R.I.P Shekh Mtopea

Dark City

JF-Expert Member
Oct 18, 2008
16,253
11,599
Nimesikia kwenye magazeti ya leo asubuhi kuwa Shekh maarufu na mwanasiasa, kada wa CCM Mtopea alifariki juzi na kuzikwa jana huko Temeke.

Shekh Mtopea namkumbuka sana katika mambo mengi ila kubwa ni ushiriki wake katika uchaguzi mdogo wa Temeke miaka ya 1990, ambako Mrema alimbwaga Sisco Mtiro wa CCM. Mtopea na Ditto Mzuzuri walikuwa waigizaji muhimu katika kampeni za uchaguzi huo.

Mungu aiweke roho ya Shekh Mtopea mahali pema pepono, AMEN!
 
Poleni sana wafiwa. marehemu nilimfahamu kupitia kwa mwanae tuliesoma nae malangali miaka ya late 1990s. Mungu ailaze mahali pema peponi, Amina
 
Shekh Mtopea ana mchango mkubwa katika siasa za mageuzi.CCM haikuanza leo siasa za udini hasa inapokumbana na upinzani mkali Shekh Mtopea alimsaidia sana A L Mrema kipindi hicho kubalance udini ulikokuwa ukitumiwa na CCM.

RIP Mtopea.
 
R.I.P Sheikh Mtopea, nilisoma na kijana wake Selemani Mtopea kule Iringa na mzee alikuwa akija kumjulia hali kijana wake.
Kwa kweli mchango wake kwa Mrema akiwa NCCR hautasahaulika.
 
Alale pema peponi sheikh mtopea. Nimekumbuka kipindi kile cha uchaguzi wa marudio TEMEKE. Mchuano ulikuwa kati ya A.L..MREMA-Nccr mageuzi na SCICO - wa CCM
 
Shekh Mtopea ana mchango mkubwa katika siasa za mageuzi.CCM haikuanza leo siasa za udini hasa inapokumbana na upinzani mkali Shekh Mtopea alimsaidia sana A L Mrema kipindi hicho kubalance udini ulikokuwa ukitumiwa na CCM.

RIP Mtopea.

Pamoja na mchango huo, marehemu kaacha familia kwenye hali ya umaskini mkubwa, inabidi familia yake ikumbukwe kwa mazuri baba yao aliyoyafanya na sio kusahaulika kama Mohamed Ali Juma (makamu wa raisi)
 
Mungu amlaze pema shekhe Mtopea, nasi twaja pia njia ya kila mmoja.marehemu watarajiwa.
 
Back
Top Bottom