Rada siri yafichuka - wahusika wakubwa waanikwa

Candid Scope
Nothing New Here... Tunajua hawa watu kwa Miaka hakuna jipya hapa... NAONA TU WACHOVU

SASA...
 
Last edited by a moderator:
Sasa siri ipi iliyofichuka na hayo yote yanajulikana!

Huwa mnakosa yakuandika, hayo yamejaa humu JF miaka kadhaa sasa.
 
Technically mafisadi wa radar wamepata msamaha wa Rais/presidential pardon,
 
Inashangaza sana viongozi hawa wa CCM kuwa na ujasiri wa kitoto na kuwahadaa watanzania kiasi hiki jamani. Wamelala usingizi wa pono hata hawaelewi kuwa watanzania wa leo siyo wale wa upashanaji habari kupitia redio moja tu. Mawasiliano yamebadilika sana na watu hata kama hawakupewa fursa ya kuingia darasani wana akili za kupambanua mambo. "Unaweza kudanganya watu kwa muda fulani tu na siyo muda wote" wajue hilo.
icon8.png
 
Sasa siri ipi iliyofichuka na hayo yote yanajulikana!

Huwa mnakosa yakuandika, hayo yamejaa humu JF miaka kadhaa sasa.
Unataka yaandikwe ya dr slaa ya kimbeya ambayo hayana vielelezo ndio utaona hatujakosa vya kuandika? nenda kajishindilie mpaka muda wa uji na tambi jioni ni mbali
 
Candid Scope
kuwa na adabu na heshima wewe ,mkuu wako wa nchi ashasema hakuna wakumshtaki asa unataka nini tena..hizi ndio habari za uchochezi zinazokatazwa kila siku humu nchini.viongozi wamemaliza we kaa kimyaaaa au kama unaushaidi kama alivyosema mh waziri basi upeleke wakawafungulie kesi....
 
Last edited by a moderator:
ccm ina wenyewe cha muhimu Nape awataje yeye si jabali na amevaa uzalendo? Vua gamba vua gwanda Vaa uzalendo ndyo muda wa kuonyesha uzalendo huu. Jaman mkama na nape wamefungiwa zizin nn hawasikiki tena. Kikwete ni chaguo la Mungu tutasikia mengi kipindi hki.
 
Nakumbuka wiki iliyopita mada ya Mzee Mwanakijiji Ambayo aliongelea mazingaombwe kitu ambacho kwa maneno mengine kimezoeleka kutamkwa viini macho jinzi vinavyoendelea kutendeka ndani ya serikali yetu, hii ni sawa na sikio la kufa kutosikia dawa hata wahisani wanapotusaidia kufunua chombo chenye kutoa harufu ili kutoa uvundo na uchafu kisiendelee kuoza zaidi, lakini cha kushangaza viongozi wa ngazi za juu wenye kushikilia mhimili mkuu wa kuongoza nchi wakikingia kifua kwa nguvu zote bila kutoa hata mwanya wa kuruhusu vyombo vya sheria kuchukua hatua.
Unapoongelea mkataba huu wa Rada ni moja kwa moja unamhusisha aliyekuwa Waziri wa Mambo ya nje wakati huo.Ni kuanzia hapo ndipo utajua ni kwa nini mamlaka za juu Serikalini hawapendi hili jamabo lifikishwe Mahakamani.
 
Sasa siri ipi iliyofichuka na hayo yote yanajulikana!

Huwa mnakosa yakuandika, hayo yamejaa humu JF miaka kadhaa sasa.

Wewe uko upande upi? ni kweli unakubali kulikuwa na rushwa? au unaungana na mwenyekiti wako ?
 
Nakumbuka wiki iliyopita mada ya Mzee Mwanakijiji Ambayo aliongelea mazingaombwe kitu ambacho kwa maneno mengine kimezoeleka kutamkwa viini macho jinzi vinavyoendelea kutendeka ndani ya serikali yetu, hii ni sawa na sikio la kufa kutosikia dawa hata wahisani wanapotusaidia kufunua chombo chenye kutoa harufu ili kutoa uvundo na uchafu kisiendelee kuoza zaidi, lakini cha kushangaza viongozi wa ngazi za juu wenye kushikilia mhimili mkuu wa kuongoza nchi wakikingia kifua kwa nguvu zote bila kutoa hata mwanya wa kuruhusu vyombo vya sheria kuchukua hatua.

halafu tunashangaa kwanini migomo haiishi!
 
Inanikumbusha Mada moja ya Wapo Radio....Kipindi jambo lenye mashakamashaka tulijadili....kwa siku ya 8/8/2012.....swali la mada jee Watanzania tumelogwa? Mimi nasema bado wanaendelea kuroga mpaka sasa...watanzania wanarogwa!!! hahahahahaha...very funny
 
Unataka yaandikwe ya dr slaa ya kimbeya ambayo hayana vielelezo ndio utaona hatujakosa vya kuandika? nenda kajishindilie mpaka muda wa uji na tambi jioni ni mbali

Dokata Slaa ana nini katika Taifa hili zaidi ya kuwaingiza mjini wachagga!
 
Candid Scope
kuwa na adabu na heshima wewe ,mkuu wako wa nchi ashasema hakuna wakumshtaki asa unataka nini tena..hizi ndio habari za uchochezi zinazokatazwa kila siku humu nchini.viongozi wamemaliza we kaa kimyaaaa au kama unaushaidi kama alivyosema mh waziri basi upeleke wakawafungulie kesi....

Ushahidi ndio huu ulioanikwa hapo gazetini, unataka ushahidi gani zaidi ya huo ambao unataja njia zilizofikisha rushwa kufichwa kwenye mabenk huko UK na majina yako hadharani, kama ni kuonewa watuhumiwa wangeshtaki waliowaanika hadharani.
 
Unapoongelea mkataba huu wa Rada ni moja kwa moja unamhusisha aliyekuwa Waziri wa Mambo ya nje wakati huo.Ni kuanzia hapo ndipo utajua ni kwa nini mamlaka za juu Serikalini hawapendi hili jamabo lifikishwe Mahakamani.

Umetoboa siri zaidi, kwani hayo yasingetendeka bila yeye kuhusika moja kwa moja kutokana na wadhifa aliokuwa nao wakati huo, hivyo tusishangai Mkuu mwenyewe kuwa golikipa kukinga goli lisifungwe.
 
Inanikumbusha Mada moja ya Wapo Radio....Kipindi jambo lenye mashakamashaka tulijadili....kwa siku ya 8/8/2012.....swali la mada jee Watanzania tumelogwa? Mimi nasema bado wanaendelea kuroga mpaka sasa...watanzania wanarogwa!!! hahahahahaha...very funny

Mkuu pamoja na habari hii kuandikwa na gazeti la Tanzania, pamoja na kuwa ipo hata hapa JF nakwambia kuwa hakuna lolote litakalotokea. Hii ni Tanzania, kama kweli mtu akichukuliwa hatua nitashangaa.
 
Back
Top Bottom