Rafiki wa ex wangu ananitaka niwe mkewe

Rafiki wa ex wangu ananitaka niwe mkewe

Wanawake kwa namna hii mtasema sisi tunawajibu vibaya. Sasa wewe kwa akili yako kweli mtu hauna mahusiano nae ingawa ulikuwa unamjua, kaona umeachana na mchumba ako, anakuja anakupiga ofa ya ndoa baada ya mwaka mmoja na wewe usivyofikiri unakimbia mbio hadi Jf kuomba msaada wa kimawazo tena kwa mkwara mzito wa kutokejeliwa. Mengine muwe mnayafikiria na kuyanena ndani ya nafsi zenu, msiwe wavivu kiasi hiko!
 
Inawezekana Tu, Tuliona Diamond Alikuwa Mpenzi Wa Worlper Kisha Harmonize Akadili Na Ex Wa Bosi Wake(Worlper).
Hivi unaweza kukaa na watu serious ukaleta sampling za hawa kina Diamond na wenzake kwenye swala la mahusiano kwamba kuna jema lolote la kujifunza kutoka kwao?
 
Wanawake kwa namna hii mtasema sisi tunawajibu vibaya. Sasa wewe kwa akili yako kweli mtu hauna mahusiano nae ingawa ulikuwa unamjua, kaona umeachana na mchumba ako, anakuja anakupiga ofa ya ndoa baada ya mwaka mmoja na wewe usivyofikiri unakimbia mbio hadi Jf kuomba msaada wa kimawazo tena kwa mkwara mzito wa kutokejeliwa. Mengine muwe mnayafikiria na kuyanena ndani ya nafsi zenu, msiwe wavivu kiasi hiko!
Yan wewe, usidhani mtu kuleta kitu huku ameshindwa kusolve, binafsi najitambua sana tu kuliko inavyoweza kufikiria. Kila kitu tungekua tunamalizana na akili zetu hili jukwaa lingeota ukurutu. Unadhani b4 jf sikuwah pata matatizo had hapa nilipofikia? That's y nimeeleza kitu kilivyo na kueleza msimamo wa ubongo wangu.
Tatzo mnaparamia kujibu bila kujua mleta mada anahitaji nn. Hili sio langu tu, kuna watu ambao wanakutwa na haya wanashindwa wafanyeje, na kumbuka penye wengi kuna mengi.

Anyway, asante pia kwa kusoma post yangu na kujibu ulichowiwa kujibu.
 
Aisee unaroho mbaya balaa yaan miaka miwili jamaa hajakamua wee ulitegemea nn kampata anaejua maana ya mwanaume
 
ha ha si unajua wanawake yeye siyo bikra wala nini,wengine anawapa lakini mwingine anamnyima ili kuforce ndoa
Mtu mwenye malengo ya kuoa, hafai kupewa papuchi. Anapaswa kunyimwa ili awe na "muhu" wa kutimiza malengo yake. Lakini akipewa akala, ndipo "speed gorvaner" huzuia mwendo kabisa.
Mchumba kama 'anashida zake' azielekeza kwa wengine, lakini mchumba si wa kupewa uroda, adi atapotimiza malengo yake.
 
Hello, habari zenu wapendwa? Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, nilikua na mchumba angu (sio mpenzi na hatukuwahi kukutana kimwili) ambaye tumedumu kwa miaka miwili, hatukuwahi kugombana wala sikumfanyia kosa lolote kwa mtazamo wangu, nilimjali kwa kila kitu hadi marafiki zake wakawa wanamwambia kwamba wangetamani na wachumba wao wawe kama mimi.

Nilimpenda kwa vitendo, nilijitoa sana kwake, and alijua kwamba kweli nampenda. Sasa miezi kama miez 5 ilopita, alianza kumfukuzia dada mmoja hv, nilipomuuliza alinijibu vibaya vibaya, nikamvumilia bila kupunguza upendo wangu kwake, lakini kadri siku zilivyoenda aliendelea kuwa karibu sana na dada yule. Niliamua kumuuliza yule dada kama ana mahusiano na mchumba angu, alikataa kabisa japo alikiri kwamba alitongozwa na mchumba angu.

Lakini kwa walivyokuwa karibu sana, ilionekana tayari wana mahusiano. Hivi juzi tu nilipomuuliza mchumba angu khs mipango yetu alinambia kwamba "kama bado ulikua na malengo na mm delete, siwezi kumsaliti (........)wangu" alitaja jina lake, jambo ambalo liliniuma sana. Sikulia sababu nilikua nishaona direction ya uhusiano wetu. Bas, nilikubaliana na matokeo sababu sipendi kumlazimisha mtu ktk mahusiano.

Sasa, kazi ipo hapa... Mmoja wa marafiki za x wangu walioujua uhusiano wetu vyema anataka anioe (kwa mujibu wake). Nimemuuliza maswali baadhi lakini kubwa likiwa "unawezaje kumuoa mtu ambaye kabisa unajua alikua ni wa rafiki yako wa karibu sana"?
Huyu kaka amenijibu kwamba CV yangu inajiuza, anapenda nilivyokua namtendea mchumba angu, na anataka anioe next year.

Hapa nimebaki dilemma, hivi kweli ni busara kuolewa na rafiki wa ex wako? Ktk moyo wangu sidhani kama nampenda maana bado nina mawazo sijatulia kias cha kuanzisha mahusiano tena. Nahitaji busara zenu wapendwa. Busara zenu pamoja na maombi nayofanya yatanipa mwisho mzuri.

Kwa wenye midomo iso tohara tusameheaneni tu. Hili halinisaidii tu mleta mada bali na wengine kama huyu mleta mada.
Tazama kwa makini dhamira!
ahadi ya ndoa ni njia nyepesi sana kuanzishia mtongozo hasa kwa mwanamke unayemuheshimu au unayefikiri kuwa ana misimamo Fulani migumu au wa aina yako (ambaye anahitimisha uhusiano na mtu unayemfahamu)!
neno nataka kuoa linaweza lisimaanishe ndoa! yawezekana ni njia rahisi ya kudai papuchi, inawezekana ukitoa mzigo tu, jamaa anaweza ku-hit akala kona!
mwanzo ulisema rafiki wa jamaa zako walikuwa na wapnzi wao, huyu mpenzi wake amempeleka wapi sasa? asikwambie wewe ni bora kuliko aliyekuwa naye!
out of topic, jamaa (your x) kwanini hukumpa mzigo? yawezekana ndio sababu za kukimbia? kwanini unaanzisha mahusiano ya kimapenzi na mtu ambaye hujihusishi naye kingono? - kuna hii Imani kuwa unaweza kuwa na mtu lakini sio lazima u-do!
kidini (uislam au ukristo) mahusiano haya yenye jina la upenzi hayapo! ukihitaji kwenda huko olewa full stop!
kwetu watu wa mataifa, uhusiano wa upenzi bila ya kutiana haupo, ukidhani upo fikiri tena, jamaa unayekaa naye hadi saa 6 usiku mmekumbatiana tu bila ya ku-do, wengi huwa na michepuko ya kushikia mahusiano yale serious, lkini huwa tunapoza machungu kwa less serious relationships, wanaume wengi watanielewa!
ni bora uwe mtu wa aina moja, mtu wa kidini, just stick na principles za dini au kama wewe wa kitaa, basi acha kujidanganya, hakuna uhusiano huo ulioutambulisha mwanzo wa topic yako! often kwa wanaume hau-exist!
 
Yaani ni bandika bandua? Kama umeachana Na huyo bf wako, tulia kwanza. Vuta pumzi, punga upepo akili itulie. Halafu utafanya maamuzi badae. Usifanye maamuzi wakati uko desperate ama ukiwa Na huzuni
 
Duh!dada una roho ngumu yaani huyo x wako ulimfanya mpenzi mtazamaji kwa miaka miwili?Enewei hata ningekuwa mimi ningejikatia zangu tamaa mapema tu ht miezi miwili isingefika ila na huyo mpya anataka ndoa bila dating ht kidgo kweeeeli?
 
