Pwani: Wanafunzi 184 wamepata mimba kwa mwaka 2019. Wengine 1900 washindwa kuendelea na masomo kwasababu ya utoro

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Wanafunzi 184 kati ya 2,091 wa Shule za Msingi na sekondari mkoani Pwani wamekatisha masomo kutokana na kupata mimba kwa mwaka 2019.

Kati yao waliopata ujauzito, wa shule za msingi ni 40 na 144 wa sekondari huku wanafunzi 1,907 wakishindwa kuendelea na masomo kutokana na utoro.

Kutokana na baa hilo, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo, amewaagiza wakaguzi wa shule kufuatilia maendeleo ya elimu mara kwa mara.

Alisema wakaguzi hao wanatakiwa kufuatilia ufundishaji wa walimu, utoro na hali ya chakula cha mchana, akisema kuwa ni vikwazo vinavyochochea utoro.

Ofisa Elimu wa Mkoa wa Pwani, Abdul Maulid, alitoa takwimu hizo za mimba na utoro mjini Kibaha wakati wa kikao cha wadau wa elimu.

"Utoro ni moja ya vikwazo katika suala la elimu katika mkoa wetu, vingine ni umbali mrefu kutoka nyumbani na ilipo shule na wanafunzi kutopata chakula cha mchana shuleni," alisema.

Maulid pia alibainisha kuwa wanafunzi 2,221 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu, hawajaripoti shuleni hadi sasa na hawajulikani waliko.

Maulid alisema wanafunzi hao ni kati ya 25,000 waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza kati ya wanafunzi 30,000 waliohitimu elimu ya msingi mwaka jana.

Baada ya kupewa taarifa hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Ndikilo, aliagiza wakaguzi wa elimu kuhakikisha wanatembelea shule na kufuatilia maendeleo ya elimu mara kwa mara.

Ndikilo alisema ikiwa wakaguzi watajenga utaratibu wa kutembelea shule mara kwa mara, matatizo yaliyopo yatapatiwa ufumbuzi na kuondoa utoro shuleni.

"Kila mwaka tuna kikao cha wadau, lakini sijawahi kuona taarifa zilizochukuliwa kwa wanaowapatia mimba wanafunzi, tunataka tuone nini kinafanyika kwa wahusika ili tabia hii ikomeshwe na tuondokane na hili katika mkoa wetu," aliagiza.

Ndikilo alisema kila halmashauri inatakiwa kufanya juhudi za kuwasaka wanafunzi ambao hawajaripoti shuleni hadi sasa na kufika shuleni kabla ya Machi 30.

Alisema ili kufanya vizuri katika suala la elimu, ni vyema kila halmashauri ikajiwekea mkakati bora na wa msingi kwa mazingira ya kujifunzia na kufundishia.

Alisema wakuu wa wilaya na viongozi wa halmashauri wanatakiwa kukaa na wadau wa elimu kujadili namna ya kuboresha miundombinu ya elimu kama ilivyofanyika katika Wilaya za Kisarawe na Kibaha.

Kikao hicho kilihudhuriwa na wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri, baadhi ya wakuu wa shule, maofisa elimu na wadau wa elimu.

IPP MEDIA
 
Yanii Kuna muda nawaza hizi kampeni za elimu ziko au zinafanyika in a sense ya kuwahimiza wasome
Ila Kuna muda nawaza huu mkoa wa PWANI seems hawapendi kusoma
Ifike mahala tufikirie jinsi ya ku empower na kufanya wanawake wajitegemee
Kuna maana gani kufanya kampeni za elimu mtoto anakuja kupata mimba after form four au anafeli?!
Najitahidi kuwaza labda Kama wamemaliza la Saba wakipewa technical skills and support itawasaidia
Mkoa wa PWANI watu wanajua kusuka, kufuma, kupika n.k
Ifike mahala serikali I invest kwenye hili endapo mtoto atataka kufanya hayo.
Elimu ya kusoma darasani Ni nzuri Ila ya vitendo Ni nzuri Zaid.
 
Watoto wa kike walitakiwa wasikatishwa masomo ,waendelee hadi watakapojifungua na kurudi shule,sheria hii ya kufukuza only watoto wa kike wanapopata mimba nitaifuta within 3hrs baada ya kuupata urais wa 24hrs;elimu kuhusiana na maumbile yetu litakuwa moja ya mada muhimu hasa kwa watoto wa kike,njia za kuzuia mimba na magonjwa ya zinaa itakua rahisi kupatikana mashuleni,condoms,sindano za kuzuia mimba zitakuwa rahisi kuzipata,unapomsomesha mwanamke unasomesha taifa .
 
Hakuna atakaye rudi shule hapo
Labda kwa kulazimisha
 
Wanafunzi 184 kati ya 2,091 wa Shule za Msingi na sekondari mkoani Pwani wamekatisha masomo kutokana na kupata mimba kwa mwaka 2019.

Kati yao waliopata ujauzito, wa shule za msingi ni 40 na 144 wa sekondari huku wanafunzi 1,907 wakishindwa kuendelea na masomo kutokana na utoro.

Kutokana na baa hilo, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo, amewaagiza wakaguzi wa shule kufuatilia maendeleo ya elimu mara kwa mara.

Alisema wakaguzi hao wanatakiwa kufuatilia ufundishaji wa walimu, utoro na hali ya chakula cha mchana, akisema kuwa ni vikwazo vinavyochochea utoro.

Ofisa Elimu wa Mkoa wa Pwani, Abdul Maulid, alitoa takwimu hizo za mimba na utoro mjini Kibaha wakati wa kikao cha wadau wa elimu.

"Utoro ni moja ya vikwazo katika suala la elimu katika mkoa wetu, vingine ni umbali mrefu kutoka nyumbani na ilipo shule na wanafunzi kutopata chakula cha mchana shuleni," alisema.

Maulid pia alibainisha kuwa wanafunzi 2,221 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu, hawajaripoti shuleni hadi sasa na hawajulikani waliko.

Maulid alisema wanafunzi hao ni kati ya 25,000 waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza kati ya wanafunzi 30,000 waliohitimu elimu ya msingi mwaka jana.

Baada ya kupewa taarifa hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Ndikilo, aliagiza wakaguzi wa elimu kuhakikisha wanatembelea shule na kufuatilia maendeleo ya elimu mara kwa mara.

Ndikilo alisema ikiwa wakaguzi watajenga utaratibu wa kutembelea shule mara kwa mara, matatizo yaliyopo yatapatiwa ufumbuzi na kuondoa utoro shuleni.

"Kila mwaka tuna kikao cha wadau, lakini sijawahi kuona taarifa zilizochukuliwa kwa wanaowapatia mimba wanafunzi, tunataka tuone nini kinafanyika kwa wahusika ili tabia hii ikomeshwe na tuondokane na hili katika mkoa wetu," aliagiza.

Ndikilo alisema kila halmashauri inatakiwa kufanya juhudi za kuwasaka wanafunzi ambao hawajaripoti shuleni hadi sasa na kufika shuleni kabla ya Machi 30.

Alisema ili kufanya vizuri katika suala la elimu, ni vyema kila halmashauri ikajiwekea mkakati bora na wa msingi kwa mazingira ya kujifunzia na kufundishia.

Alisema wakuu wa wilaya na viongozi wa halmashauri wanatakiwa kukaa na wadau wa elimu kujadili namna ya kuboresha miundombinu ya elimu kama ilivyofanyika katika Wilaya za Kisarawe na Kibaha.

Kikao hicho kilihudhuriwa na wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri, baadhi ya wakuu wa shule, maofisa elimu na wadau wa elimu.

IPP MEDIA
huko kunanifaa ngoja nikaishi kwenye huo mkoa
 
Back
Top Bottom