Rada siri yafichuka - wahusika wakubwa waanikwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rada siri yafichuka - wahusika wakubwa waanikwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Aug 8, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Aug 8, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG] [​IMG] [​IMG] ​​​
  SERIKALI na Utetezi wake
  Serikali imeelezwa kuwa imeamua kutofungua mashtaka dhidi ya vigogo wanaodaiwa kuhusika katika kashfa ya ununuzi wa rada kwa madai kuwa kesi hiyo ingemgusa mmoja wa marais wastaafu, na watu wa karibu wa Rais Jakaya Kikwete, imefahamika.

  Serikali inakingia kifua kulinda vigogo
  Serikali imekacha kufungua mashitaka kwa lengo la kuwalinda vigogo, mara ya kwanza iliibuliwa na mtandao maarufu wa Wikileaks, ambao umekuwa ukifichua siri nzito katika duru za kiserikali, kidiplomasia na kisiasa katika nchi nyingi duniani. Mchakato wa ununuzi wa rada hiyo iliyouzwa kwa bei ya kuruka ya sh bilioni 40, uliwahusisha watu wa madaraka na kada mbalimbali ambao ni pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Tony Blair.

  Tony
  Blair
  Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza, anatajwa kuwa ndiye aliyemshawishi aliyekuwa Rais wa Tanzania wakati huo, Benjamin Mkapa, kununua rada hiyo kutoka Kampuni ya kutengeneza silaha ya Uingereza, BAE-Systems.

  Clare Short
  Aliyekuwa Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa, alikataa katakata, na hata kumshauri Rais Mkapa kwamba Tanzania ni moja kati ya nchi masikini duniani, isingekuwa busara kutumia sh bilioni 40 kununua rada katikati ya umasikini unaonuka.

  Andrew Chenge (CCM)
  Mwingine anayetajwa kuishauri vibaya Serikali ni Mbunge wa Bariadi Mashariki, ambaye kwa muda mrefu amekuwa akitajwa ndani na nje ya chama chake kuhusika na kashfa ya ununuzi wa rada kutoka Kampuni ya BAE- System ya nchini Uingereza.
  Chenge, ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Fedha na Uchumi, anatajwa kuhusika kutoa ushauri wa kisheria wakati huo akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ushauri ambao unatajwa kuzingatiwa katika hatua za uamuzi.

  Dk. Idriss Rashid.
  Dr Idriss Rashid anayehusishwa na kashfa hiyo ni aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT),

  Tanil Somaiya, Sailesh (Shailesh) Vithlani
  Pamoja na hao, wanatajwa wafanyabiashara wenye asili ya India, lakini ambao wanaishi/walipata kuishi Tanzania, Tanil Somaiya, ambaye alikuwa akimiliki kampuni ya uwakala wa simu ya Shivacom na Sailesh (Shailesh) Vithlani kuwa watu wa kati wa biashara hiyo.

  Namna walivyochota mamilioni


  1. Kwa mujibu wa rasimu ya ripoti ya SFO (Taasisi ya Uchunguzi Makosa ya Jinai ya Uingereza), Chenge alipokea malipo ya jumla ya dola za Marekani milioni 1.5 (zaidi ya sh bilioni 1.5) kati ya Juni 1997 na Aprili 1998 kutoka Benki ya Barclays, tawi la Frankfurt.
  2. Fedha hizo zililipwa katika benki ya Barclays huko Jersey - Uingereza, katika akaunti inayomilikiwa na kampuni iliyotajwa kwa jina la Franton Investment Limited.
  3. Kampuni hiyo imetajwa kumilikiwa na Chenge, ikiwa ni maalumu kwa ajili ya uhamishaji fedha kiasi cha dola za Marekani 600,000 (zaidi ya sh milioni 600).
  4. Dola hizo 600,000 za Marekani zilihamishwa kutoka kwenye akaunti ya kampuni ya Chenge kwenda kwenye akaunti nyingine, inayomilikiwa na Kampuni ya Langley Investments Ltd, iliyokuwa ikiendeshwa na Dk. Idriss (aliyewahi pia kuwa Mkurugenzi wa TANESCO).
  5. Septemba 20, mwaka 1999, Chenge binafsi aliidhinisha uhamishaji wa dola za Marekani milioni 1.2 (zaidi ya sh bilioni 1.2) kutoka akaunti ya Kampuni (yake) ya Franton kwenda Royal Bank of Scotland International, huko Jersey.

  Serikali yajenga utetezi kupitia Rais Kikwete na Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe watetea

  Rais Kikwete, Waziri Mathias Chikawe
  Pamoja na wahusika walioliingiza mkenge taifa kujulikana, Rais Kikwete na Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe kwa nyakati tofauti wametoa msimamo wa serikali.

  Rais Kikwete
  katika mkutano wake na wahariri wa vyombo vya habari, alisema kuwa serikali yake haiwezi kumfikisha mahakamani mtu yeyote kwa vile hakuna rushwa katika ununuzi huo, na badala yake kulikuwa na makosa ya uchapaji katika kuweka kumbukumbu za fedha na mahesabu.

  Waziri Chikawe
  Juzi na jana alisema serikali haiwezi kumfikisha mtu yeyote mahakamani katika kesi ya rada, kwani hakuna ushahidi hasa baada ya Serikali ya Uingereza kukataa kuja kutoa ushahidi.
  Akijibu swali la Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA) jana bungeni, Chikawe alisisitiza kuwa serikali haina ushahidi wa kumshitaki mtu yeyote mahakamani kwa kashfa ya ununuzi wa rada.

  Alisema kutokana na hali hiyo, iwapo kuna mtu yeyote mwenye ushahidi wa kuaminika ndani au nje ya nchi auwasilishe na kwamba wataweza kwenda mahakamani wakati wowote. “Hili la rada, sina ushahidi, nilisema jana na nasema tena leo ndani ya Bunge hili kama yupo mtu, nje ya Bunge hili mwenye ushahidi ambao ni ‘credible’ wa kumshitaki mtu yeyote ambaye ni Mtanzania, tutamchukua mtu huyo na kwenda naye mahakamani kesho,” alisema Waziri Chikawe.

  Mbunge Mnyika
  Katika swali lake la msingi, Mnyika alisema kwa kuwa kampuni ya Uingereza ya silaha za kivita (BAE Systems) ilishakiri makosa ya kutoweka kumbukumbu za fedha na mahesabu katika mchakato wa mauzo ya rada kwa Serikali ya Tanzania, ni dhahiri kuna makosa yalifanyika ya kimanunuzi kati ya pande zote mbili, hali iliyosababisha kuwapo kwa tozo ya pauni milioni 29.5 kama fedha zilizochukuliwa na BAE Systems, hivyo wahusika wachukuliwe hatua.

  Pia alihoji serikali imewachukulia hatua gani waliohusika na mchakato wa ununuzi huo kwa upande wa Tanzania.
  “Katika hali kama hii tukichukua mtu na kumpeleka tutapata wapi ushahidi na tunaowategemea ni BAE na SFO ambao sasa kule hata kumtaja mtu hauruhusuwi. Na katika ushahidi ni lazima kuwapo na mtoaji na mpokeaji,” alisema.


  Bunge la Uingereza lapendekeza wahusika kufikishwa mahakamani
  Wakati serikali ikisema Uingereza imekataa kutoa ushahidi kwa vile hakuna rushwa, Bunge la nchi hiyo hiyo liliwahi kuitaka Serikali ya Tanzania iwafikishe mahakamani wote walioshiriki katika ununuzi wake na kuiingiza nchi katika hasara ya mabilioni ya fedha.

  Kupitia kamati yake ya Maendeleo ya Kimataifa, Bunge hilo limesema lingependa kuona watu wote walioshiriki katika mchakato wa ununuzi wa rada hiyo wakifikishwa mahakamani kujibu tuhuma za ufisadi.

  BBC ilinukuru taarifa ya Bunge la Uingereza
  Taarifa ya kamati hiyo iliyonukuliwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), ilieleza kwamba wajumbe wake ambao ni wabunge kutoka vyama mbalimbali nchini humo, walisema watatoa ushirikiano wa dhati kwa Tanzania iwapo itaamua kuwashtaki watuhumiwa hao nchini Tanzania au Uingereza.

  Kwa mujibu wa BBC, wabunge hao wamesema, mbali na kurudishiwa fedha iliyozidi kwenye ununuzi huo unaosemekana ulitawaliwa na rushwa, Serikali ya Tanzania inapaswa kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wote haraka iwezekanavyo ili haki itendeke.
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Aug 8, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Nakumbuka wiki iliyopita mada ya Mzee Mwanakijiji Ambayo aliongelea mazingaombwe kitu ambacho kwa maneno mengine kimezoeleka kutamkwa viini macho jinzi vinavyoendelea kutendeka ndani ya serikali yetu, hii ni sawa na sikio la kufa kutosikia dawa hata wahisani wanapotusaidia kufunua chombo chenye kutoa harufu ili kutoa uvundo na uchafu kisiendelee kuoza zaidi, lakini cha kushangaza viongozi wa ngazi za juu wenye kushikilia mhimili mkuu wa kuongoza nchi wakikingia kifua kwa nguvu zote bila kutoa hata mwanya wa kuruhusu vyombo vya sheria kuchukua hatua.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #3
  Aug 8, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  AG anataka ushahidi upi? serikali dhaifu
   
