Visacard
JF-Expert Member
- May 12, 2017
- 233
- 215
Nina tabia ya kupenda penda kukaa mwenyewe tu miaka ya sasa hivi ukilinganisha na zamani. Kufupisha stori ni kuwa miaka ya shule ya msingi nilikua napenda kujichanganya na marafiki zangu muda wote kucheza kusoma na hata kufanya kazi za nyumbani kwa pamoja.
Tulipenda kushirikiana kila kitu, tulipoingia form one niliendelea na tabia ya kujichanganya na watu sasa suala la mademu ndio liliniletea hayo yote.
Sasa mimi na jamaa yangu tulikua marafiki wa kushibana ile mbaya toka primary huko na tulitokea mtaa mmoja majirani kabisa. Sasa nilikua na demu wangu form one jamaa si akamtamani, akawa ananitania kuwa atanichukulia nikaona joke tu. One day nikamkuta kamshika na mkono kabisa tena nikaona wakikumbatiana.
Nilimind kichizi kesho nikamfata jamaa mbele ya masela nikamwambia oya hii tabia sijaipenda mbona madem wapo kibao tu kwanini usitafute wako? Ilikua nusu tupigane pale basi jamaa mmoja akatutoa pale.
Kuanzia hiyo siku ikawa ni bifu na msela ukimsalimia au ukimsemesha haongei ikawa ameweka bifu kabisa.
Jamaa alipochaguliwa monitor na baadae akawa kiranja si ndo akaanza kuniattack! Akawa anatumia ushawishi wake mpaka akaweza kunigawa na kunitenganisha na darasa lote atafanya matukio ila atahakikisha kanipakazia mimi inshort alikua ananionea mimi.
Ilifika kipindi ikawa kahakikisha kanigombanisha,kunitenganisha na darasa lote na hadi kwenye list ya wasumbufu au hata akiwa kama kiongozi ikawa akipeleka list ya wanafunzi wasumbufu au wasiofaa ananiweka mimi tu.
Ukizingatia nilikua ni mpole na nilikua nasoma kwa bidii sana na ndio kitu kilimuua pia na kwao pia walikua na uwezo sana compare na mimi nilotokea family ya kawaida japo tulikua majirani.
Ilifikia kipindi nikaona uonevu umezidi na kunidhalilisha maana kila kibaya kikinitokea atanizomea, au kunicheka kwa nguvu darasani akisema "Safi sana" alinichukia bure bila sababu yoyote.
Nakumbuka kuna siku ilitokea nikaanguka alishangilia na kucheka sana nyumbani wazazi wetu waliujua ukweli na wazazi wake walikaa wakamuuliza sababu ya kunichukia akasema hana akaambiwa apatane na mimi akagoma kabisa.
Kitu kipotee darasani ataniandika mimi ilhan mimi sikua mwizi kabisa hata mpaka leo ni agano langu sitoiba mpaka naingia kaburini.
Nilivyoona udhalilishaji na visa vyake vimezidi kwa sababu tu alikua na ushawishi darasani niliona tu ni bora nianze kujitenga na darasa na kuamua kukaa mwenyewe mwenyewe tu.
Maisha ya mimi kukaa mwenyewe yalianzia hapo hadi nikazoea miaka 3 mfululizo hadi tulipofika form 4 siku moja alinifata mwenyewe akaniomba msamaha nilimsamehe ila ilikua tayari ni too late nilikua tayari nishazoea ile tabia ya upweke upweke tu.
Wanafunzi wenzangu walikuja kugundua ukweli wote wakati tunamaliza kidato cha nne kwamba rafiki yangu ndio alikua anafanya matukio yote yale niliokua napakaziwa mimi kwasababu pia kuna rafiki yake mmoja walikorofishana ndio akanipasha ukweli wote kuwa jamaa ndio alikua ananihujumu.
Basi ndo hivyo tangu hicho kipindi sipendi kuchanganyika na watu kivileeee japo ni muongeaji sana ila muda mwingi napenda kujifungia tu geto yaani ni kuwa huwezi kunikuta eti kijiweni na wanaume wenzangu tunapiga stori no hiyo ni ndoto nitatoka nitaenda dukani na kurejea ndani tu.
Mpaka leo ninaishi hivyo nina marafiki wa kiume wa juu juu tu ile basi tu na hata tukikutana ni salamu tu na kuondoka nina rafiki mmoja tu namuamini na ndio kila kitu kwangu tena ni msichana. Huyu msichana ndio rafiki yangu wa dhati anayenielewa kiufupi anajua kila kitu kuhusu mimi a to Z.
Nina mengi ya kueleza nitawaeleza yote hivi karibuni hili jambo nikikumbuka huwa nalia sana hapa naandika huku nikiumia sana.
PART TWO
Maisha yangu yanaenda hivyo hivyo najilazimisha kuchanganyika na washkaji kwa kujiforce na kupretend tu nina rafiki mshikaji wangu wa kiume mmoja tu na napendaga tukae naye tu tupige stor huwa sipendi marafiki wengi kwa kua sipo interested na masela nina huyo mshkaji mmoja tu wa kiume na ndo namchukulia km rafik yangu wa pekee wa kiume huyu mtu ananijua anajua mapungufu yangu na ananichukulia km ndugu yake kbs....huwa namuona km faraja yangu tu yaani rafik wa kiume peke yake
Ananivumilia mengi sana kutoka kwangu na huwa hayasemi kbs ni siri zangu anatunza tu na huwa hasemi popote hata tugombane vp huwa hasemi public tukiwa public au na washkaj hata km tulipishana au kugombana bas tutacheka tu pale ili watu wasijue kinachoendelea
Huwa namuomba mungu tubaki washkaji milele tusizinguane na nashukuru anaelewa hali yangu na ananifundisha jinsi ya kukabiliana na mazingira na jinsi ya kuishi na watu bila watu kujua mapungufu yangu au udhaifu...kupitia yeye nimeweza angalau nachanganyika na washkaji japo najilazimisha maana mara ya kwanza nilikua nikichanganyika siongei nasikiliza tu mazungumzo yaani nikiwa nae tu wawili ndo nitaongea na najihisi huru lakini akagundua akanambia niwe naongea na kuchangia mada nikawa naongea na kuchangia mada na kucheka na watu na kutaniana na washkaji influence yangu ikaongezeka hadi wana wakawa wananichukulia km msela wao wa muhimu ....
Sent using jamii forums mobile a
pp