Rafiki tuliyezoeana muda mrefu kapunguza mawasiliano na mimi, ni wiki mwezi tangu nifungue biashara karibu na ofisini kwake je, ndio chanzo?

Uncle bright

JF-Expert Member
Feb 9, 2023
1,040
4,080
Alikuwa ni rafiki ambae ananichangamkia sana haipiti siku bila kunitumia meseji za salamu, alikuwa anapenda tuchat, kukumbushana visa vya shuleni, n.k.

Kiukweli niwe muwazi kiuchumi tumepishana ila hatuchunguzani sana, tunajuana vichache yeye anajua tu kwamba mimi nina biashara kadhaa ambazo hajawai kuniuliza kwa ndani japo analijua duka langu moja na mimi najua tu kwamba shughuli anayofanya anauza vinywaji baridi sehemu flani hivi kaweka kioski haingii gharama za kodi yoyote.

Sasa mwezi iliyopita kuna sehemu karibu na eneo alipo huyo rafiki yangu kuna frem nzuri kuna mtu alikuwa anaiacha, mimi kulingana na biasharra nayoifanya nikaona niongezee tawi hapo maana hio sehemu ina wateja wa bidhaa nazoiuza.

Wakati mafundi wanakianaa chumba nilifika kumtembelea rafiki tukawa tunapiga stori za hapa na pale, rafiki naona alishapiga research kwamba kaniona na mafundi kwenye fremu, wala sikukataa nlilikubali, alianza kuwa interested sana na biashara nayotaka kufanya zaidi kuzidi mazungumzo ya kawaida.

Kuweka stori iwe fupi mimi hapo kwenye frem huwa sishindi ni jioni tu huwa napitia hesabu, biashara si haba nimenunua pikipiki huwa inapiga deluvery za kutosha tu kwa wateja wa maeneo hayo.

Ishu ni kwamba rafiki yangu kwa sasa ni kama kapoa sana, sio kama zamani.

Kwa namna yoyote hii hali inahusiana na chochote milichoorodhesha?
 
Wewe tafuta pesa, mambo ya rafiki yapo bongo tu kwenye nchi ya ujamaa ila ukiingia ulaya na America unakuta phone book ya mzungu Ina namba tatu tuu moja ya mke wake mbili za watoto wake (hawazai watoto zaidi ya wawili)
Comment ipo nje kidogo ya maada ila hao uliowataja ni wazungu na sio kupimo cha benchmark ya kufuata kila lifestyle waliyonayo, kwa tamaduni za Afrika tunaishi kwa vikundi sana hasa kwa hizi extended families,

anyway turejee kwenye maada
 
Mtu ukishamuona hivyo unampotezea unaendelea na mishe zako as long as hujamkosea ni wivu unamsumbua kwanini akuumize kichwa kwani anakulisha au anakuchangia kitu Gani
 
Ni kama umeend au unafanya kushindana na rafiki yako. Labda ulimfanyoa majivuno na pikipiki yako ukamwambia hii ni usafiri binafsi sio bodaboda. .
Ukiishi kufatilia ya walimwengu maisha yako yatakuwa hayana furaha. Huwezi kumfurahisha kila mtu. .
 
Wewe tafuta pesa, mambo ya rafiki yapo bongo tu kwenye nchi ya ujamaa ila ukiingia ulaya na America unakuta phone book ya mzungu Ina namba tatu tuu moja ya mke wake mbili za watoto wake (hawazai watoto zaidi ya wawili)
Dogo unaakili sana

Daaah we ni asset kabisa hii ni point nxuri na waalimu ndo wamejaa kutupa majungu na kujaza ma namba ya ajabu sio
 
Mimi napenda sana watu wa hivyo kajipunguza mwenyewe huyo we kuwa kama yeye tu mpotezee siku akikuona wa maana fresh akikaza fresh pia maisha asaiv magumu ndugu muda wa kuwaza marafiki sjui ndugu unatolea wapi na mtu akuchangii chochote kwenye life yako?
 
Alikuwa ni rafiki ambae ananichangamkia sana haipiti siku bila kunitumia meseji za salamu, alikuwa anapenda tuchat, kukumbushana visa vya shuleni, n.k.

Kiukweli niwe muwazi kiuchumi tumepishana ila hatuchunguzani sana, tunajuana vichache yeye anajua tu kwamba mimi nina biashara kadhaa ambazo hajawai kuniuliza kwa ndani japo analijua duka langu moja na mimi najua tu kwamba shughuli anayofanya anauza vinywaji baridi sehemu flani hivi kaweka kioski haingii gharama za kodi yoyote.

Sasa mwezi iliyopita kuna sehemu karibu na eneo alipo huyo rafiki yangu kuna frem nzuri kuna mtu alikuwa anaiacha, mimi kulingana na biasharra nayoifanya nikaona niongezee tawi hapo maana hio sehemu ina wateja wa bidhaa nazoiuza.

