Rafiki yangu alinidhalilisha nilipokuwa shuleni, nikatengwa na wanafunzi wenzangu mpaka leo napenda kukaa peke yangu tu

Visacard

JF-Expert Member
May 12, 2017
210
250
Nina tabia ya kupenda penda kukaa mwenyewe tu miaka ya sasa hivi ukilinganisha na zamani. Kufupisha stori ni kuwa miaka ya shule ya msingi nilikua napenda kujichanganya na marafiki zangu muda wote kucheza kusoma na hata kufanya kazi za nyumbani kwa pamoja.

Tulipenda kushirikiana kila kitu, tulipoingia form one niliendelea na tabia ya kujichanganya na watu sasa suala la mademu ndio liliniletea hayo yote.

Sasa mimi na jamaa yangu tulikua marafiki wa kushibana ile mbaya toka primary huko na tulitokea mtaa mmoja majirani kabisa. Sasa nilikua na demu wangu form one jamaa si akamtamani, akawa ananitania kuwa atanichukulia nikaona joke tu. One day nikamkuta kamshika na mkono kabisa tena nikaona wakikumbatiana.

Nilimind kichizi kesho nikamfata jamaa mbele ya masela nikamwambia oya hii tabia sijaipenda mbona madem wapo kibao tu kwanini usitafute wako? Ilikua nusu tupigane pale basi jamaa mmoja akatutoa pale.

Kuanzia hiyo siku ikawa ni bifu na msela ukimsalimia au ukimsemesha haongei ikawa ameweka bifu kabisa.

Jamaa alipochaguliwa monitor na baadae akawa kiranja si ndo akaanza kuniattack! Akawa anatumia ushawishi wake mpaka akaweza kunigawa na kunitenganisha na darasa lote atafanya matukio ila atahakikisha kanipakazia mimi inshort alikua ananionea mimi.

Ilifika kipindi ikawa kahakikisha kanigombanisha,kunitenganisha na darasa lote na hadi kwenye list ya wasumbufu au hata akiwa kama kiongozi ikawa akipeleka list ya wanafunzi wasumbufu au wasiofaa ananiweka mimi tu.

Ukizingatia nilikua ni mpole na nilikua nasoma kwa bidii sana na ndio kitu kilimuua pia na kwao pia walikua na uwezo sana compare na mimi nilotokea family ya kawaida japo tulikua majirani.

Ilifikia kipindi nikaona uonevu umezidi na kunidhalilisha maana kila kibaya kikinitokea atanizomea, au kunicheka kwa nguvu darasani akisema "Safi sana" alinichukia bure bila sababu yoyote.

Nakumbuka kuna siku ilitokea nikaanguka alishangilia na kucheka sana nyumbani wazazi wetu waliujua ukweli na wazazi wake walikaa wakamuuliza sababu ya kunichukia akasema hana akaambiwa apatane na mimi akagoma kabisa.

Kitu kipotee darasani ataniandika mimi ilhan mimi sikua mwizi kabisa hata mpaka leo ni agano langu sitoiba mpaka naingia kaburini.

Nilivyoona udhalilishaji na visa vyake vimezidi kwa sababu tu alikua na ushawishi darasani niliona tu ni bora nianze kujitenga na darasa na kuamua kukaa mwenyewe mwenyewe tu.

Maisha ya mimi kukaa mwenyewe yalianzia hapo hadi nikazoea miaka 3 mfululizo hadi tulipofika form 4 siku moja alinifata mwenyewe akaniomba msamaha nilimsamehe ila ilikua tayari ni too late nilikua tayari nishazoea ile tabia ya upweke upweke tu.

Wanafunzi wenzangu walikuja kugundua ukweli wote wakati tunamaliza kidato cha nne kwamba rafiki yangu ndio alikua anafanya matukio yote yale niliokua napakaziwa mimi kwasababu pia kuna rafiki yake mmoja walikorofishana ndio akanipasha ukweli wote kuwa jamaa ndio alikua ananihujumu.

Basi ndo hivyo tangu hicho kipindi sipendi kuchanganyika na watu kivileeee japo ni muongeaji sana ila muda mwingi napenda kujifungia tu geto yaani ni kuwa huwezi kunikuta eti kijiweni na wanaume wenzangu tunapiga stori no hiyo ni ndoto nitatoka nitaenda dukani na kurejea ndani tu.

