Pwani kuna viwanda 371... How!??

Pwani kuna viwanda 371... How!??

Mmeshaambiwa kuwa ukiwa na vyerehani vyako vitatu inahesabika ni kiwanda kidogo
Definition of industry
plural
industries
  1. 1 : diligence in an employment or pursuit; especially : steady or habitual effort
  2. 2a : systematic labor especially for some useful purpose or the creation of something of value b : a department or branch of a craft, art, business, or manufacture; especially : one that employs a large personnel and capital especially in manufacturing c : a distinct group of productive or profit-making enterprises the banking industry d : manufacturing activity as a whole the nation's industry

  3. 3 : work devoted to the study of a particular subject or author the Shakespeare industry
Kwahiyo walivyosema kufikia uchumi wa kati walimaanisha tutafika huko kwa vyerehani na waranda mbao?? Je kumaliza tatizo la ajira walimaanisha tukajiajiri kwenye kuranda mbao na kutengeza majiko ya mkaa???

Duh
 
Wazungu walivyofika.kwene industry revolution sidhani kama walikuwa wanaongelea cherehani 4. So ina maana tanzania tuna viwanda vingi kuliko nchi yoyote duniani?? Mbona hakuna ajira sasa na viwanda vyote hivyo
 
Dar es salaam imeshajaa. Kupata ardhi ya kujenga kiwanda inakubidi ununue nyumba na kuzivunja. Pwani ina maeneo mengi kwa hiyo wawekezaji wengi sasa hivi wanawekeza mkoa wa Pwani
 
mbona umeshindwa kuhoji impact ya madini kwa wana kanda ya ziwa?

Topic ni Viwanda vya Pwani, na sio madini ya kanda ya ziwa. Ni vizuri ukaanzisha uzi wa madini na faida yake kwa watanzania tutakuja kuchangia.. hii ni topic ya viwanda vya pwani ni vyema tukajikita hapo kwa hoja baadala ya kejeli na ushabiki..
 
kwa takwimu hizi bila shaka Mkoa wa Pwani utakuwa ni moja ya mikoa ya viwanda vingi sana duniani ila pia utakuwa ni moja ya mkoa wenye viwanda vingi masikini..
 
hayo mambo ya siasa ni mabaya sana, eti viwanda 300+, viwanda 300+ maana yake huo mkoa unatakiwa uwe tajiri kupita kiasi na watu wake wawe na kipato cha 1mil+ kwa mwezi, sasa nenda pale TRA ukaone serikali inakusanya mapato kiasi gani kwa hivyo viwanda 300+, au nenda kafanye uchunguzi wa impact za kiuchumi kwenye hivyo viwanda 300++
Unaongea hayo2 kwa sababu huna msamiati wa kukubali au2 basi ulishaamua kuwa hivyo- kwann usitumie muda wako ukajiridhishe? kwani viwanda vinakaa mifukoni? Watz kweli ni shida!!!!!!!!
 
kwa takwimu hizi bila shaka Mkoa wa Pwani utakuwa ni moja ya mikoa ya viwanda vingi sana duniani ila pia utakuwa ni moja ya mkoa wenye viwanda vingi masikini..
Tembea uone mkuu. Wewe uko Kishumundu au Rombo midizini unapinga bila kufahamu. Kasi ya ujenzi wa viwanda mkoa wa Pwani ni dhahiri hasa baada ya Dar kujaa.
 
Tembea uone mkuu. Wewe uko Kishumundu au Rombo midizini unapinga bila kufahamu. Kasi ya ujenzi wa viwanda mkoa wa Pwani ni dhahiri hasa baada ya Dar kujaa.

Sipingi kuwepo uwingi wa viwanda mkoa wa Pwani, Uwingi wa hivyo viwanda uendane na maendeleo ya maeneo husika kuanzia miundo mbinu na watu wake, Pia ni nini impact ya hivyo viwanda kwa uchumi wa Taifa.. hivyo viwanda mbona vipo vingi sana mkoa wa Pwani siku nyingi, lakini bado maeneo husika ni masikini kwa kila kitu??????????
 
Unaongea hayo2 kwa sababu huna msamiati wa kukubali au2 basi ulishaamua kuwa hivyo- kwann usitumie muda wako ukajiridhishe? kwani viwanda vinakaa mifukoni? Watz kweli ni shida!!!!!!!!

Tumia akili kidogo kufikiri na usiwe mpiga makofi au mshangiliaji wa kila jambo kwa kuwa limesemwa, sijakataa uwepo wa Viwanda 300+ ila najiuliza na kujaribu kufananisha eneo lenye viwanda 300+ litakuwa tajiri kiasi gani kwa maana ya miundo mbinu, income kwa watu wake na serikali.. Pwani kila mtu anaijua na binafsi naijua kuliko wewe nina uhakika katika hilo..

