Rafiki yangu ameniomba nizae na mume wake

Unapaswa kulifaham hilo... Aidha anapita katika kipindi kigumu chenye majaribu. Wote mke na mume wamtumaini sn mungu asije watupa wakafarakana
 
Kuwa nao makini sana hao marafiki zako, watakuharibia familia na maisha yako usipokuwa mwangalifu
Maneno yako kweli mkuu manake nimekaa nawaza ivi huyu akipata fursa kwa mume wangu hata mvulia nguo huyu?
 
Sababu ameshaijua kama ametoa mimba mara 3!!!
Hakuna muujiza ashukuru Mungu tuu.
Mayai hayo yanakuja kwa hesabu sasa ameharibu mwenyewe asitafute visingizio
 
Surrogate system ni ngeni hapa kwetu TZ! Lkn nchi za wenzetu ni jambo la kawaida!
 
Inabidi ajue kwanza Tatizo liko WP yawezekana ukampa huyo jamaa na kwako ikashindika huyo mtoto na huku ameshakumega. Mshauri waende kwanza wajue tatizo liko wp na aangalie historia ya familia zao. Mimi nimeowa mwaka 1992 mtoto wangu wa kwanza 1997 hivi nina 9
hawana tatizo walishawahi kutoa mimba kama 3 sasa mpaka hapo inaonyesha wazi kua hawana tatizo na sio mwanamke peke yake alokwenda kutoa na mume pia alikua anamwambia hatuko tayari kua na watoto,sasaivi wako tayari na mimba haziko tayari .........
 
Sababu ameshaijua kama ametoa mimba mara 3!!!
Hakuna muujiza ashukuru Mungu tuu.
Mayai hayo yanakuja kwa hesabu sasa ameharibu mwenyewe asitafute visingizio
kweli kabisa lakini bianadamu hua hatuchoki kujiona tumeonewa.........
 
Surrogate system ni ngeni hapa kwetu TZ! Lkn nchi za wenzetu ni jambo la kawaida!
Labda niseme kila mtu na Mila za kwao tuko nje ya Tanzania sote na ni nchi zilizo endelea lakini kwa style hii mie apana ...
 
Mungu aninusuru lakini apana na sidhani kama anajua nini anasema miaka mi5 sio mingi kabisa anajitia BP bure...
Msamehe bure, hajitambui! Amekata tamaa!! Umefanya vyema kumgomea, kwa hilo ni dhahiri urafiki mbele ya safari ungekufa tu! Halafu huyo mumeo walitegemea awaunge mkono kwenye hilo???🙄
 
Ha...nikajua hujaolewa ndo maana wakaona unafaa...kumbe una mme kabisa....wamekukosea adabu...wamekuonaje kwanza hadi kukuchukulia poa kirahisi hivyo...
Wana utani na mume wa huyu dada. In fact, hawana adabu kabisaaa!!
 
Msamehe bure, hajitambui! Amekata tamaa!! Umefanya vyema kumgomea, kwa hilo ni dhahiri urafiki mbele ya safari ungekufa tu! Halafu huyo mumeo walitegemea awaunge mkono kwenye hilo???🙄
Halafu shoga yangu mie hawana mazowea na mumewangu sababau simpi shoga nafasi yakumzoea mumewangu na vile vile mumewangu hana time kama akija nyumani na akikuta niko na shogangu baada ya salam atapita chumbani moja kwa moja
sasa mazowea hana na kuna siku alinambia mume wangu ananambia napenda shoga yako anavyovaa baibui inanitia mshawasha kujua ndani ya baibui kunanini, nikamwambia njoo chumbani kwangu chukua baibui unalotaka vaa,kasema aaah
nisije kuanguka bureeeeee...
 
Ana PEPO huyo achana nae; keshajua ndoa yake imebuma sasa anataka kukuharibia na wewe!
 
Habari ya asubuhi Waungwana,

Nina rafiki yangu lakini tunaishi nchi tofauti tunakutana mara 3-5 kwa mwaka hua mie nikienda nchi anayoishi anakuja kunitembelea na yeye akija nnakoishi anafikia kwangu.

Yeye hajabahatika kupata mtoto mwaka wa 5 sasa tangu ameolewa,jana wakati tuna kula akaniomba tuonge kitu muhimu baada ya chakula,nikamwambia inshallah tutaongea.

Basi baada ya chakula na mambo mengine nikaenda kuwalaza watoto nikaenda chumbani kwake
haya nimekuja tuonge,basi akanambia kama unavyojua sina mtoto na nimejaribu dawa zote unazo
zijua zakizungu na miti shamba sijafanikiwa kupata ujauzito sasa tumeshauriyana na Mume wangu
nikamwambia changua rafiki yangu yoyote mimi ntaongea nae ili atupatie mtoto.