Wakati mafundi wanakianaa chumba nilifika kumtembelea rafiki tukawa tunapiga stori za hapa na pale, rafiki naona alishapiga research kwamba kaniona na mafundi kwenye fremu, wala sikukataa nlilikubali, alianza kuwa interested sana na biashara nayotaka kufanya zaidi kuzidi mazungumzo ya kawaida.

Kuweka stori iwe fupi mimi hapo kwenye frem huwa sishindi ni jioni tu huwa napitia hesabu, biashara si haba nimenunua pikipiki huwa inapiga deluvery za kutosha tu kwa wateja wa maeneo hayo.

Ishu ni kwamba rafiki yangu kwa sasa ni kama kapoa sana, sio kama zamani.

Kwa namna yoyote hii hali inahusiana na chochote milichoorodhesha?
Wabongo bana.Yani usikute unaingiza siyo zaidi ya elfu hamsin kwa siku halafu anakuchukia na kukuonea wivu. Wakati sisi tunamuonea wivu Elon Musk. Aliposhuka tu akawa wa pili kwa utajiri duniani watu tulifurahi na kusheherekea. Mabilionea huwa hatupendani kabisa.
 
Alikuwa ni rafiki ambae ananichangamkia sana haipiti siku bila kunitumia meseji za salamu, alikuwa anapenda tuchat, kukumbushana visa vya shuleni, n.k.

Kiukweli niwe muwazi kiuchumi tumepishana ila hatuchunguzani sana, tunajuana vichache yeye anajua tu kwamba mimi nina biashara kadhaa ambazo hajawai kuniuliza kwa ndani japo analijua duka langu moja na mimi najua tu kwamba shughuli anayofanya anauza vinywaji baridi sehemu flani hivi kaweka kioski haingii gharama za kodi yoyote.

Sasa mwezi iliyopita kuna sehemu karibu na eneo alipo huyo rafiki yangu kuna frem nzuri kuna mtu alikuwa anaiacha, mimi kulingana na biasharra nayoifanya nikaona niongezee tawi hapo maana hio sehemu ina wateja wa bidhaa nazoiuza.

Wakati mafundi wanakianaa chumba nilifika kumtembelea rafiki tukawa tunapiga stori za hapa na pale, rafiki naona alishapiga research kwamba kaniona na mafundi kwenye fremu, wala sikukataa nlilikubali, alianza kuwa interested sana na biashara nayotaka kufanya zaidi kuzidi mazungumzo ya kawaida.

Kuweka stori iwe fupi mimi hapo kwenye frem huwa sishindi ni jioni tu huwa napitia hesabu, biashara si haba nimenunua pikipiki huwa inapiga deluvery za kutosha tu kwa wateja wa maeneo hayo.

Ishu ni kwamba rafiki yangu kwa sasa ni kama kapoa sana, sio kama zamani.

Kwa namna yoyote hii hali inahusiana na chochote milichoorodhesha?
Pengine kwa kuwa mko karibu karibu, mnaonana kila siku, mawasiliano ya simu ya nini tena? Au unajishtukia? Wewe unamtumia salamu?
 
Hajakutukana, hajakusema vibaya, wala hujui nini kinamsibu, huenda anatafakari afanyaje na yeye awe kama wewe au pengine biashara yake inayumba. Kuliko kupeleka Mawazo kwamba anayawazia mafanikio yako, mpigie au text kumjulia hali na mpe ideas za kuongeza biashara kujitanua.
 
Comment ipo nje kidogo ya maada ila hao uliowataja ni wazungu na sio kupimo cha benchmark ya kufuata kila lifestyle waliyonayo, kwa tamaduni za Afrika tunaishi kwa vikundi sana hasa kwa hizi extended families,

anyway turejee kwenye maada
Unaonekana unapenda Sana ujamaa 😅sasa Kama ndivyo ulivyo si umuulize kisa Cha kuwa hivyo,wewe uliye karibu naye na unamfahamu kuliko hata sisi tulio mbali nanyi 🤔usijistukie bloo,kama unajihisi vibaya kisa kufungua goli jipya jirani yake,basi lifunge ili rafiki yako afurahi,uendelee kuwa mjamaa na mtu mwema kwake 😅 😅
 
Mtu kusoma naye haimaanishi ni rafiki yako. Tena zaidi inamaanisha ni mshindani wako. Haijalishi mlisoma wote level gani. Fikiria wote mmesoma labda chuo kozi fulani, huo ni rafiki yako au mshindani wako kwenye soko la ajira? Au mmemaliza wote form four. Wakataka mfanyakazi wa form four au kwenda kozi VETA, huyo unayesema rafiki ni mshindani wako. Achana na habari za marafiki dunia ya leo. Kwanza mnaongea vitu gani vya maana kama siyo kusimanga classmates wenu na waalimu wenu wa zamani!?
 
Back
Top Bottom