliza vipi mkuu? Akatumbua macho, akasema ametoka kwenye giza sasa yupo kwenye nuru. Akanusuru roho zetu tusife kinyume na dini. Alituambia sisi makafiri hatufai kuwepo duniani. Tulishangaa sana.

---

2016: Taarifa za Kustaajabisha

Baada ya hapo, hatukuwahi kumuona tena Cheda. Mwaka 2016, zikaibuka taarifa za vikundi vya ugaidi maeneo ya Morogoro. Kati ya majina yaliyohusishwa, kulikuwa na uvumi mkubwa kuwa na yeye yumo. Mimi nilimaliza chuo nikasepa zangu China kutafuta maisha. Niliporudi 2019, nikaamua kufunga safari hadi Morogoro kumtafuta familia yake.

---

2019: Mazungumzo ya Kinyonge na Bibi

Nilipofika Morogoro, nikakutana na bibi yake. Mama yake hakuwepo—bibi akaniambia walishawahi kumuona kwao kwa muda mfupi lakini alikuwa mtu wa ajabu kabisa. Alikuwa anawatishia familia yake wabadili dini, alikuwa mtu wa hofu na hasira zisizoeleweka. Akawa mtu asiyejulikana kabisa nyumbani kwao.

Taarifa walizopata kuhusu hatma yake zilikua mbili:

1. Kifo Morogoro: Kuna askari mmoja alimwambia mama yake kuwa Cheda aliuawa kwenye mapambano ya vikundi vya kigaidi vilivyokuwa kwenye milima ya Morogoro. Hii inaaminika kwa asilimia 90.


2. Safari ya Namanga: Taarifa nyingine zinasema alipita Namanga kuelekea Kenya, huenda akaingia Al-Shabaab. Hii haikuaminika sana, ilikua ni fununu tu bila ushahidi kamili.

---

Hitimisho la Maumivu

Mpaka leo, mwaka 2025, miaka 9 imepita bila kujua rasmi alipo Cheda. Rafiki yetu wa utotoni, kijana mwenye akili na ndoto, alipotezwa na mikono ya itikadi kali ya kidini. Alianza na bangi, akamaliza kwenye misimamo mikali inayodanganya vijana kuwa jihadi ni njia ya wokovu.

Leo naandika hii makala sio kwa chuki na sio kwa kumhukumu, bali kwa kuelimisha. Wazazi, walimu, viongozi—tusipochukua hatua mapema, vijana wengi wataangukia huko. Cheda alikuwa mmoja wetu. Leo ni kivuli tu cha kumbukumbu.
 
Ipeleke jukwaa la hadithi na story hapa ni jukwaa la siasa.
 
Ikiwa uliwai kuslimu ama kuwa muislam ukatoka bila kutupiwa JINI(PAGAO) Mungu ana mango na wewe.
mtu akiingia tu kwenye hiyo dini asipotoka haraka mjue mshapoteza.

Islam ni cult kama ilivyo illuminate ama freeMason na ndiyo maana Cult zote ukitaka kuachana nazo zitaji hitaji uhai wako kwa namna yotote unless urejee kundini.
Ukitakq kuacha uislam,waislam watataka uhai wako.

Nb; Story hi inafanana sana na Story ya Fready(dogo wa Zimbabwe).
alitoka Zimbabwe akiwa na akili timamu na mkristo Safi kabisa akaenda Uingereza..baada ya miaka miwili hivi akakutana na vizee vya karata Tatu. trick zao ni zile zile: Yesu alikuwa ni muislam kabla hujakaa sawa unaulizwa swali lingine; ni wapi yesu aliingia kanisana etc".

basi, fready akaelekea Kibra baada kuelemewa hoja.. mawasiliano na ndugu zake yakawa ya kusuasua, ndugu wakataka kujua nini shida "why"mawasiliano ni shida..fready akawachana kuwa wao ni makafiri..status za WhatsApp zikawa ni Aya za kuran kila saa..
Ilo kwao halikuwa shida..muda ukasonga kidogo,fready hakawa hapatikani kabisa..2 yrs baadae watu wanamuona fready anatrend kwenye video akiwa kwenye Toyota zile za magaidi na uku ameshika Bendera Nyeusi yenye maneno ya rangi Nyeupe uku anawashikaji zake waarabu.

