Biashara ikianza kuwa ngumu unaanza kujikosoa, "hivi ni mimi niliesema ajira ya kupokea mshahara kila mwezi na posho za kila wiki ni utumwa ?"

Uncle bright

JF-Expert Member
Feb 9, 2023
1,040
4,080
Nashudia live haya mambo nipo kwenye taasisi ambayo wafanyabiashara inabidi watoe maelezo yenye ushahidi wa hali zao kibiashara ili tuweze kuwasaidia kama wadhamini wa shida wanazopitia,

itoshe kusema wafanyabiashara waliofanikiwa ni wachache, usikurupuke kutamani biashara kwa kuwaangalia hawa wachache ukadhani wengi wana hali hizo, utavamia mtumbwi wa vibwengo !!

kiuhlisia wafanya biashara wengi sana wanapitia magumu kwa stress za marejesho ya mikopo, wateja wachache, ushindani kuharibu faida, kushinda ofisini kila siku asubuhi hadi usiku, kushindwa kulipia frem, kufirisika, n.k,

ni tofauti na waajiriwa wengi hasa wa serikalini, hawafikii mafanikio ya wafanyabiashara wachache matajiri lakini angalau wana uhakika wa kipato.

Unaanza kujiuliza, "hivi ni mimi niliesema ajira ya kupokea mshahara kila mwezi na posho za kila wiki ni utumwa ?"
 
Hii nchi acha ijae nyumba za ibada na manabii wa uongo ili yapoze vichwa vya wanachi kwa kuwapromise kuwa kuna maisha mengine wakifa.
Mfanyakazi serikalini anaenda kumbana mfanyabiashara huku hajui huyo mfanyabiashara ndie anamlipa mshahara kupitia kodi anazotozwa kwenye biashara.
 
Nilifanikiwa kufanya biashara miaka 6 then nikanyoosha mikono nikaingia kwenye upande wa ajira.

Namshukuru Mungu nilichokivuna kwenye biashara nisingekipata kwenye ajira miaka 6. Sasa hivi nataka nijipange nifungue tena biashara kuongeza kipato cha ziada.
mhn! nina kama siku nne nimefunga frame rasmi baada ya biashara kuisimamisha kwa zaidi ya mwaka baada ya mfanyakazi kunichanganya.
 
Tofautisha haya makundi; wafanyabiashara/wachuuzi (kununua na kuuza) vs Wajasiriamali (tengeneza na kuuza); wajasiriamali lengo la mauzo au kupata pesa huwa ni la pili, ila lengo lao la kwanza ni kutaka wajulikane kwa kufanya vitu vingine ambavyo wengine wameshindwa n.k​
 
Maelf ya fremu zinarudishwa kwa wenye nazo, na maelf za start up business wanazichukua ili nao waunge mkono kuzirudisha baada ya kodi ya miezi 12.

Ila upepo wa biashara ni mbaya....mbaya.....mbaya....mbaya sana
Fremu asiee singekuwa Bei nafuu angalau nawahurumia watu Wana lipia milion 18 kwa mwaka kwa fremu tu bila tra jiji

Ni stress tupu kwa kweli nawaonea huruma wakuu
 
Maelf ya fremu zinarudishwa kwa wenye nazo, na maelf za start up business wanazichukua ili nao waunge mkono kuzirudisha baada ya kodi ya miezi 12.

Ila upepo wa biashara ni mbaya....mbaya.....mbaya....mbaya sana
Haya sema sasa! Si mlimsimanga JPM? Sasa hivi mtaani hela hamna na hakuna miradi ya kiuchumi mipya inajengwa angalau kuwa na kisingizio! Mama anaupiga mwingi!
 
Haya sema sasa! Si mlimsimanga JPM? Sasa hivi mtaani hela hamna na hakuna miradi ya kiuchumi mipya inajengwa angalau kuwa na kisingizio! Mama anaupiga mwingi!
Miradi aliyoanzisha Kuna hata mmoja ushakamilika au kuzalisha so yote bado inahitaji fedha...Mungu mkubwa la mnusuru Ana aibu kubwa marehemu angeaibika so ajabu angejingonga Kama sio kutunyonga ...system failure...
 
Haya sema sasa! Si mlimsimanga JPM? Sasa hivi mtaani hela hamna na hakuna miradi ya kiuchumi mipya inajengwa angalau kuwa na kisingizio! Mama anaupiga mwingi!
Sijawah ponda lile jiwe, kwanza alikuwa role model wangu, anaamua kitu kigumu sana ila mwisho wa siku unaona matokeo hadi una shangaa. Na wakat wake ndipo biashara zangu zilienda vizuri sana,
 
Miradi aliyoanzisha Kuna hata mmoja ushakamilika au kuzalisha so yote bado inahitaji fedha...Mungu mkubwa la mnusuru Ana aibu kubwa marehemu angeaibika so ajabu angejingonga Kama sio kutunyonga ...system failure...
Stand ya magufuli mbona aliikamilisha, au uliikamilisha wewe? Barabara za juu Tazara na Ubungo nazo ulizikamilisha wewe?
 
Back
Top Bottom