Rada ya Tanzania kimeo tena

Rada ya Tanzania kimeo tena

Rada inayotumika kuongozea ndege kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNIA) imeharibika tena kufuatia kifaa cha mfumo wa kusambazia umeme kupata hitilafu........ JAMANI HUVI ILE CHANGE ILIISHA RUDISHWA........?
 
watanzania walisha sahau mambo ya rada,epa,richmond na mabilion kule uswiss sasa hivi tunashughulika na wabaya wetu wakristo/waislam
 
Rada ya Tanzania inayotumika kuongozea ndege imaharibika tena na safari hii ni kifaa kinachohitaji milioni 40 ili itengamae.

Miezi kama miwili iliyopita rada hii iliharibika na kugharimu mamilioni ya fedha

Rada hii ni mtumba ambayo serikali ya Ben Mkapa iliamua kuinunua katika mzaingira yaliyojaa harufu ya rushwa.

Soma hapa chini;

19th October 2012

Rada inayotumika kuongozea ndege kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNIA) imeharibika tena kufuatia kifaa cha mfumo wa kusambazia umeme kupata hitilafu.

Chanzo chetu cha habari kinasema kuwa kifaa hicho kiliaharibika Ijumaa iliyopita na tangu siku hiyo hadi jana mafundi kutoka Kenya walikuwa wanahangaika kukitengeneza.

Habari zaidi zinaeleza kuwa kifaa hicho kilichopo ndani ya UPS (Uninterrupted Power Supply) ambacho kinatumika kusambazia umeme, kina thamani ya Sh. milioni 40.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, ikiwa kitashindikana kutengenezwa, serikali italazimika kununua UPS nyingine mpya na gharama yake itakuwa kubwa zaidi.

Mamlaka ya Usafirishaji wa Anga (TCAA) imetithibitishia NIPASHE kuharibika kwa kifaa hicho.

Mkurugenzi Mkuu wa Anga TCAA, Fadhili Manongi, alisema ndani ya rada kuna kifaa kinachotumika kusambazia umeme ambacho kiliharibika tangu Oktoba 12, mwaka huu na kuna mafundi kutoka Kenya ambao wameitwa kuja kukifanyia matengenezo na kwamba kwa sasa wanaendelea na kazi.

“Ni kweli kuna tatizo dogo limetokea kwenye rada usiku wa kuamkia Jumamosi ya wiki iliyopita, lakini kuna mafundi kutoka Kenya wanalifanyia kazi,” alisema Manongi alipozungumza na NIPASHE kwa njia ya simu jana.

Manongi alisema kuwa leo mtaalamu kutoka Afrika Kusini atawasili nchini kwa ajili ya kuongeza nguvu ya matengenezo pamoja na uchunguzi zaidi wa UPS kujua sababu inayosababisha kuungua mara kwa mara.

“Rada kama rada ni nzima, ila kuna tatizo dogo limetokea ndani ya rada, lakini muda si mrefu tatizo hilo litamalizika kwa kuwa wataalamu wanalishughulikia,” alisema Manongi.

Taarifa za ndani zaidi ambazo NIPASHE imezipata zinaeleza kuwa UPS hiyo au “Power Suply” iliungua zaidi ya wiki moja iliyopita na tatizo ndani ya rada hiyo lilianza kuonekana tangu siku walipoifanyia ukarabati (Agosti 18, mwaka huu) kwa kuanza kuonyesha taa nyekundu ikiashiria kuna hitilafu ndani ya chombo hicho.

“Unajua hata ile mara ya kwanza walipofanya matenegenezo baada ya kuungua, ilipofungwa tu alarm ilianza kulia. Hii ilionyesha wazi haitadumu,” kilisema chanzo chetu ndani ya TCAA na kuongeza:

“Kinachofanyika ni kama mota yako imeungua halafu unaishuka tena, sijui kama itakuwa na nguvu ile. Sana sana itakusukuma siku mbili tatu na tatizo litarudi pale pale.

“Tukubali tu ukweli kwamba hili lidubwasha limechoka, muda wake wa matumizi umekwisha, sasa kama hawataki kutambua ukweli na kudhani labda ni hujuma na kusaka mchawi, mambo haya yatakuwa hivi tu”.

Mmoja wa marubani kutoka Shirika la Ndege la Coast (jina limehifadhiwa), aliliambia NIPASHE kuwa ni muda wa wiki moja sasa hapewi “Code” pindi anapotaka kutua na ndege, jambo linalomlazimisha kutumia uzoefu wake.

Alisema, marubani wengi wanalalamika kwa kukosa mawasiliano pindi wanapotaka kutua na kuwa wameambiwa kuwa kuna matengenezo yanafanyika katika rada.

Kifaa hicho kiliharibika Agosti mwaka huu na kupelekwa Afrika Kusini na kutengenezwa kwa gharama ya Sh. milioni 40.

Rada hiyo ilinunuliwa kwa Dola za Marekeni milioni 40 na Serikali ya Tanzania kutoka Kampuni ya vifaa vya kijeshi ya BAE Systems ya Uingereza na ilileta mzozo mkubwa nchini kutokana na kununuliwa kwa bei kubwa kuliko thamani yake.

Ununuzi wa rada hiyo ulizua mjadala mkali nchini huku makundi mbalimbali ya jamii yakitaka waliohusika na ununuzi huo wachukuliwe hatua.

Kabla ya ununuzi wa rada hiyo, aliyekuwa Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza, Clare Short, alipinga ununuzi huo na kuitaka serikali ya Tanzania kusitisha mpango huo kwa kuwa ungigharimu sana kama nchi maskini lakini bei hiyo hakuwa ni thamani yake halisi, alihisi kuwa kulikuwa na rushwa inatembea kutekeleza mpango huo.

Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati wa ununuzi wa rada hiyo, Andrew Chenge, ni mmoja wa watu waliotajwa kuhusika katika kufanikisha ununuzi wa rada hiyo kwa bei ya juu.

Chenge alikutwa na Dola za Marekani milioni moja (Sh. bilioni 1.2) katika kisiwani cha New Jersey nchini Uingereza.

Taasisi ya Makosa Makubwa ya Jinai (SFO) ya Uingereza, ilikuwa ikichunguza kama fedha hizo zilikuwa na uhusiano na dili hilo. Chenge alikwisha kunanusha mara kadhaa fedha hizo kuwa na uhusiano na rada, akisema ni akiba yake na familia aliyoipata kwa kazi zake za uawakili.

Baada ya SFO kuendesha uchunguzi kwa muda mrefu kama uuuzaji wa rada hiyo ulikuwa umegubikwa na rushwa, BAE waliamua kukubalia yaishe kwa kukiri kosa la kusindwa kuweka hesabu zake sawa kwa kuwa kiasi cha Dola milioni 12 zilikuwa zimetolewa kama kamisheni kwa waliofanikisha mpango huo, hivyo kulipa fidia Tanzania ya Sh bilioni 72, sawa na bei ya rada.

CHANZO: NIPASHE

Kwa mtindo huu hata Joy atatupiga tu maana habari nyeti kama hizi kwa wenzetu ni siri kwa ajili ya usalama wa nchi husika, hata kwa wenzetu huwa hivi vitu vinaharibika ila hawana madomo kaya kama huku kwetu, sasa tukilianzisha na Joy tu inteligencia yake haita kuwa na tabu, ni kuingia tu JF habari zote wanapata, bureee!
 
UPS ndio unaita mafundi toka kenya na africa kusini ili kuonyesha kuwa hiyo UPS ni kitu sensitive ( muhimu ) sana kumbe ni kitu ambacho hata mimi naweza kukitengeneza bila wasiwasi, huo ndo utumiaji mbaya wa hela zetu
 
Back
Top Bottom