 4. h

  hans79 JF-Expert Member

  #4
  Aug 8, 2012
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  chikawe na mr dhaifu wote wezi,unategemea nani wa kumpeleka mwenzake mahakamani ili hali wote wamenawa kamzigo ka rada.Kumpeleka Chenge na Idrisa mahakamani ni sawa na nhinyiemu kujifukia yenyewe kaburi. Wahusika wakuu ni mr dhaifu, mr benjamin,chenge,waziri wa fedha wakati huo,idrisa,hosea,na wengineo wengi.Suala hili vigogo wengi wengi wa nyinyiemu wamo,ila waendelee tu kujiteteana lakini ipo siku kila kitu kitakuwa wazi.
   
 5. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #5
  Aug 8, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Hiyo ndo ccm bana
  serikali dhaifu inayoongozwa na Rais dhaifu!
   
 6. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #6
  Aug 8, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Rais dhaifu unategemea awe na Watendaji makini?
   
 7. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #7
  Aug 8, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  acha kikwete amalize mda wake watakiona tu
   
 8. m

  markj JF-Expert Member

  #8
  Aug 8, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 1,756
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  kweli mtu ukiitwa dhaifu hapa utakasirika nini! yani kipi cha kutetea sasa kwenye ili swala kama si ujambazi wa waziwazi tu huu! i
   
 9. K

  Kassim Awadh JF-Expert Member

  #9
  Aug 8, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 887
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Mkuu mbona hakuna siri mpya hapa? Yote haya yalishaanikwa kitambo sana plus majina ya wahusika uliyoyaweka
   
 10. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #10
  Aug 8, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kashfa ya Rada Rais Kikwete anahusika kwa kuwa kipindi hicho alikuwa Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na ushirikiano wa Kimataifa, hivyo jambo kama hilo lisingepitia nyuma ya mgongo wake. Huku kukingia kifua ni jambo linaloweza kujenga taswira ya woga wakubwa wengi wanahusika.
   
 11. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #11
  Aug 8, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Wengine ni kizazi cha Akina Lulu hawajui yaliyotokea mwaka juzi.
   
 12. lm317

  lm317 JF-Expert Member

  #12
  Aug 8, 2012
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 452
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Unatakiwa ushahidi "credible"
   
 13. MATESLAA

  MATESLAA JF-Expert Member

  #13
  Aug 8, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,252
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mweshimiwa kawalinda majambazi kama vp hata yeye ni jambazi
   
 14. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #14
  Aug 8, 2012
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Ukimya wa watanzania kuna siku utatoa majibu.
   
 15. KIJOME

  KIJOME JF-Expert Member

  #15
  Aug 8, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 3,079
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  hakuna dhuluma iliyowahi kuishinda haki hata siku moja...time will tell....
   
 16. K

  Kassim Awadh JF-Expert Member

  #16
  Aug 8, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 887
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Nimekupata Mkuu,,wapo pia wale vichwa vya panzi!
   
 17. tonnyalmeida

  tonnyalmeida JF-Expert Member

  #17
  Aug 8, 2012
  Joined: Feb 1, 2012
  Messages: 226
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hao mawaziri wanamfata Dhaifu na Kusahau mwenzao anakinga ya kutokushitakiwa akimaliza mda wake ndipo watakapokijua cha moto.
   
 18. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #18
  Aug 9, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,839
  Trophy Points: 280
  Kweli hii nchi ni shamba la bibi!
   
 19. salosalo

  salosalo JF-Expert Member

  #19
  Aug 9, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 579
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  Hata kama hamna ushahidi, inamaana biashara ilifanyika bila mkataba? Nini kinathibitisha Tanzania inastahiri kurudishiwa pesa za rushwa ambazo siku hizi wanaziita change za radar? Upuuzi mtupu huu. Hizo change za radar toka Uingereza Tz inapokea kama posa? kama si hivyo ulisikia wapi mtu analipa Tsh 50,000/= ili arudishiwe change ya Tsh 20,000/= au siku hizi Tz tuna note ya Tsh 50,000/=?
   
 20. Borat69

  Borat69 JF-Expert Member

  #20
  Aug 9, 2012
  Joined: Jun 17, 2012
  Messages: 2,536
  Likes Received: 1,220
  Trophy Points: 280
  Wakuu,
  Mh. Chenge Vijisenti anatumia OBAGI products (mkorogo)!? Au kwenye hiyo picha Camera imemtoa anabadilika rangi Kama kinyonga!
   
Loading...