Muda si mrefu Putin naye akafanya yake(ni kati kati ya slogan maarufu ya Putin akisema" kuua magaidi ni kazi yake na kuwasamehea ni kazi ya Mungu") hii kauli ili enda na Uhai wa Fready..mzimbabwe aliyeenda kutafuta maisha Uingereza akiishia Syria.
 
Religious radicalization ni tatizo sana.
 
Prof SEDOYEKA hajawahi kumzungumzia mdogo wake?sema bro wake naye anaishi kama mwingereza effects za kusoma SCOTLAND sa hivi naona karudi tena IAA
 
Ilikuwaje akatoka kwenye ukristo wake Safi mpaka kuwa muislamu?
 
Daah! Umenikumbusha rafiki zangu wa utotoni, wamepotea kwny mazingira kama hayo, hatujui kama huko waliko wapo hai au laa! Mara wapo Kongo, mara Msumbiji, wengine wanasema baadhi walikufa Kule Mtwara mpakani, familia zao zimebaki wapweke, baadhi yao waliacha wake na watoto, inasikitisha sana, kama si kuondoka nyumbani miaka ile na kwenda kutafta maisha mikoa mingne labda na mm ningekuwa miungoni mwao mana tulikuwa ma rafiki tuliokuwa, kucheza, na kusoma pamoja, ilikuwa rahisi sana kushawishiana vitu wakati ule na akili za utoto/ujana, nikirudi home naenda kuwasalimia wazazi wao naona huruma sana na huwa wanatokwa na machozi wakiniona, nazani wanakumbuka namna tulishibana na wale wana.
 
Dini zote ni uongo. Watu wakilijua hili wataishi kwa amani sana
Dini zina roho nyuma yake, sio rahisi kuikana familia? kuna roho inaingizwa ndani yako kupitia maneno, ukikubaliana nayo umesign in kwa hiyo roho, sasa omba hiyo roho iwe roho safi.
 
Hahah! Haya maisha bhana we acha tu.

Enzi hizo utoto tupo na jamaa zetu ghafla mshikaji wetu wa mbali( huyu alikuwa Muislam wa kawaida sana) ghafla kabadilika akawa wale wa itikadi kali akaanza kuwashawishi na Waislam wenzake pale mtaani wakawa na ile itikadi kali kingine wakaanza kujifua na Martial Arts.

Haikutosha hapo wakaamua sasa kutushawishi na sisi Wakristo tuhamie kwenye dini yao wakaanza na mshikaji flani hivi jamaa alikuwa Msabato mzuri tu kweli jamaa wakafanikiwa kwa huyo mwamba wakaona mambo si ndo haya bwana.

Term hii sasa wakaja kwa nguvu zote kutushawishi na sisi wakiwa pamoja nayule jamaa Msabato😂😂😂 wakaanza porojo zao pale me nkawauliza swali, unaweza fanya chochote kile ili kuutetea Uislam? Lijamaa likajibu ndio hata kuua, moyoni nkasema hapa hamna watu kabisa nkawachenjia nkapita zangu hivi
 
Ni kama ugonjwa wa akili tuu, siasa kali hawana tofauti na walokole, mwisho wao ni kuona kila mtu ambaye haamini wanachoamini ni adui, tofauti kubwa ni upande wa kina mudi wanaona ni wajibu/ duty kuwabadilisha wengine kuwaokoa kutoka kwenye ukafiri, wanaishia kuwa magaidi na kuishia kupoteza maisha
 
Si ajabu kweli yupo hai ila ndo hivyo kaaminishwa ndgu zake ni wale katika imani tu.
 
Huu uzi umenikumbusha mwanangu Saigon alivyotuchenjia kutoka kuwa rapper wa The Diplomats mpaka kuja kuwa maalim wa dini.
 
Hayo anoyasema mtoa mada kulingana na kipindi hicho yametokea kweli vijana wa kiislamu walirubuniwa na fikra mbovu za kikhawariji ambazo ni mafundisho mabovu hayafai kufuatwa
Kuna watu walikuja kweli kueneza fikra hizo na kuwazoa vijana wa kiislamu kuwapeleka Al shabab
ilifika hatua mnamo 2012 mpk 2013 watu wengi waliacha vyuo na kuchana vyeti vyao kisa kuambiwa kusoma Secular ni ukafiri ila tushukuru jitihada zilichukuliwa na masheikh wetu wa kisalafi kuwaelimisha vijana ikiwamo kwenda vyuoni kuelimisha vijana waachane na hizi fikra potofu za kikhawariji
 
Back
Top Bottom