Queen Sendiga akabidhiwa ilani ya CCM

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
87,062
2,000
Ukikubali cheo cha bure lazima ukubali na masharti ya mtoa cheo , Mtaka cha uvunguni sharti ainame

Swahili_Times_(@swahilitimes)_posted_on_Instagram_•_May_24,_2021_at_9:09am_UTC%22_(1).jpgIfahamike kwamba hapa duniani hakuna kitu cha bure , nipe nikupe , haiwezekani Magonjwa Mtambuka aliyepigania ccm kufa na kupona atelekezwe halafu upewe wewe ukuu wa mkoa bila masharti yoyote , hicho kitu hakuna

Sasa huyu dada siku yoyote msishangae mkimuona akikabidhiwa kadi ya ccm " kwa mara ya pili "
 
Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
18,246
2,000
🤣🤣🤣🤣

Malkia mwenye kauli tamu bana!!!

Mpinzani wa kweli hawezi kufanya kazi ndani ya serikali ya CCM kutekeleza ilani ya CCM.

Ahadi ya Mama ilikuwa ni maneno matamu tu ya kuwapoza watu walio na uelewa finyu wa mambo.
Watu ni wale wale. Lengo ni FURSA ya kutafuna keki ya taifa na kutokukaa JOBLESS.

Hata leo CHADEMA wakishika Dola hao CCM watahamia huko huko CHADEMA kwa fujo.

Wakishika Dola CHAUMA ni hivyo hivyo, hao hao CCM wanaoitwa hawafai watahamia huko huko CHAUMA.

Biblia inasema "Palipo na Mzoga ndipo wakusanyikiapo TAI"

Kenya KANU haipo, ila watu wale wale wa KANU ndio walioshika madaraka kupitia JUBILEE.
 
Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
14,737
2,000
Mpinzani wa kweli kabisa anajijua moyoni mwake na huwezi kumuona kwa kumtazama usoni.

Maslahi binafsi ya mtu yanatazamwa siku zote. Mama Anna Mgwhira kwa muda wote aliokuwa mkuu wa mkoa Kilimanjaro kajikusanyia mpunga wake wa moyoni na sasa anajiandaa kupokea pensheni yake nono.

Profesa Lipumba anazunguka majukwaani akigombea urais halafu uchaguzi ukimalizika anaunganishiwa kazi moja ya maana Ulaya anakaa huko miezi sita au mwaka halafu anarudi bongo akiwa vizuri akaunti zikisoma vyema.

Siasa zipo na maslahi ya mtu ya leo na kesho yapo pia.
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
28,996
2,000
Ukikubali cheo cha bure lazima ukubali na masharti ya mtoa cheo , Mtaka cha uvunguni sharti ainame

View attachment 1796168

Ifahamike kwamba hapa duniani hakuna kitu cha bure , nipe nikupe , haiwezekani Magonjwa Mtambuka aliyepigania ccm kufa na kupona atelekezwe halafu upewe wewe ukuu wa mkoa bila masharti yoyote , hicho kitu hakuna

Sasa huyu dada siku yoyote msishangae mkimuona akikabidhiwa kadi ya ccm " kwa mara ya pili "
Wale wanasiasa malaya malaya by J K Nyerere
 
Kadhi Mkuu 1

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
11,150
2,000
Ukikubali cheo cha bure lazima ukubali na masharti ya mtoa cheo , Mtaka cha uvunguni sharti ainame

View attachment 1796168

Ifahamike kwamba hapa duniani hakuna kitu cha bure , nipe nikupe , haiwezekani Magonjwa Mtambuka aliyepigania ccm kufa na kupona atelekezwe halafu upewe wewe ukuu wa mkoa bila masharti yoyote , hicho kitu hakuna

Sasa huyu dada siku yoyote msishangae mkimuona akikabidhiwa kadi ya ccm " kwa mara ya pili "
Kaamua kuitumikia nchi inayoongozwa na CCM. Katibu mkuu wenu alipoteuliwa ubalozi alikabidhiwa pia ilani ya CCM.
Anna Mghwira alikabidhiwa pia ilani ya CCM.
Unaponda uteuzi kuuita kitu Cha bure sababu hajateuliwa mwanasaccos.