Mpaka leo ninaishi hivyo nina marafiki wa kiume wa juu juu tu ile basi tu na hata tukikutana ni salamu tu na kuondoka nina rafiki mmoja tu namuamini na ndio kila kitu kwangu tena ni msichana. Huyu msichana ndio rafiki yangu wa dhati anayenielewa kiufupi anajua kila kitu kuhusu mimi a to Z.

Nina mengi ya kueleza nitawaeleza yote hivi karibuni hili jambo nikikumbuka huwa nalia sana hapa naandika huku nikiumia sana.
Sent using jamii forums mobile a
pp
 

TANMO

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
9,407
2,000
Umekuwa victim wa Bullying (Udhalilishaji). Shukuru Mungu hata uko hai mpaka sasa. Wengine huchukua hata maamuzi ya kujitoa uhai.

Kwetu Tanzania Bullying ni jambo la kawaida kiasi kwamba hata Viongozi wakubwa wanaweza kum-bully mtu hadharani na tukashangilia kama Mazuzu.

Nchi zilizoendelea wanajitahidi sana kupambana na Bullying. Maana huua kabisa mfumo wa maisha ya mtu au ndoto zake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Visacard

JF-Expert Member
May 12, 2017
210
250
Umekuwa victim wa Bullying (Udhalilishaji). Shukuru Mungu hata uko hai mpaka sasa. Wengine huchukua hata maamuzi ya kujitoa uhai.

Kwetu Tanzania Bullying ni jambo la kawaida kiasi kwamba hata Viongozi wakubwa wanaweza kum-bully mtu hadharani na tukashangilia kama Mazuzu.

Nchi zilizoendelea wanajitahidi sana kupambana na Bullying. Maana huua kabisa mfumo wa maisha ya mtu au ndoto zake.

Sent using Jamii Forums mobile app
Niliteseka sana mungu ndo anajua
Sent using Jamii Forums mobile app
 

EvilSpirit

JF-Expert Member
Jun 15, 2017
3,500
2,000
Huyo rafiki yako kwa sasa lazimabatakuwa amejiunga na kikundi cha wachawi sehemu fulani
 

snowhite

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
15,959
2,000
Una shida kubwa sana ya identity kijana!
Sijui hata tunakusaidiaje!
Yes, pengine shida ilianzia hapa ila dah!
Mungu akusaidie, tunatoka kwenye changamoto za kila aina kwenye mahali tunapita na Maisha tunapitia.
Ila namna ya kurespond kwenye hizo changamoto na kuendelea afterwards ni uchaguzi binafsi!

Umekubali sana huu utambulisho nafsi!
 
  • Thanks
Reactions: amu

DREAMBOY

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
1,851
2,000
Fanya jambo kwanza, jiamini ila penda kusikiliza watu wanapoongea nenda karibu yao ,uschangie ila tabasamu tu....jibu ulichoulizwa ,ukiwa hukijua tabasamu tu.......itaendelea
 

vexozanzhu

JF-Expert Member
Mar 1, 2019
327
500
Siku nyingine ukiwa bullied stand bold na wewe rusha kombora au fanya tukio konki lisilotegewa, mengine yatajisort huko mbele kuna sentensi fupi mfano Nitakachokufanya utajuta, Utasimulia Usiku hutapita Nitakuendea yani ulikosa kabisa sentensi au unamtafuta mtu akiwa peke yake unampa tamko au tangazo takatifu
 

Visacard

JF-Expert Member
May 12, 2017
210
250
Una shida kubwa sana ya identity kijana!
Sijui hata tunakusaidiaje!
Yes, pengine shida ilianzia hapa ila dah!
Mungu akusaidie, tunatoka kwenye changamoto za kila aina kwenye mahali tunapita na Maisha tunapitia.
Ila namna ya kurespond kwenye hizo changamoto na kuendelea afterwards ni uchaguzi binafsi!

Umekubali sana huu utambulisho nafsi!
Nidadavulie kidogo

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Visacard

JF-Expert Member
May 12, 2017
210
250
Umekuwa victim wa Bullying (Udhalilishaji). Shukuru Mungu hata uko hai mpaka sasa. Wengine huchukua hata maamuzi ya kujitoa uhai.

Kwetu Tanzania Bullying ni jambo la kawaida kiasi kwamba hata Viongozi wakubwa wanaweza kum-bully mtu hadharani na tukashangilia kama Mazuzu.

Nchi zilizoendelea wanajitahidi sana kupambana na Bullying. Maana huua kabisa mfumo wa maisha ya mtu au ndoto zake.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimekutana na ulichokisema
IMG_20200311_173945_089.JPG


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Top Bottom