OP lumumba
Twende kwenye jicho la Tatu
Je urusi Ni nchi ikiyostaarabika na kuheshimiana km nchi za ulaya na Marikani?
Kwanini wakimbizi wengi wanaotorekea vita middle east na Arab world wengi wanarefaa kwenda Europe na amerika na sio Russia
Angalia Syria kwa mfano mfadhili mkuu wa Assad Ni serkali ya bwana putin
Lkn hana Habari na wakimbizi
Unafikiri Urus imestaarabika kweli au kwa kuwa ipo ulaya tu
Mkuu,
Mosi, Ustaarabu is a Relative Term.
Wanadamu hatuwezi kulingana, na kama unaamini kwamba mfumo wa maisha wa Warumi na Wagiriki ndiyo Ustaarabu. Basi ni dhahiri kwamba kila ambacho sicho cha Mzungu utakiona ni kitu cha kishenzi, hata kama ni dhahabu.
Pili, Wakimbizi wa Syria kukimbilia Ulaya haimaanishi wao ndiyo wamestaarabika kuliko wengine.
Huu mfano hauna mashiko kabisa kwasababu Wakimbizi hata Tanzania, Congo DRC na Uganda wapo wengi tu,
Wala hili halimaanishi kwamba sisi Watanzania tumestaarabika sana kuliko Wanyarwanda, Warundi au Wakongo.
Tatu, neno mkimbizi kilatini chake ni "
fugere" ambalo linamaanisha mtu mkimbiaji.
Ukisoma vizuri UNITED NATIONS REFUGEE CONVENTION 1951 wanasema A refugee is a person who runs away from his home country, and seek asylum in another foreign state due to the fear of persecution which can result out of War, Ethnic Violence, Religious Persecution, Natural Calamities etc. Mpaka hapa utakuja kugundua kitu kimoja cha muhimu kwamba, mkimbizi huwa hana uchaguzi wa wapi aelekee. Yeye hukimbilia popote pale ambapo atapata usalama wake kwa muda tu. Ukiona mkimbizi anachagua kwa kwenda huyi siyo mkimbizi bali ni muhuni tu anaganga njaa.
Mifano hai:
1. Wakimbizi tokea Syria hawakimbilii Ulaya peke yake kama unavyoamini, wengi wako Jordan na Lebanon.
2. Wazungu wengi sana wakati wa vita ya pili ya dunia walikimbilia Africa na India (Hapa una la kusema ?)
3. Watanzania wengi baada ya Mkapa kuwavuga Zanzibar mwaka 2001 walikimbilia Somalia (teh teh teh)
NB: Hapa hoja yako ya Ulaya mkuu wangu inakosa mashiko kabisa.
Kwasababu hata Somalia ishawahi kutunza Wakimbizi wa kipemba japo kule kuna vurugu kuliko hapa kwetu.
Nne, ukweli mchungu ambao unaufumbia mambo ni kwamba,
Watu wengi wanakimbilia Ulaya kutafuta maisha na walu hakuna jingine la maana sana.
Takwimu zinasema siku hizi mambo yanabadilika sana, watu wakishchuma mapesa huko Ulaya huwa wanarudi kwao.
Hapa suala la kustaarabika au kutostaarabika halina mashiko kabisa kwasababu watu wanaangalia Maslahi kwanza.
Hivyo kama Urusi ingekuwa bado ina nguvu kubwa kiuchumi kama zamani basi leo hii wangekuwa wanapata wageni sana kama ilivyokuwa miaka ya 60's, 70's na 80's. Kukuhakikishia hili tembea hata hapo Afrika Kusini uone jinsi ambavyo Watanzania, Waethipia na Wakenya wamezamia kutafuta maisha. Hili halimaanishi kwamba wao ndiyo wastaarabu kuliko Afrika nzima, la hasha. Ila tu wana mapesa mengi na madili kuliko sehemu yoyote ya kusini mwa jangwa la sahara.
NB:Ustaarabu ambao wewe unauongelea kuhusiana na Ulaya siuelewei ni upi,
Hebu dadavua kwanza kisha tuendelee na mjadala.