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Masahihisho - Dr Slaa alikwishajiuzulu vyeo vyote Chadema kwa maelezo ya kuwakimbia Sumaye na Lowassa ndio akahongwa ubalozi , Hakuwa Katibu Mkuu wa Chadema , cha kushangaza sasa leo hii yuko Chama kimoja na Rostam , Lowassa na Sumaye na wala hajakimbia !
 
sweettablet

JF-Expert Member
Nov 16, 2014
7,450
2,000
Ukikubali cheo cha bure lazima ukubali na masharti ya mtoa cheo , Mtaka cha uvunguni sharti ainame

View attachment 1796168

Ifahamike kwamba hapa duniani hakuna kitu cha bure , nipe nikupe , haiwezekani Magonjwa Mtambuka aliyepigania ccm kufa na kupona atelekezwe halafu upewe wewe ukuu wa mkoa bila masharti yoyote , hicho kitu hakuna

Sasa huyu dada siku yoyote msishangae mkimuona akikabidhiwa kadi ya ccm " kwa mara ya pili "
Hata Lissu akiteuliwa aidha Ubalozi au Uwanasheria Mkuu au Ukatibu Tarafa Ikungi lazima akabidhiwe ILANI YA CCM ili akaisimamie na kuitekeleza. Kwahiyo, mnapofurahia kauli ya Mama kujumuishwa kwenye Serikali msilisahau hilo.
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
49,062
2,000
Masahihisho - Dr Slaa alikwishajiuzulu vyeo vyote Chadema kwa maelezo ya kuwakimbia Sumaye na Lowassa ndio akahongwa ubalozi , Hakuwa Katibu Mkuu wa Chadema , cha kushangaza sasa leo hii yuko Chama kimoja na Rostam , Lowassa na Sumaye na wala hajakimbia !
Aibu yake
 
sweettablet

JF-Expert Member
Nov 16, 2014
7,450
2,000
Samia lazima achague wapinzani "soft" ili afanye nao kazi kwa amani, akichagua vichwa ngumu watampasua kichwa, sipati picha Lema au Mbowe akabidhiwe hiyo ilani then ainyanyue juu namna hiyo.
Acha dharau weweee! Achaguliwe Lema ili afanye kazi gani katika Serikali ya Tanzania!?
 
Drifter

JF-Expert Member
Jan 4, 2010
2,998
2,000
Tanzania hii watumishi wa umma wanatakiwa kutekeleza "ilani ya CCM"! Hizi ni mambo za nchi za kikomunisti. Ilani ni ya wenye chama. Inaishia huko huko kwao. Wao wenye chama wanatakiwa kupeleka bungeni mapendekezo ya miradi na marekebisho ya sheria kuhusiana na ahadi zao na kuyatetea. Yakipita ndipo hukabidhiwa serikalini kwa utekelezaji. Hizi picha za kukabidhi ilani ni aibu kwa taifa lenye waelewa. Ni kama vile wote tumekuwa hamnazo, illiterates, ignorants.

Yaani tunaona sawa tu kudai kuwa "serikali inatakiwa kutekeleza ilani ya chama kilichoko madarakani - CCM"! UNFILTERED. Ni kama leo Kevin McCarthy na Mitch McConnell kule US wadai kwamba wako pale kuhakikisha "ilani" ya Democrats inatekelezwa. Capitol itavamiwa mara ya pili kwa kwa kishindo kikubwa zaidi. Hadi hapo, bunge linakuwa halina maana zaidi ya kuwa taasisi ya watu fulani kugawana maslahi basi. Nchi ishakuwa a complete banana republic.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom