Rafiki wa kike wa mume wangu ananitesa

Rafiki wa kike wa mume wangu ananitesa

Iko hivi..... Rafiki wa bf wangu aligeuka kuwa best friend wangu. Then ubest ukazaa feelings kali kweli kweli. Tukashindwa kujizuia, ikabidi nimuache bf niwe na rafiki yake[emoji85][emoji85][emoji85][emoji85]
Dadeq!!!

Mungu anawaona wanawake kudadeq...
 
Pole Sana ndoa zinachangamoto nyingi Sana hii unaweza Iona kubwa ila kuna makubwa zaidi ya hayo yako.

,Kama unaona huwezi kuvunja hayo mahusiano, bado unaipenda ndoa yako jifunze kudharau, mdharau mumeo na huyo Dada, simu ya mumeo Ione Kama Bomu LA machozi, kuwa busy na maisha yako hapo nyumbani na chuoni. Akiwa busy na simu yake usiku na wewe washa yako cheza hata game ya nyoka . Vaa vizuri pendeza weekend tafuta mitoko huna ,nenda chuo huko kazuge zuge.

Usimuulize chochote kuhusu huyo rafiki yake jifanye Kama huoni japo inauma ila ndio dawa kadri unavyolizungumzia hill swala yeye anapata kiburi na sifa .

Badilisha mfumo wa maisha yako , iko siku atakuuliza au kukudodosa kwanini huna habari naye humfatilii jibu ni moja siwezi kuwafatilia MTU na rafiki yake. Huku ukiendelea na utaratibu wako wa awali .
Asee hii n dawa tosha
 
Nimekuwa mfuatiliaji wa mikasa ya watu humu leo na mimi nikaona nilete jambo langu linalonitesa kwa muda mrefu ili nijue nini cha kufanya. Mimi ni binti niko ndani ya ndoa, wakati naolewa mume wangu alikua na rafiki yake wa kike ambaye wenyewe wanadai urafiki wao ni wa kawaida tu kwani wanajuana muda mrefu. sasa tatizo huu urafiki wao umekuwa kero kwangu yani ni ule urafiki uliopitiliza kiasi kwamba kilasiku nikiangalia kwenye cm ya Mr lazima nikute wamewasiliana hata mara 50 text ndo usiseme. Kila sehemu wanaenda wote na huyo binti yani kama kumbikumbi mimi niko chuo wakati mwingine nikiwa chuo nikirudi hom namkuta huyo binti na Mr sebuleni inamaana ana courage ya kuja kwangu mimi nikiwa sipo, mara nyingine weekend tuko nyumbani na Mr, binti anampigia Mr cm njoo nyumbani kwangu ule nimepika, mume naye kilasiku lazima aripoti nyumbani kwa binti, mara binti aje nyumbani kumpitia Mr amsindikize sehemu, wakati mwingine tumelala weekend asubuh saa 1 binti kapiga cm kwa mr unafanya nini amka twende kwa fulani {mshikaji wao} yani full tafrani hana adabu kabisa ila nilichogundua ni kua mr nae ndo anampa ujeuri coz kuna kipindi niligombana sana na huyu binti kuhusu tabia zake huwezi amini alinijibu kuwa mimi siwezi kuwatenganisha kamwe nikitaka nimwambie mume wangu ndio ampige yeye marufuku kua na ukaribu nae ila sio mimi. Jamani cm wanapigiana mpaka saa 6 usiku. wenyew wanadai wao ni marafiki wa kawaida tu na hakuna kinachoendelea. nimejaribu kuuvunja urafiki huo unaoniumiza nimeshindwa mimi wenyewe hawana hata habari. Je kuna urafiki wa aina hii kweli kati ya mwanamke na mwanaume tena mume wa mtu? kwanini kusiwe na mipaka jamani..Huyo mwanamke ni mjeuri hatari ukimwambia anakujibu kwa dharau sana, mume naye ndo kwanza hana habari nisaidieni jamani nifanyaje?
wewe unaweza Kuwa na mpenzi ambaye anamke ukafanya hivyo kwake?. Mapenzi hayafichiki, huo wasiwasi wako tu na kinachokutesa ni wivu wako. Ukiwa Huru Nao Wala hautapata maumivu. Na mahusiano ya kimapenzi hayawi hivyo. Relax mama.
 
wewe huna marafiki wa karibu kwani? huyo mumeo ni mwanachuo nayeye?? kazi kweli kweli
 
Seems huyo demu hana njemba wa kum-keep busy! Kuwa naye rafiki halafu umkuwadie kwa jamaa awe busy na baby wake otherwise nachoweza kukuambia kwa sasa ni kwamba lazma wana mahusiano.
 
Huwezi ka camp moja na wasafi hahah! Unamuacha mpenzio kisa rafiki yake duh! Huruma basi
Mbona mimi hunionei huruma sasa kukaa ktk mahusiano huku moyo uko kwa mwingine!!! Nawe mbinguni huendi😂😂😂😂
 
Mwanamke anaweza kuwa na urafiki na mwanaume ila mwanaume hawezi kuwa na urafiki na mwanamke,
Ipo siku atamla tu tena mchana kweupe na jua linawaka.

Wewe upo chuo huna marafiki wa kiume?
 
hakunaga urafiki kati ya mwanaume na mwanamke jiongeze dada.....na iko hivi ukigombana na huyo rafiki wa mpenzi wako kubali kumpoteza hata mumeo sababu inaonesha mumeo anamkubali sana huyu rafiki yake kuliko wewe

chakufanya nawe anzisha safari hata za uongo uongo na muombe mumeo akusindikize kupunguza urafiki wao
 
Aisee Una moyo yaani Unaibiwa huku unaona.
 
kwani nini shida me nina marafkki kibao wa kike na sijawahi kuwagonga
 
Back
Top Bottom