Rada ya Tanzania kimeo tena | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rada ya Tanzania kimeo tena

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mdutch, Oct 19, 2012.

 1. Mdutch

  Mdutch JF-Expert Member

  #1
  Oct 19, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 214
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Rada ya Tanzania inayotumika kuongozea ndege imaharibika tena na safari hii ni kifaa kinachohitaji milioni 40 ili itengamae.

  Miezi kama miwili iliyopita rada hii iliharibika na kugharimu mamilioni ya fedha

  Rada hii ni mtumba ambayo serikali ya Ben Mkapa iliamua kuinunua katika mzaingira yaliyojaa harufu ya rushwa.

  Soma hapa chini;


  19th October 2012

  Rada inayotumika kuongozea ndege kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNIA) imeharibika tena kufuatia kifaa cha mfumo wa kusambazia umeme kupata hitilafu.

  Chanzo chetu cha habari kinasema kuwa kifaa hicho kiliaharibika Ijumaa iliyopita na tangu siku hiyo hadi jana mafundi kutoka Kenya walikuwa wanahangaika kukitengeneza.

  Habari zaidi zinaeleza kuwa kifaa hicho kilichopo ndani ya UPS (Uninterrupted Power Supply) ambacho kinatumika kusambazia umeme, kina thamani ya Sh. milioni 40.

  Kwa mujibu wa chanzo hicho, ikiwa kitashindikana kutengenezwa, serikali italazimika kununua UPS nyingine mpya na gharama yake itakuwa kubwa zaidi.

  Mamlaka ya Usafirishaji wa Anga (TCAA) imetithibitishia NIPASHE kuharibika kwa kifaa hicho.

  Mkurugenzi Mkuu wa Anga TCAA, Fadhili Manongi, alisema ndani ya rada kuna kifaa kinachotumika kusambazia umeme ambacho kiliharibika tangu Oktoba 12, mwaka huu na kuna mafundi kutoka Kenya ambao wameitwa kuja kukifanyia matengenezo na kwamba kwa sasa wanaendelea na kazi.

  “Ni kweli kuna tatizo dogo limetokea kwenye rada usiku wa kuamkia Jumamosi ya wiki iliyopita, lakini kuna mafundi kutoka Kenya wanalifanyia kazi,” alisema Manongi alipozungumza na NIPASHE kwa njia ya simu jana.

  Manongi alisema kuwa leo mtaalamu kutoka Afrika Kusini atawasili nchini kwa ajili ya kuongeza nguvu ya matengenezo pamoja na uchunguzi zaidi wa UPS kujua sababu inayosababisha kuungua mara kwa mara.

  “Rada kama rada ni nzima, ila kuna tatizo dogo limetokea ndani ya rada, lakini muda si mrefu tatizo hilo litamalizika kwa kuwa wataalamu wanalishughulikia,” alisema Manongi.

  Taarifa za ndani zaidi ambazo NIPASHE imezipata zinaeleza kuwa UPS hiyo au “Power Suply” iliungua zaidi ya wiki moja iliyopita na tatizo ndani ya rada hiyo lilianza kuonekana tangu siku walipoifanyia ukarabati (Agosti 18, mwaka huu) kwa kuanza kuonyesha taa nyekundu ikiashiria kuna hitilafu ndani ya chombo hicho.

  “Unajua hata ile mara ya kwanza walipofanya matenegenezo baada ya kuungua, ilipofungwa tu alarm ilianza kulia. Hii ilionyesha wazi haitadumu,” kilisema chanzo chetu ndani ya TCAA na kuongeza:

  “Kinachofanyika ni kama mota yako imeungua halafu unaishuka tena, sijui kama itakuwa na nguvu ile. Sana sana itakusukuma siku mbili tatu na tatizo litarudi pale pale.

  “Tukubali tu ukweli kwamba hili lidubwasha limechoka, muda wake wa matumizi umekwisha, sasa kama hawataki kutambua ukweli na kudhani labda ni hujuma na kusaka mchawi, mambo haya yatakuwa hivi tu”.

  Mmoja wa marubani kutoka Shirika la Ndege la Coast (jina limehifadhiwa), aliliambia NIPASHE kuwa ni muda wa wiki moja sasa hapewi “Code” pindi anapotaka kutua na ndege, jambo linalomlazimisha kutumia uzoefu wake.

  Alisema, marubani wengi wanalalamika kwa kukosa mawasiliano pindi wanapotaka kutua na kuwa wameambiwa kuwa kuna matengenezo yanafanyika katika rada.

  Kifaa hicho kiliharibika Agosti mwaka huu na kupelekwa Afrika Kusini na kutengenezwa kwa gharama ya Sh. milioni 40.

  Rada hiyo ilinunuliwa kwa Dola za Marekeni milioni 40 na Serikali ya Tanzania kutoka Kampuni ya vifaa vya kijeshi ya BAE Systems ya Uingereza na ilileta mzozo mkubwa nchini kutokana na kununuliwa kwa bei kubwa kuliko thamani yake.

  Ununuzi wa rada hiyo ulizua mjadala mkali nchini huku makundi mbalimbali ya jamii yakitaka waliohusika na ununuzi huo wachukuliwe hatua.

  Kabla ya ununuzi wa rada hiyo, aliyekuwa Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza, Clare Short, alipinga ununuzi huo na kuitaka serikali ya Tanzania kusitisha mpango huo kwa kuwa ungigharimu sana kama nchi maskini lakini bei hiyo hakuwa ni thamani yake halisi, alihisi kuwa kulikuwa na rushwa inatembea kutekeleza mpango huo.

  Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati wa ununuzi wa rada hiyo, Andrew Chenge, ni mmoja wa watu waliotajwa kuhusika katika kufanikisha ununuzi wa rada hiyo kwa bei ya juu.

  Chenge alikutwa na Dola za Marekani milioni moja (Sh. bilioni 1.2) katika kisiwani cha New Jersey nchini Uingereza.

  Taasisi ya Makosa Makubwa ya Jinai (SFO) ya Uingereza, ilikuwa ikichunguza kama fedha hizo zilikuwa na uhusiano na dili hilo. Chenge alikwisha kunanusha mara kadhaa fedha hizo kuwa na uhusiano na rada, akisema ni akiba yake na familia aliyoipata kwa kazi zake za uawakili.

  Baada ya SFO kuendesha uchunguzi kwa muda mrefu kama uuuzaji wa rada hiyo ulikuwa umegubikwa na rushwa, BAE waliamua kukubalia yaishe kwa kukiri kosa la kusindwa kuweka hesabu zake sawa kwa kuwa kiasi cha Dola milioni 12 zilikuwa zimetolewa kama kamisheni kwa waliofanikisha mpango huo, hivyo kulipa fidia Tanzania ya Sh bilioni 72, sawa na bei ya rada.


  CHANZO: NIPASHE   
 2. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #2
  Oct 19, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,798
  Likes Received: 36,830
  Trophy Points: 280
  Hii nchi imekua jalala sasa.

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 3. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #3
  Oct 19, 2012
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,642
  Likes Received: 2,877
  Trophy Points: 280
  Watupeleke training tuwe tunatengeneza wenyewe
   
 4. Mdutch

  Mdutch JF-Expert Member

  #4
  Oct 19, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 214
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  The effects of dark markets!
   
 5. i

  iseesa JF-Expert Member

  #5
  Oct 19, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 944
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sijui mzee wa VIJISENTI anasemaje anapoona haya yakitokea?
   
 6. mwaxxxx

  mwaxxxx JF-Expert Member

  #6
  Oct 19, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 846
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  akatwe kwenye marupurupu yake huyo Ben
   
 7. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #7
  Oct 19, 2012
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Anaendelea kutumbua. Hawasutwagi na dhamira hawa!
   
 8. Chizi Fureshi

  Chizi Fureshi JF-Expert Member

  #8
  Oct 19, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 1,710
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Tengenezeni haraka, kazi na malawi haiko mbali.
   
 9. O

  Oremus Member

  #9
  Oct 19, 2012
  Joined: Oct 17, 2012
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nitarudi...........
   
 10. c

  chitanda.nyoka Senior Member

  #10
  Oct 19, 2012
  Joined: May 3, 2012
  Messages: 195
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hii rada ingenunuliwa kipindi cha jk mbona angekoma sema kwa kua amenunua ben kimya lakini ajabu pia bado analaumiwa kikwete kwanini hawakamati walonunua.
   
 11. Bavaria

  Bavaria JF-Expert Member

  #11
  Oct 19, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 44,100
  Likes Received: 11,251
  Trophy Points: 280
  nchi imekua dampo. Bidhaa feki na mbovu zimejazana.
   
 12. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #12
  Oct 19, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  usanii mwingine tena.
   
 13. Mkuu rombo

  Mkuu rombo JF-Expert Member

  #13
  Oct 19, 2012
  Joined: Oct 18, 2012
  Messages: 1,559
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Aiseee babaangu kwanini isipelekwe india kwa matibabu zaidi
   
 14. HUNIJUI

  HUNIJUI JF-Expert Member

  #14
  Oct 19, 2012
  Joined: Oct 10, 2012
  Messages: 1,441
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  kazi ipo
   
 15. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #15
  Oct 19, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Khaaa! Natamani tupate uongozi utakaowakata vichwa wote waliohusika na madudu yote ya aina hii! Halafu kumbe hata mafundi ni wa kutoka kenya!!! Yaani hatuna mafundi, vipi kule kwenye chama la kina shimbo au hawaruhusiwi kugusa dude la kiraia nini.
   
 16. Mandingo

  Mandingo JF-Expert Member

  #16
  Oct 19, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 3,380
  Likes Received: 318
  Trophy Points: 180
  Mama Banda kweli acha awe na kiburi tu!kwa style hii dhaifu lazima achezee kichapo vita ikija!
   
 17. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #17
  Oct 19, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Umenikumbusha, hivi ile chenji ya rada iko wapi jamani, si tuliambiwa wananunua madawati sijui vitabu? Yako wapi sasa hadi kifaa chenyewe chali!!!!!
   
 18. k

  kasimba123 JF-Expert Member

  #18
  Oct 19, 2012
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 1,318
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160
  power = IVcos(theta) hii cos(theta) ni power factor na inatakiwa iwe inakaribia moja. usambazaji wa umeme tanzania hawatilii mkazo sana kuifanya hi power factor kuwa stable na ndio maana vitu vinaungua ovyo. kama hakutakua na uimarishaji mfumo wa usambazaji umeme na kuifanya pf kuwa stable tutakuwa tunacheza tu
   
 19. J

  Jikombe Senior Member

  #19
  Oct 19, 2012
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 198
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Mbona maandiko yako yakibaguzi na kichochezi sana? Watu wenye mitizamo kama yako ndo waliochochea vurungu kule mbagala (kuchoma makanisa,), vurugu za leo k,koo dar.
  Ndugu yangu mtu utuhumiwa kwa matendo yake na si kingine
   
 20. StayReal

  StayReal JF-Expert Member

  #20
  Oct 19, 2012
  Joined: Sep 29, 2012
  Messages: 519
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hili nalo jambo...i support you mkuu
   
Loading...