Rafiki yangu ameniomba nizae na mume wake

NIMPENDENANI

JF-Expert Member
Nov 2, 2014
6,114
5,388
Habari waungwana,

Nina rafiki yangu lakini tunaishi nchi tofauti tunakutana mara 3-5 kwa mwaka hua mie nikienda nchi anayoishi anakuja kunitembelea na yeye akija ninakoishi anafikia kwangu.Yeye hajabahatika kupata mtoto mwaka wa 5 sasa tangu ameolewa, jana wakati tunakula akaniomba tuongee kitu muhimu baada ya chakula, nikamwambia inshallah tutaongea.

Basi baada ya chakula na mambo mengine nikaenda kuwalaza watoto nikaenda chumbani kwake haya nimekuja tuongee, basi akanambia kama unavyojua sina mtoto na nimejaribu dawa zote unazozijua za kizungu na miti shamba sijafanikiwa kupata ujauzito sasa tumeshauriyana na mume wangu nikamwambia changua rafiki yangu yoyote mimi nitaongea nae ili atupatie mtoto.

Mie macho niliyatoa nakutetemeka juu, nikamwambia sijafahamu unamaanisha nini ukisema rafiki yako akupe mtoto je unataka nikupe mwanangu ule au vipi? Kasema NO nataka ulale na mume wangu nilimshangaa lakini sikutaka ahisi vibaya ilibidi nijikaze nikamwambia na ilikuwaje nikawa mie?

Kasema ndani ya moyo wangu nili wish mume wangu akuchague wewe na aliposema bora wewe ndio nikafurahi zaidi.Waungwana nilimpa maneno mengi yakumpa moyo lakini naomba niseme kuwa sijakubaliana na ombi lake na nimemwambia anisamehe sitoweza kufanya hicho kitu ila nitamsaidia kwa hali na mali.

Nitamuulizia kwa watu kama kuna tiba lakini kwa mimi siwezi na mumewe pia niliongea nae nikamwambia wanisamehe sitoweza, je nimekosea kuwakatalia?

Sijapenda lakini sina choice naipenda Family yangu sana na hata hili jambo silifikishi kwa Mr.
 
Kwahiyo unataka kusema hicho kinaniliuu chako hujawahi kumpa mwingine zaidi ya huyo mr wako??

Mtendee hisani mwenzio mimba si itapandikizwa kwake ama mi sijaelewa?!
 
Daah hayo mambo nayaonaga tu kwenye movie kumbe yapo mpe pole sana vp kuhsu njia ya kupandkiziwa mbegu angejaribu pia hyo au kwa dokta mwaka anasaidia weng maombi pia kwa iman yang maombi yanasaidia sana nmeona watu weng wanapata watoto kwa maombi
 
yaan ungekua hujaolewa ningesema sawa tu ila kwa sababu umeolewa heshimu ndoa yako kwa maana ungekubal si kwamba ungekua umemsaidia rafik ako bali utakua umemsalit mume wako na angekuja kujua siku za uson ingeleta shida bakia na msimamo huo huo mama....
 
maisha yanaweza kuendelea vyovyote ulivyo cha muhimu ni kujikubali kwamba kitu flani siwezi basi, mpelele kwa mwanasaikolojia coz hilo jambo linamsumbua sana kama mwanamke, alienda hosp. walimwambia tatzo ni nini?
 
Habari ya asubuhi Waungwana,
Nna shogangu lakini tunaishi nchi tofauti tunakutana mara 3-5 kwa mwaka hua mie nikienda nchi anayoishi anakuja kunitembelea na yeye akija nnakoishi anafikia kwangu...
yeye hajabahatika kupata mtoto mwaka wa 5 sasa tangu ameolewa,jana wakati tuna kula akaniomba tuonge kitu muhimu baada ya chakula,nikamwambia inshallah tutaongea

basi baada ya chakula na mambo mengine nikaenda kuwalaza watoto nikaenda chumbani kwake
haya nimekuja tuonge,basi akanambia kama unavyojua sina mtoto na nimejaribu dawa zote unazo
zijua zakizungu na miti shamba sijafanikiwa kupata ujauzito sasa tumeshauriyana na Mume wangu
nikamwambia changua rafiki yangu yoyote mimi ntaongea nae ili atupatie mtoto..mie macho niliyatoa nakutetemeka juu,nikamwambia sijafahamu unamaanisha nini ukisema rafiki yako akupe mtoto jee unataka nikupe mwanangu ule au vipi? kasema NO nataka ulale na mumewangu nilimshangaa lakini sikutaka ahisi vibaya ilibidi nijikaze nikamwambia na ilikuwaje nikawa mie?
kasema ndani ya moyo wangu nili wish mumewangu akuchague wewe na aliposema bora wewe
ndio nikafurahi zaidi.

Waungwana nilimpa maneno mengi yakumpa moyo lakini naomba nisema kua sijakubaliana na ombi lake na nimemwambia anisamehe sitoweza kufanya hicho kitu ila ntamsaidia kwa hali na mali
ntamuulizia kwa watu kama kuna tiba lakini kwa mimi siwezi na mumewe pia niliongea nae nikamwambia wanisamehe sitoweza,jee nimekosea kuwakatalia? sijapenda lakini sina choice
naipenda Family yangu sanaa na hata hili jambo silifikishi kwa Mr...


Una maana kuwa wamejaribu kupandikiza pia ikashindikana?
 
Ha...nikajua hujaolewa ndo maana wakaona unafaa...kumbe una mme kabisa....wamekukosea adabu...wamekuonaje kwanza hadi kukuchukulia poa kirahisi hivyo...
 
Yeye kajuaje kama tatizo ni lake na sio mumewe
... Mwambie anitafute tujaribu mm nayy kwnz
 
Kwahiyo unataka kusema hicho kinaniliuu chako hujawahi kumpa mwingine zaidi ya huyo mr wako??

Mtendee hisani mwenzio mimba si itapandikizwa kwake ama mi sijaelewa?!
sidhani kama ni sawa anajua kama nna familia yangu na naipenda sanaa,sina fikra zakujilengesha kwa mwengine iwe kwa pesa au kwa msaada,na sijui aliwaza nini mpaka amefikia huko,kibaya zaidi mumewe pia ana shadidia mwanamme mzima..
 
Washauri waende SCOAN wakaongeze imani kwa Prophet TB Joshua mambo yao yatakaa sawa huwo ndio mtazamo wangu,kama sayansi imeshindwa sasa wajaribu na Imani.
 
Huyo mtoto utakaye zaa na mume wake atakuwaje wake. Baada ya kuzaa utamkabidhi, au mbadirishane wewe uhamie kwa mumewe
 
Inamaana wameshajua mwenye tatizo ni nani kati yao? Ukute lijamaa ndio lenye tatizo likakugeggeda bure na mimba usipate hahahahaaaa
mume sidhani sababu alikua anapata mimba na ametoa kama 3 ambazo alizo nambia..
 
Huyo mtoto utakaye zaa na mume wake atakuwaje wake. Baada ya kuzaa utamkabidhi, au mbadirishane wewe uhamie kwa mumewe
yani mkuu hata nimeshindwa kumsoma na sikutaka kuumiza kichwa,ivi kweli nizae mwanangu halafu nimpe yeye eti huyu mmm mie anapana ushoga naufe lakini siwezi kufanya...
 
Wamekukosea adabu wewe na familia yako. Mumeo akijua huo upumbavu atajisikia vibaya mno. Watafute njia zingine kama adoption au insemination lakini sio huo upuuzi waliopendekeza kwako.
Kwanza nani alimwambia atoe mimba ujanani, hayo ndio matokeo yake sasa.
 
Back
Top Bottom