Rafiki yako leo ndio adui yako mkubwa kesho linapokuja suala la maslahi

nyboma

JF-Expert Member
Aug 29, 2021
1,193
2,000
Tuwe makini sana na hawa tunaowaita marafiki zetu wa faida, hawa hawa ndio hugeuka kuwa mwiba mkali katika maisha yetu hasa mkipishana kidogo kwenye masuala ya maslahi.

Rafiki huyu huyu ndio anaweza kuwa sumu ya kukuondoa hata uhai kisa maslahi, mwisho kabisa tusiwaamini sana hawa tunaowaita marafiki wa faida.

Na ikitokea wewe ni mtu wa vyombo, jitahidi sana pale unapotoka kwenda “wash room” ikitokea umeacha kinywaji mezani jitahidi sana kinywaji kile unaporudi mezani ukimwage ama fungua bia nyingine.

Huku kwenye starehe ndio tunalishwa vitu vya ajabu na marafiki ambao tumetokea kuwaamini sana katika maisha yetu hapa duniani.
 

nyboma

JF-Expert Member
Aug 29, 2021
1,193
2,000
siyo rafiki tu, hata jirani na ndugu.
Ndugu labda wa damu ya mbali ama ukoo wa mbali ndugu wa nitoke utoke huu uhuni huwa ni ngumu kutokea.

Kuna mdau alishawahi leta ushuhuda humu jinsi alivyoshughulika na mhuni mmoja ambaye alimpiga kipande mzee wake, hapa nakupa mfano tu ndugu kwenye matatizo huwa wanashikana sana.

Huyu member alikiri aliwashughulikia ipasavyo wabaya wa mzee wake kimyakimya wote walipotea kiutani utani.
 

Nielsen

JF-Expert Member
Sep 10, 2021
275
1,000
Una marafiki wanaothamini marafiki, huku makazini fitina nje nje boss.
Ni kweli kabisa ila kwangu Baba angu ni role model wangu na najiona kabisa nimemfuata yeye.

Sina tamaa ya pesa wala mafanikio ya mtu.

Eg. Mzee wangu alikua huko Oman akakutana na mdada kutoka Burundi, yule mdada inaonekana alikua anateseka sehemu aliyokua anaishi.

So yule dada alimpatia baba fedha milioni kadhaa amfichie na baba alikuja nazo huku Tz imagine mtu hamfahamini mmekutana tu huko abroad.

After year yule mdada alirudi kwao burundi akawasiliana na mzee akaja Tanzania. Akaja akapatiwa pesa zake zote bila shida, ingekua mtu wa mwingine kama watu dar maneno mwngi wangemdhurumu huyo dada
 

nyboma

JF-Expert Member
Aug 29, 2021
1,193
2,000
Ni kweli kabisa ila kwangu Baba angu ni role model wangu na najiona kabisa nimemfuata yeye.
Sina tamaa ya pesa wala mafanikio ya mtu...
Upendo wa ajabu, bila shaka kile kiasi cha fedha kiliongezela pia kwa huyo dada wa kutoka burundi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom