Qaswida ni muziki au sio muziki?

Qaswida ni muziki au sio muziki?

Wallahi Qaswida hizi za kileo ni Muziki tena zinamadhara Makubwa kuliko Bongo Fleva maana hizi Qaswida ni Bidaa Sugu ambayo baadhi ya Waislam wasiojielewa wanazitumia eti kama Njia ya Dawa / kulingania watu SubhanAllah
 
kaswida/ qaswida kama ina beat ni haramu ila kama haina beat sio haramu, kinachoharamisha muziki ni maneno na beat, so kawida zina ujumbe mzuri ila beat ndo tatizo linalopelekea kua haramu, zipo kaswida ambazo hazina beat na zinaruhusiwa mfano ile kaswida aliyoimba marehemu Michael Jackson inaitwa Give Thanks To Allah, haina beat na michael aliulizwa akafundishwa ndo mana akafanya vile
NB,kuna kaswida zinaitwa Nasheedi hizi/haya ni mashairi ambayo hayana beat yanaruhusiwa na hua yanamsifia Mungu, mitume,manabii na kufundisha jamii
Uliwahi kuona wapi inanoga bila dufu? ka,ma sikosei dufu ni zile aina za ngoma zilizokatwa hizo ni beat pot ndio zinatunza mwondoka/mapigo (time signature) za wimbo husika na zile filimbi zinazopigwa kunogesha ni sawa sawa na kinanda tuu kwani hata kinanda unaweza ku seat pure flute na ukazitunmia kwa minajili hiyo
 
Sio kuchora tuu sasa hivi nipo mefungua progam zangu za kuchora nota za muse score na sibellius naweza kuchora dakika moja na ku harmonize lakini sitaki kufanya hivyo kwa sababu

1. Ninaheshimu misingi ya dini ya wengine na ninajua nyia moja wapo ya kutunza taaluma zenu za dini ni kukariri ( kuhifadhi) kuanzia maandiko hadi sauti hivyo nikifanya hivyo watu wataanza kujifunza muziki ili wafuate mwenendo wa nota na hivyo kuaharibu asili ila nilikuwa nakujulisha tuu kuwa inawezekana na ni kazi rahisi sana maana hakuna sauti ambazo zinashindikana mbele ya DO-RE-MI-FA-SO-LA-TI-DO
kaka unaweza kunisaidia kutafuta vocal nataka kuanza kuimba gospel shida ni vocal
 
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa
sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu hukumu ya muziki inayotiwa katika Nashiyd na Qaswiydah.
Muziki na utumiaji wa ala za muziki ni haramu katika Dini yetu hii, Uislamu. Zifuatazo ni dalili kuhusu hilo:
Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “ Kutakuwa watu katika Ummah wangu watakao halalisha uzinzi, uvaaji wa Hariri, pombe (unywaji) na ma’aazif (ala za muziki) ” (al-Bukhaariy).
Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “ Mwisho wa zama (dunia) kutakuwa na maporomoko ya ardhi, mawe kutoka mbinguni na kugeuza kwa wanyama, wakati ambapo ala za muziki na waimbaji wanawake watakapoenea na pombe kuruhusiwa ” (atw-Twabaraniy).
Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “ Watu katika ummah wangu watakunywa pombe, kuiita kwa jina jingine. Watatiwa furaha kwa uchezaji wa ala za muziki na uimbaji wa wanawake (watakao waimbia). Allaah Ataifanya ardhi kuwameza wote na kuwageuza kuwa nyani na nguruwe ” (Ibn Maajah).
Na Allaah Aliyetukuka Amesema:
“ Na katika watu wako wanaokhitari maneno ya upuuzi ili wawapoteze watu na njia ya Allaah, pasipo wao kujua lolote, na wanaicheza shere hiyo njia ya Allaah. Basi hao watapata adhabu ifedheheshayo ” (Luqmaan [31]: 6).
Ibn Jariyr atw-Twabariy katika Jaami‘ul Bayaan amesema kuwa rai ya mufasirina wa Qur-aan kuhusiana na maana ya ibara “ Lahwal Hadiyth (maneno ya upuuzi) ” inaweza kugawanywa katika aina tatu. Nazo ni:
1. Uimbaji na kusikiliza nyimbo.
2. Kuajiri au kununua waimbaji wataalamu, wanaume na wanawake.
3. Kununua ala za starehe.
Rai hii ndio iliyokuwa rai ya Maswahaba wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kama Ibn Mas‘ud, Jaabir bin ‘Abdillaah na Ibn ‘Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhum) {al-Kanadi Mustafa Abu Bilaal, The Islamic Ruling on Music and Singing in the Light of the Qur’an, Sunnah and the Consensus of the Salaf (Hukumu ya Kiislamu ya Muziki na Nyimbo katika Muono wa Qur-aan, Sunnah na Ijmaa ya Watangu Wema, uk. 9}.
Na pale Ibn Mas‘ud (Radhiya Allaahu ‘anhu) alipoulizwa kuhusu Aayah hii, alijibu: “ Naapa kwa Yule ambaye hakuna Mola ila Yeye kuwa Aayah hii inamaanisha muziki” . Naye aliikariri ibara hiyo mara tatu kuitilia mkazo rai yake hiyo. Na waliokuwa na rai hiyo katika Tabi‘iyn ni ‘Ikrimah, Mujaahid, Makhuul, ‘Umar bin Shu‘ayb na wengineo.
Hata hivyo, upo wakati ambao mashairi yanaruhusiwa kuimbwa bila ya kuwepo kwa ala za muziki isipokuwa daff (dufu, twari) tu kwa wanawake. Na hali hizo ni kama:
1. Wakati wa Jihaad na mapambano mengine katika Njia ya Allaah Aliyetukuka. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiimba wakati wa Vita vya Khandaq (Muslim).
2. Wakati wa sherehe za Kiislamu kama ‘Iyd al-Fitwr na ‘Iyd Al-Adhwhaa.
3. Pia ruhusa imetolewa kwa wanawake na wasichana kuimba na kupiga daff (dufu) wakati wa harusi.
Bonyeza kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi:
Hukmu Ya Muziki Katika Qur-aan Na Sunnah - Ewe Upendaye Nyimbo Na Muziki, Haujafika Wakati Wa Kuogopa Adhabu Kali Za Allaah?
Ngoma, Muziki Haramu
Na Allaah Anajua zaidi
Email Telegram WhatsApp
vizuri je Qaswida ni muziki maana Kuna vionjo vyote vya muziki
 