Mie macho niliyatoa nakutetemeka juu,nikamwambia sijafahamu unamaanisha nini ukisema rafiki yako akupe mtoto jee unataka nikupe mwanangu ule au vipi? kasema NO nataka ulale na mumewangu nilimshangaa lakini sikutaka ahisi vibaya ilibidi nijikaze nikamwambia na ilikuwaje nikawa mie?

Kasema ndani ya moyo wangu nili wish mumewangu akuchague wewe na aliposema bora wewe ndio nikafurahi zaidi.

Waungwana nilimpa maneno mengi yakumpa moyo lakini naomba nisema kua sijakubaliana na ombi lake na nimemwambia anisamehe sitoweza kufanya hicho kitu ila ntamsaidia kwa hali na mali.

Nitamuulizia kwa watu kama kuna tiba lakini kwa mimi siwezi na mumewe pia niliongea nae nikamwambia wanisamehe sitoweza,jee nimekosea kuwakatalia?

Sijapenda lakini sina choice
naipenda Family yangu sanaa na hata hili jambo silifikishi kwa Mr.
umeolewa au?
 
Alitoa mimba hata kipindi yuko na huyo mumewe wakati haja muoa,sasaivi anahangaika na i use to her usitoe mimba
sasaivi mume ana m stress anataka mtoto ....

duuuuh kumbe aliwahi kutoa bomu lipo kwa mume akapime
 
Ana PEPO huyo achana nae; keshajua ndoa yake imebuma sasa anataka kukuharibia na wewe!
Na trust me sikutegemea kama anaweza kunambia kitu kama hiki au hata kufikiria kama naweza kukubali,anajua mpaka ananambia kama wewe nawe huyo mumeo kakutia kwenye kibuyu anakufanya kwani mpaka ukapagawa? mie nacheka tuu..
 
hawana tatizo walishawahi kutoa mimba kama 3 sasa mpaka hapo inaonyesha wazi kua hawana tatizo na sio mwanamke peke yake alokwenda kutoa na mume pia alikua anamwambia hatuko tayari kua na watoto,sasaivi wako tayari na mimba haziko tayari .........
😱😱😱 CHACHA BASI
 
Habari ya asubuhi Waungwana,

Nina rafiki yangu lakini tunaishi nchi tofauti tunakutana mara 3-5 kwa mwaka hua mie nikienda nchi anayoishi anakuja kunitembelea na yeye akija nnakoishi anafikia kwangu.

Yeye hajabahatika kupata mtoto mwaka wa 5 sasa tangu ameolewa,jana wakati tuna kula akaniomba tuonge kitu muhimu baada ya chakula,nikamwambia inshallah tutaongea.

Basi baada ya chakula na mambo mengine nikaenda kuwalaza watoto nikaenda chumbani kwake
haya nimekuja tuonge,basi akanambia kama unavyojua sina mtoto na nimejaribu dawa zote unazo
zijua zakizungu na miti shamba sijafanikiwa kupata ujauzito sasa tumeshauriyana na Mume wangu
nikamwambia changua rafiki yangu yoyote mimi ntaongea nae ili atupatie mtoto.

Mie macho niliyatoa nakutetemeka juu,nikamwambia sijafahamu unamaanisha nini ukisema rafiki yako akupe mtoto jee unataka nikupe mwanangu ule au vipi? kasema NO nataka ulale na mumewangu nilimshangaa lakini sikutaka ahisi vibaya ilibidi nijikaze nikamwambia na ilikuwaje nikawa mie?

Kasema ndani ya moyo wangu nili wish mumewangu akuchague wewe na aliposema bora wewe ndio nikafurahi zaidi.

Waungwana nilimpa maneno mengi yakumpa moyo lakini naomba nisema kua sijakubaliana na ombi lake na nimemwambia anisamehe sitoweza kufanya hicho kitu ila ntamsaidia kwa hali na mali.

Nitamuulizia kwa watu kama kuna tiba lakini kwa mimi siwezi na mumewe pia niliongea nae nikamwambia wanisamehe sitoweza,jee nimekosea kuwakatalia?

Sijapenda lakini sina choice
naipenda Family yangu sanaa na hata hili jambo silifikishi kwa Mr.
Baada ya kuwalaza watoto..............hao watoto ulizalishwa na wahuni au una mumeo? Maana mpaka akufikirie wewe huenda una watoto lakini huna mume na uko poa tuu
 
Back
Top Bottom