Miaka yote haujampa papuch kwnn?mwenzio kampa jamaa kanogewa.ila ushaur wng sikiliza moyo wako unataka nini.
 
Utu wangu n zaidi ya hcho unachofikiria. Kama kweli mtu ana lengo la kuoa, kwann atake ngono kwanza wakati huduma hyo atapata tu akioa? Kuna ulazima gani wa kufanya haraka kuonjana onjana?
Nn anataka mbuz kwenye gunia?
 
Jamaa ni mvumilivu sna anahitaji pongezi miaka miwili ajakugegeda?Huyo ni mwanaume wa pekee sana
 
Mkishachoka hamna anayehangaika na ninyi mnaanza kutafuta wachumba kila sehemu. Ila kwa sasa ukifuatwa humpendi endelea kuwa na subira kila wakati ukuta make up huwa zinadunda
 
Pole sisteri...
Naona unajiweka mwenyewe Kwenye Dilema..
Uchumba huisha na maisha yanaendelea, huyu ni rafiki wa aliyekuwa mchumba wako binafsi sioni tatizo.
Jambo la msingi ni kuangalia tabia na nia safi ya huyo kijana.
Kila la kheri sisteri.
 
Hello, habari zenu wapendwa? Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, nilikua na mchumba angu (sio mpenzi na hatukuwahi kukutana kimwili) ambaye tumedumu kwa miaka miwili, hatukuwahi kugombana wala sikumfanyia kosa lolote kwa mtazamo wangu, nilimjali kwa kila kitu hadi marafiki zake wakawa wanamwambia kwamba wangetamani na wachumba wao wawe kama mimi.

Nilimpenda kwa vitendo, nilijitoa sana kwake, and alijua kwamba kweli nampenda. Sasa miezi kama miez 5 ilopita, alianza kumfukuzia dada mmoja hv, nilipomuuliza alinijibu vibaya vibaya, nikamvumilia bila kupunguza upendo wangu kwake, lakini kadri siku zilivyoenda aliendelea kuwa karibu sana na dada yule. Niliamua kumuuliza yule dada kama ana mahusiano na mchumba angu, alikataa kabisa japo alikiri kwamba alitongozwa na mchumba angu.

Lakini kwa walivyokuwa karibu sana, ilionekana tayari wana mahusiano. Hivi juzi tu nilipomuuliza mchumba angu khs mipango yetu alinambia kwamba "kama bado ulikua na malengo na mm delete, siwezi kumsaliti (........)wangu" alitaja jina lake, jambo ambalo liliniuma sana. Sikulia sababu nilikua nishaona direction ya uhusiano wetu. Bas, nilikubaliana na matokeo sababu sipendi kumlazimisha mtu ktk mahusiano.

Sasa, kazi ipo hapa... Mmoja wa marafiki za x wangu walioujua uhusiano wetu vyema anataka anioe (kwa mujibu wake). Nimemuuliza maswali baadhi lakini kubwa likiwa "unawezaje kumuoa mtu ambaye kabisa unajua alikua ni wa rafiki yako wa karibu sana"?
Huyu kaka amenijibu kwamba CV yangu inajiuza, anapenda nilivyokua namtendea mchumba angu, na anataka anioe next year.

Hapa nimebaki dilemma, hivi kweli ni busara kuolewa na rafiki wa ex wako? Ktk moyo wangu sidhani kama nampenda maana bado nina mawazo sijatulia kias cha kuanzisha mahusiano tena. Nahitaji busara zenu wapendwa. Busara zenu pamoja na maombi nayofanya yatanipa mwisho mzuri.

Kwa wenye midomo iso tohara tusameheaneni tu. Hili halinisaidii tu mleta mada bali na wengine kama huyu mleta mada.
Amini nakwambia ukiolewa na huyo jamaa basi undugu wa urafiki mliokuwa ano na x wako unageuka kuwa uadui mkubwa sana
Hata huyo bwana hatakuwa na amani mbele za x wako kwa kudhani kwamba huenda mkasameheana na kuamua kusaliti
 
Back
Top Bottom