Uliwahi kuona wapi inanoga bila dufu? ka,ma sikosei dufu ni zile aina za ngoma zilizokatwa hizo ni beat pot ndio zinatunza mwondoka/mapigo (time signature) za wimbo husika na zile filimbi zinazopigwa kunogesha ni sawa sawa na kinanda tuu kwani hata kinanda unaweza ku seat pure flute na ukazitunmia kwa minajili hiyo

Dufu haziruhusiwi pia kaka ni beat pia wanatengeneza ala pale, tena siku hizi huku mtaani hadi wanacheza viduku na kubambiana kabisa kama disko dini haisemi ivo that y siku hizi madufu yanapungua si kama zamani watu wanaelimika wanasoma kikubwa ni Elimu Elimu Elimu, na pia dufu wanaruhusiwa kupiga wasichana tu tena wakiwa wenyewe, enzi hizo madugu yalipigwa siku moja wakati mtume anatoka makka kwenda madina alikaribishwa na madufu na wapigaji walikua ni wasichana, hakuwakataza wala kuwaambia waendelee kipiga dufu
 
Acha uboya ww kama huna la kusema kaaga kimya !!!
Brother, mbona unashangaa!! nilichokisema ni kweli kabisa na wala sijatia chunvi. Hizo nota zake ni rahisi zana na muziki wake unafanana sana na sauti za kilatini cha kale ( gregorian chant) hivyo usidhani nina lengo baya kama huelewi embu fanya utafiti kwa watu waliosoma vyuo vya muziki.
 
uislamu unapinga muziki je Qaswida nini au Ni aina gani ya muziki ambao wanaupinga na kuita haramu
mziki akiimba mkristo waitwa KWAYA
mziki akiimba mkongo waitwa DANSI
mziki huo huo akiimba kijana kama alikiba waitwa Bongofleva
mziki huohuo akiimba fid Q waitwa Hip Hop
mziki huohuo akiimba mtu wa pwani waitwa taarabu au kisingeli
mziki huohuo wakiimba wahuni waitwa mchiriku
mziki huohuo akiiimba muislamu waitwa QASWIDA!!!
Kwa lugha nyepesi tu mziki ni HARAMU kwa mujibu wa QURAN TUKUFU!!
Assalam alaykum warahmatullahi wabaraakatuh!!
 
Sio kaswida tuu hata ile sauti ya adhana ni muziki kwani naweza kukuchorea nota zake kwa sababu ni melodic
Huko ulikofika mkui siko, adhana ya duniani hadithi za Mtume (S.A.W) zinatufunza kuwa inasikika hadi mbinguni kwa Mwenyezi Mungu na ndiyo maana hapaswi mwiisilamu kuongea wakati wa adhana.
 