Kosa lako huijui dunia na hujawahi hata kuona eneo au mkoa wenye viwanda 50 tu na maendeleo ya watu wake sembuse eneo lenye viwanda 300+ halafu watu wake hawana maji, hospitali za kisasa, shule nzuri na maisha yao ni duni..

Dangote amejenga kiwanda mtwara na kutoa ajira kwa watanzania zaidi ya 200, lakini impact ya hizo ajira 200 kwenye jamii husika ikoje, dar es salaam kuna viwanda vingi saaaaana vya wahindi nk na vimetoa ajira kwa maelfu kwa watanzania lakini je impact ya hizo ajira kwa wazawa ikoje?? au nawe ni wale wanaoshangilia watanzania kulipwa 60000/= kwa mwezi na ukiwa exposed kwenye sumu huku hata PPE hupewi?
 
Bila vyerehani vinne au mashine yoyote ile. Hata ukiweza kuzalisha chochote kwa kutumia kiwiliwili chako basi ni kiwanda.

Kuna viwanda vya korosho ambavyo toka a mpaka z ya process yote hutegemea mikono ya binaadam.

Kuwa na vyerehani vinne ukajuwa cha kuzalisha, ni kiwanda kidogo cha kujivunia sana. Kwa mwenye kuelewa.

Hiyo niliyoweka nyekundu ni definition mpya ya kiwanda..!
 
Tumia akili kidogo kufikiri na usiwe mpiga makofi au mshangiliaji wa kila jambo kwa kuwa limesemwa, sijakataa uwepo wa Viwanda 300+ ila najiuliza na kujaribu kufananisha eneo lenye viwanda 300+ litakuwa tajiri kiasi gani kwa maana ya miundo mbinu, income kwa watu wake na serikali.. Pwani kila mtu anaijua na binafsi naijua kuliko wewe nina uhakika katika hilo..

Kosa lako huijui dunia na hujawahi hata kuona eneo au mkoa wenye viwanda 50 tu na maendeleo ya watu wake sembuse eneo lenye viwanda 300+ halafu watu wake hawana maji, hospitali za kisasa, shule nzuri na maisha yao ni duni..

Dangote amejenga kiwanda mtwara na kutoa ajira kwa watanzania zaidi ya 200, lakini impact ya hizo ajira 200 kwenye jamii husika ikoje, dar es salaam kuna viwanda vingi saaaaana vya wahindi nk na vimetoa ajira kwa maelfu kwa watanzania lakini je impact ya hizo ajira kwa wazawa ikoje?? au nawe ni wale wanaoshangilia watanzania kulipwa 60000/= kwa mwezi na ukiwa exposed kwenye sumu huku hata PPE hupewi?
Haya maneno unayaongea ukiwa kwetu tz au ww umezaliwa ulaya muda mrefu2 ila unajaribu2 kulinganisha? bro nchi zetu hazijaendelea ila ndo zinaendelea, wakati mwibgine tuwe na mifano inayofanana na hizi nchi zetu za kiafrika. Pia inawezekana uelewa wako na uzoefu wako ni kwa nchi zilizoendelea wakati meingine lazima ikupe tabu kidogo.
 
sasa hapo naona unapoteza mwelekeo wa kujadili.
Hoja vipo au havipo katika idadi hiyo?
mapato ya hivyo viwanda, kunufaika kwa wananchi pwani, shule zahanati, ni vitu vingine.
Idadi inaendana na mapato otherwise is rubbish, kama ni hivyo kwanini msimwambie rais Pwani ina viwanda 5,000 ili afurahi zaidi.
 
Idadi inaendana na mapato otherwise is rubbish, kama ni hivyo kwanini msimwambie rais Pwani ina viwanda 5,000 ili afurahi zaidi.
SASA HUELWEKI UNAPINGA NINI, Idadi ya viwanda au faida ya viwanda.
siku wakizungumzia economic impact ya viwanda kwa wananchi utapinga nini. jifunze kufocus kwenye kile ulichoanza kuzungumzia
 
Bado kuna viwanda 80+ vinaendelea kujengwa...Tuliahidi tunatekeleza....hamuangaliagi taarifa ya habari...Mkuu wa mkoa wapwani akiibuka ujue kuna kiwanda anakizindua
Wachomelea mageti,wafyatuaa tofali,mafundi cherehani naona mmewaingiza kwenye mafanikio yenu ya viwandaaa

OvA
 
Back
Top Bottom