Rafiki angu ananiroga

Rafiki angu ananiroga

Mkuu..

Ushirikina Upo..
Hilo mi sina Doubt nalo..

Ila tunatofautiana tu njia ya kukabiliana nao.. kwa sababu za kiimani

Wengine Humtumia Mwenyezi Mungu
Wengine Humtumia
Miungu yao

Wewe umechagua kutumia Nguvu za giza
Basi nakushauri kulingana na uchaguzi wako..

Pambana na tatizo lako bila kurudirudi nyuma
Ukianzisha vita hakikisha unaimaliza
Maana hapo umeshachokoza tayari mapambano dhidi ya rafiki yako
Hata yeye pia ameshatambua kuwa mpo katika vita..
PAMBANA SANA..
 
Binafsi sikuwa nawajua waganga,
Yeye jamaa ndio alinipeleka. Na mbaya zaidi alikuwa akinipeleka kwa waganga kumbe feki wanapanga mambo yao naenda naliwa hela. Imagine unaenda kwa mganga anataja mpaka ofisi unayofanyia kazi he huoni kama ni mchezo. Na cha ajabu jamaa ni MTU wa waganga sana sasa inafika kipindi ananifanyia vitu badae anakuja anaropoka vyote.
Alaaa...kumbe!
 
Mkuu..

Ushirikina Upo..
Hilo mi sina Doubt nalo..

Ila tunatofautiana tu njia ya kukabiliana nao.. kwa sababu za kiimani

Wengine Humtumia Mwenyezi Mungu
Wengine Humtumia
Miungu yao

Wewe umechagua kutumia Nguvu za giza
Basi nakushauri kulingana na uchaguzi wako..

Pambana na tatizo lako bila kurudirudi nyuma
Ukianzisha vita hakikisha unaimaliza
Maana hapo umeshachokoza tayari mapambano dhidi ya rafiki yako
Hata yeye pia ameshatambua kuwa mpo katika vita..
PAMBANA SANA..
Poa mkuu niombee nishinde vita hii
 
Usimwambie chochote kwa sababu huna uthibitisho ila mkwepe kaa naye mbali mtu mbaya hawezi kutoka mbali ni uyo uyo rafiki yako.
Inaonyesha umelelewa katika mazingira ya ushirikina na uchawi, hutakaa umwanini yeyote
 
Nashukuru kwa ushauri, sitaki tena waganga. Kampani yake nayo siitaki.

Anapiga sim sana mpaka missed call 12. Sipokei wala SMS simjibu.
Anabadilisha mpaka namba nimeshtuka sipokei namba ngeni.

Amezoea ukitonga wake anakufa njaa sasa. Jamaa nilikuwa namsaidia sana, hela ya kula nilikuwa nampa, funguo ya gari nampa. Kuna siku nilimlipia mpaka guest house akaenda kupumzika na rafiki ake.

Sasa anaisoma namba
huna lolote tak***o we, unaleta sifa hapa kua ulikua unampa Gari mara ooh kula kwako,mara mumlipia gest, huu upuuzi tu hapa, mbona kipindi cha KUMSAIDIA hukumuanika, me binafsi naona wewe ndie mchawi mwenyewe wa maisha yako.tuondolee harufu ya uvungu hapa
 
Ni mwezi wa tatu sasa, siko poa na matatizo mengi yananiandama. Nimeenda kwa babu kuangalia akanipa full image. Best angu ndo ananimaliza. Jamaa tumejuana yapata mwaka sasa. Nimempeleka mpaka kwa bimkubwa, home kwangu anakuja all the time. Misosi tunakula pamoja, job kwangu anakuja mpaka staff wenzangu wanamjua.

Gari langu namwachia siku nzima, nikiwa kazini funguo nampa. Hela ndogo ndogo nampa. Kumbe jamaa anannipiga misumari.

Babu kanishauri nimpe makavu live. Mimi naogopa atanidhuru zaidi ya hapa. Je nifanyeje??
Wife nimemwambia kashalianzisha bifu hawaongei.

Na katika kutafuta ukweli jamaa ameanza kujishtukia. Maana Sikh hizi simpi gari, akipiga sim sipokei, akituma SMS sijibu. Jana katuma SMS anasema" Mbona hupokei sim unanikwepa, au tuna ugomvi?"

Ushauri wadau
Natamani nikutukane ila basi tu. Kiufupi kwa waganga utamaliza hela, waongo wa hovyo hao
 
Ila waganga huwa ni waongo mnoo na ni wataalam wa kusoma saikolojia ya mtu, epukana na huyo rafiki yako na uache tabia ya kwenda kwa waganga, muamini Mungu kwa kila kitu.
 
Kwa akili hizi Tanzania tuna safari ndefu ya kusonga katika nchi ya kusadikia ya viwanda.

Kapimwe akili mkuu huenda una matatizo ya kisaikolojia.
😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀
 
Na wewe ni mshirikina kwa babu image ulipataje?

Anyway uwe unatembea na jani la bangi mfukoni&ule kitimoto sana uchawi haukugusi.
 
Madam, duniani tunahangaika huku na huko nikajikuta naenda kwa babu. Asante kwa ushauri wako naufanyia kazi
 
...teh hee hee..uzi umejaa wasioamini uchawi wakati wamesoma kichwa cha habari kinahusu nini..,badala ya kupuuza wasome vingine,wakafungua.,wakasoma hadi kucomment..
..kweli maisha bila unafiki hayaendi!
 
Back
Top Bottom