Huko ulikofika mkui siko, adhana ya duniani hadithi za Mtume (S.A.W) zinatufunza kuwa inasikika hadi mbinguni kwa Mwenyezi Mungu na ndiyo maana hapaswi mwiisilamu kuongea wakati wa adhana.
Kusikika mpaka mbinguni ninatambua sana hilo naliheshimu na nakubali issue n moja tuu je! inawezwa kuchorwa kwenye nota za muziki ambapo mtu yeyote aliyesoma muziki anaweza kuimba kwa ufasaha bila kukosea hata sehenu moja??? jibu ni ndio
 
LABDA MNASHINDWA KUELEWANA SEHEMU MOJA NI KUWA KILICHOHARAMISHWA NI ALA NA SIO USHAIRI WAKE
 
LABDA MNASHINDWA KUELEWANA SEHEMU MOJA NI KUWA KILICHOHARAMISHWA NI ALA NA SIO USHAIRI WAKE
Ala ninazozifahamu kuwa zinatumika ni

1. Dufu

2. Filimbi

3. Kule zanzibar kuna filimbi fulani mfano wa tarumbeta sijui zinaitwaje
Hizo zote ni ala za muziki ( music instruments)
 
Brother, mbona unashangaa!! nilichokisema ni kweli kabisa na wala sijatia chunvi. Hizo nota zake ni rahisi zana na muziki wake unafanana sana na sauti za kilatini cha kale ( gregorian chant) hivyo usidhani nina lengo baya kama huelewi embu fanya utafiti kwa watu waliosoma vyuo vya muziki.
Hivi ww unajua kuwa Adhana ni katika nembo kubwa ya Uislam hapewezi sehemu kutambulikuwa kuwa kuna uislam bila ya kuwepo Adhana hiki ni kitu kitukufu sana tena sana kwaiyo huwezi ukafananisha na sauti ya Shaytwan "Mziki " naomba "do not compare btn these two things "
 
Kaswida yapaswa kuwa aina ya ghani kama vile mnavyo sema kanisani "Bwaaana aawe nanyi" .
Wanaoutia mziki wanakosea sawa na wale wanaochukua beat ya Koffi Olomide na kuigeuza gospel
 
Uliwahi kuona wapi inanoga bila dufu? ka,ma sikosei dufu ni zile aina za ngoma zilizokatwa hizo ni beat pot ndio zinatunza mwondoka/mapigo (time signature) za wimbo husika na zile filimbi zinazopigwa kunogesha ni sawa sawa na kinanda tuu kwani hata kinanda unaweza ku seat pure flute na ukazitunmia kwa minajili hiyo
Mkuu yaelekea wewe ni mtaalamu wa muziki

Natamani sana kujua kupiga kinanda...hata kwa kulipa pesa.

Seriously.
 
Mkuu yaelekea wewe ni mtaalamu wa muziki

Natamani sana kujua kupiga kinanda...hata kwa kulipa pesa.

Seriously.
Kama ndio mgeni kabisa, mkuu bora ujifunze kwanza hata elementary level ya muziki kujua angalau

1. Key na aina zake ili unaposhika kinanda angalau ujue unafanya nini maana utaona rangi mbili tuu nyeupe na nyeusi ambazo zimepangiliwa 2 kwa tatu

2. Angalau ujue aina za mapigo ya muziki na kwa kuanzia zakutosha kujua 4/4, 2/4, 3/4 3/8 nk

3. Angalau ukariri sauti za msingi wa muziki wowote DO-RE- MI - FA - SO - LA- TI- DO ( wengine wanaita solfa notation)
Hii itakusaidia kujua kwa uhakika sauti unayopiga kwenye kinanda na haka kama utaboyeza key tofauti ikalia off key utajua

4. Ukikomaa komaa ukijifunza angalau staff notation sio mbaya kwani waweza kuzitumia hizo kuupiga wimbo ambao hata hujawahi kuusikia na akalia kama mtunzi alivyotunga (Hii staff notation ndio yale madude ambayo kwa mbali ukiangalia waweza kusema labda ni maandishi ya kiarabu lakini ndio muziki wenyewe)

5. Ukitaka kubobea zaidi sasa tafuta zile lesson za fingering ambazo zitakuonyesha njia sahihi za kupanga vidole vyako unaposhika kinanda na sio kujibonyezea bonyezea tuu.

6. Kama kweli unatamani kujua kinanda, au unauna umri wako umeenda huwezi au huna muda wa kutulia kujifunza basi waandalie wanao, nunua angalau portable key bord weka sebuleni wakichoka kusoma wana piga kwani watakizoea na wakipata mtu wa kuwaelekeza kidogo watakuwa wataalamu. Kumbuka wapigaji vyombo mahiri karibia wengi either mzazi wao alikuwa na chombo hicho nyumbani au wamejifunzia kwenye nyumba za inada.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom