Qaswida ni muziki au sio muziki?

Qaswida ni muziki au sio muziki?

WAIMBA MUZIKI WENGI BONGO NI DINI HIYO.
 
"Hekma" na ukongwe wako vimenifanya nisikupe harsh-counterargument".
Muziki kama muziki hauwi defined kwa dini..Rather an "artistic form of auditory communication" involving instrumental or vocal tones in a well arranged and continuous manner...!
Hata hivyo nadhani muuliza swali kuna kitu alitaka kujua,;ni bahati mbaya hakujua namna ya kuliweka swali lake.
Kwa Ufupi, Kwaswida (Qaswida) ni genre ya muziki, ikirandana na Classical/Baroque genre.
kaka umejibu vizuri sana, kaswida hazishabihiani kokote na uislam, bali ni genre
 
Ukiniambia zile sauti (maana mnasema ala sijui muziki, sijui nota) nazosikiaga kitaani kwetu kipindi cha sherehe za ndoa, ramadhan na eidy sio muziki ntakupinga mpaka mwisho!.😀😀😀😀
 
Khadiria, hatuukubali muziki wa aina yeyote ile. Ushafaham, hata ili adhana hatuitaki ila tukuiteje tu weye muislam ujue saa ya swalaa imefika?? Zamani kidogo, late 60's tulikuwa na muidhini/muita swala akitembea barabaran saa 11 asubuhi kutuita twende swalaa. Kulipokuja vipaaza sauti tukamwacha huyu. Sasa twaitiwa kule kule msikitini. Qaswida ni muziki tuu
 
Sio kaswida tuu hata ile sauti ya adhana ni muziki kwani naweza kukuchorea nota zake kwa sababu ni melodic
Tambua kwamba uislamu una sheria zake na taratibu zake.
Muziki kwa sheria ya kiislamu ni ule unaojumuisha ala. Sasa adhana haina ala
 
Neno Qaswida (قصيدة)maana yake ni nyimbo.
Mleta mada bila ya shaka alitaka kujua uhalali wa muziki katika uislam. Bila ya shaka uislam unapinga na kuharamisha muziki, iwe inaimbwa kwa kuegemezea kwenye dini au vyovyote vile.
Na wale wote wanaoimba hizo nyimbo na kutia ala za muziki wanafanya makosa.
jibu murua no discusion mkuu
 
uislamu unapinga muziki je Qaswida nini au Ni aina gani ya muziki ambao wanaupinga na kuita haramu
Kaswida kama kaswida ni kumsifu na kumtukuza mtume bila ya kutumia kitu kilichowambwa na ngozi! Nikusoma tu na kumswalia bwana wetu mtume!! Sasa unachokiona sasa hivi hizi ni mabadiliko yakidunia tu na wala mtume hakuyafanya haya uyaonayo! Ila wakikubali kusoma basi wataepuka kufanya haya wayafanyao!! So ukiona ngoma zinapigwa na danci zinaangushwa basi jua kabisa wanafanya makosa!!
 
Tambua kwamba uislamu una sheria zake na taratibu zake.
Muziki kwa sheria ya kiislamu ni ule unaojumuisha ala. Sasa adhana haina ala
Hata kama hauna ala bado ni muziki. Ina maana nikienda studio kurekodi wimbo wangu bila kutumia kifaa chchote cha muziki, hautaitwa wimbo? je ! wewe wafahamu maana ya accappela ? HUO NI MUZIKI UNAOIMBWA BILA ALA YOYOTE BALI SAUTI ZA BIN ADAM TUU.
 
Kaswida kama kaswida ni kumsifu na kumtukuza mtume bila ya kutumia kitu kilichowambwa na ngozi! Nikusoma tu na kumswalia bwana wetu mtume!! Sasa unachokiona sasa hivi hizi ni mabadiliko yakidunia tu na wala mtume hakuyafanya haya uyaonayo! Ila wakikubali kusoma basi wataepuka kufanya haya wayafanyao!! So ukiona ngoma zinapigwa na danci zinaangushwa basi jua kabisa wanafanya makosa!!
Kumsisifu mtume kupita ngoma!!!!!! Kama sio umedata kiwe nini, Kumsifu na kumtukuza Mtume صل الله عليه وسلم ni kwa Kushika na kufuata Sunnah zake
 
Back
Top Bottom