Qaswida ni muziki au sio muziki?

Qaswida ni muziki au sio muziki?

JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa
sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu hukumu ya muziki inayotiwa katika Nashiyd na Qaswiydah.
Muziki na utumiaji wa ala za muziki ni haramu katika Dini yetu hii, Uislamu. Zifuatazo ni dalili kuhusu hilo:
Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “ Kutakuwa watu katika Ummah wangu watakao halalisha uzinzi, uvaaji wa Hariri, pombe (unywaji) na ma’aazif (ala za muziki) ” (al-Bukhaariy).
Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “ Mwisho wa zama (dunia) kutakuwa na maporomoko ya ardhi, mawe kutoka mbinguni na kugeuza kwa wanyama, wakati ambapo ala za muziki na waimbaji wanawake watakapoenea na pombe kuruhusiwa ” (atw-Twabaraniy).
Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “ Watu katika ummah wangu watakunywa pombe, kuiita kwa jina jingine. Watatiwa furaha kwa uchezaji wa ala za muziki na uimbaji wa wanawake (watakao waimbia). Allaah Ataifanya ardhi kuwameza wote na kuwageuza kuwa nyani na nguruwe ” (Ibn Maajah).
Na Allaah Aliyetukuka Amesema:
“ Na katika watu wako wanaokhitari maneno ya upuuzi ili wawapoteze watu na njia ya Allaah, pasipo wao kujua lolote, na wanaicheza shere hiyo njia ya Allaah. Basi hao watapata adhabu ifedheheshayo ” (Luqmaan [31]: 6).
Ibn Jariyr atw-Twabariy katika Jaami‘ul Bayaan amesema kuwa rai ya mufasirina wa Qur-aan kuhusiana na maana ya ibara “ Lahwal Hadiyth (maneno ya upuuzi) ” inaweza kugawanywa katika aina tatu. Nazo ni:
1. Uimbaji na kusikiliza nyimbo.
2. Kuajiri au kununua waimbaji wataalamu, wanaume na wanawake.
3. Kununua ala za starehe.
Rai hii ndio iliyokuwa rai ya Maswahaba wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kama Ibn Mas‘ud, Jaabir bin ‘Abdillaah na Ibn ‘Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhum) {al-Kanadi Mustafa Abu Bilaal, The Islamic Ruling on Music and Singing in the Light of the Qur’an, Sunnah and the Consensus of the Salaf (Hukumu ya Kiislamu ya Muziki na Nyimbo katika Muono wa Qur-aan, Sunnah na Ijmaa ya Watangu Wema, uk. 9}.
Na pale Ibn Mas‘ud (Radhiya Allaahu ‘anhu) alipoulizwa kuhusu Aayah hii, alijibu: “ Naapa kwa Yule ambaye hakuna Mola ila Yeye kuwa Aayah hii inamaanisha muziki” . Naye aliikariri ibara hiyo mara tatu kuitilia mkazo rai yake hiyo. Na waliokuwa na rai hiyo katika Tabi‘iyn ni ‘Ikrimah, Mujaahid, Makhuul, ‘Umar bin Shu‘ayb na wengineo.
Hata hivyo, upo wakati ambao mashairi yanaruhusiwa kuimbwa bila ya kuwepo kwa ala za muziki isipokuwa daff (dufu, twari) tu kwa wanawake. Na hali hizo ni kama:
1. Wakati wa Jihaad na mapambano mengine katika Njia ya Allaah Aliyetukuka. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiimba wakati wa Vita vya Khandaq (Muslim).
2. Wakati wa sherehe za Kiislamu kama ‘Iyd al-Fitwr na ‘Iyd Al-Adhwhaa.
3. Pia ruhusa imetolewa kwa wanawake na wasichana kuimba na kupiga daff (dufu) wakati wa harusi.
Bonyeza kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi:
Hukmu Ya Muziki Katika Qur-aan Na Sunnah - Ewe Upendaye Nyimbo Na Muziki, Haujafika Wakati Wa Kuogopa Adhabu Kali Za Allaah?
Ngoma, Muziki Haramu
Na Allaah Anajua zaidi
Email Telegram WhatsApp
 
nini maana ya ala?
1.Ala ni kifaa ama kwa kiingereza twaweza kusema ni '' instrument"

2.Kuna uimbaji wa sauti kavu kavu ( accappela) na uimbaji wa kutumia sauti pamoja na vifaa vya kuboreshea (music instruments)

3. Vifaa hivi vya kuimbia ( music instruments) vimegawanyika kaatika sehemu nyingi na vina majina tofauti kama ngoma ( hata dufu ni ngoma) filimbi ( nadhani hizi mnazitumia sana kwenye qaswida) vinanda, magitaa, vyote hivyo ni ala za muziki sasa inategemea mpigaji ame seti kifaa chake au anapiga mapigo gani ndio zinatofautisha aina za muziki lakini ala ni zile zile.
 
Neno Qaswida (قصيدة)maana yake ni nyimbo.
Mleta mada bila ya shaka alitaka kujua uhalali wa muziki katika uislam. Bila ya shaka uislam unapinga na kuharamisha muziki, iwe inaimbwa kwa kuegemezea kwenye dini au vyovyote vile.
Na wale wote wanaoimba hizo nyimbo na kutia ala za muziki wanafanya makosa.
Kaswida za zama hizi ni haramu hili halipingiki asante
 
Mziki kwakua tayari kuna ngoma,ingekuwa hamna midundo ya ngoma basi isingekuwa muziki
 
1.Ala ni kifaa ama kwa kiingereza twaweza kusema ni '' instrument"

2.Kuna uimbaji wa sauti kavu kavu ( accappela) na uimbaji wa kutumia sauti pamoja na vifaa vya kuboreshea (music instruments)

3. Vifaa hivi vya kuimbia ( music instruments) vimegawanyika kaatika sehemu nyingi na vina majina tofauti kama ngoma ( hata dufu ni ngoma) filimbi ( nadhani hizi mnazitumia sana kwenye qaswida) vinanda, magitaa, vyote hivyo ni ala za muziki sasa inategemea mpigaji ame seti kifaa chake au anapiga mapigo gani ndio zinatofautisha aina za muziki lakini ala ni zile zile.
umeelezea vizur kuhusiana na ala,hizo unazosema filimbi zote hazitakiwi!!
imeruhusiwa mashairi na kavukavu bila sauti za maboresho ila tui ni yawe maneno yasiyopingana na dini kiujumla!!!
 
QASWIDA ni Instrumental sio muziki, wimbo wala pambio.
 
kaswida/ qaswida kama ina beat ni haramu ila kama haina beat sio haramu, kinachoharamisha muziki ni maneno na beat, so kawida zina ujumbe mzuri ila beat ndo tatizo linalopelekea kua haramu, zipo kaswida ambazo hazina beat na zinaruhusiwa mfano ile kaswida aliyoimba marehemu Michael Jackson inaitwa Give Thanks To Allah, haina beat na michael aliulizwa akafundishwa ndo mana akafanya vile
NB,kuna kaswida zinaitwa Nasheedi hizi/haya ni mashairi ambayo hayana beat yanaruhusiwa na hua yanamsifia Mungu, mitume,manabii na kufundisha jamii
 
Hebu chora tuone
Sio kuchora tuu sasa hivi nipo mefungua progam zangu za kuchora nota za muse score na sibellius naweza kuchora dakika moja na ku harmonize lakini sitaki kufanya hivyo kwa sababu

1. Ninaheshimu misingi ya dini ya wengine na ninajua nyia moja wapo ya kutunza taaluma zenu za dini ni kukariri ( kuhifadhi) kuanzia maandiko hadi sauti hivyo nikifanya hivyo watu wataanza kujifunza muziki ili wafuate mwenendo wa nota na hivyo kuaharibu asili ila nilikuwa nakujulisha tuu kuwa inawezekana na ni kazi rahisi sana maana hakuna sauti ambazo zinashindikana mbele ya DO-RE-MI-FA-SO-LA-TI-DO
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom