Push Mobile wampa Tuzo ya Mwanasiasa Bora Prof. Sospeter Muhongo

Push Mobile wampa Tuzo ya Mwanasiasa Bora Prof. Sospeter Muhongo

PUSH MOBILE IMEHARALISHA UFISADI WA ESCROW

* Ni kupitia Tuzo za jamii

* January Makamba akaangwa

Usistaajabu ya Musa kabla haujaona ya Firauni ndivyo yalivyojitokeza kwenye tuzo za jamii ambazo zimeacha maduwazo na maswali kede wa kede.

Vipengele ama tuzo mbili zimetokea kuwaacha watu midomo wazi. Tuzo ya kwanza ni ile ya Mwanasiasa bora ambayo imechukuliwa na aliyekuwa Waziri wa nishati na madini aliyejiuzulu kwa kashfa ya ufisadi wa Escrow, Prof. Sospeter Muhongo.

Tuzo hizo ambazo zimefanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere zilizua gumzo kubwa kuwa ile kashfa ya ufisadi wa bilioni zaidi ya 300 ambayo ilitikisa nchi kutokana na kuchukizwa wengi hali iliyopelekea Baraza la mawaziri kuvunjwa, mawaziri kujiuzulu akiwemo Prof. Muhongo leo hii anapewa tuzo ya mwanasiasa bora. Haya ni maajabu ya Dunia.

Kashfa ile ya ufisadi wa Escrow iliyosababisha wahisani kuifungia misaada Tanzania katika bajeti ya nchi, kashfa iliyosababisha hali ya kifedha nchini kuwa mbaya, ndio hiyo hiyo ambayo Push mobile wameamua kubariki ufisadi huo kwa kumpa tuzo ya Mwanasiasa bora mtuhumiwa wa kashfa hiyo aitwaye Prof. Muhongo ili waisafishe kashfa hiyo chukizo kwa watu.

Watu ukumbini wakaanza kuhoji, hakuna mwanasiasa msafi asiye na kashfa wa kupewa tuzo hiyo mpaka wampe Prof. Muhongo? Ni kweli Watanzania wamepiga kura zao kumpigia mtuhumiwa wa ufisadi wa Escrow?

Tuzo ya pili iliyozua gumzo ni tuzo ya mwanasiasa kijana anayechipukia ambayo alipewa January Makamba.

Maswali mengi yaliibuka kuwa January Makamba ni mwanasiasa bora kijana kumzidi Zitto Kabwe, kumzidi John Mnyika, ama kumzidi Mwigulu Nchemba? Kwanini push mobile wampe ushindi January Makamba?

Kwa muda mrefu January Makamba ambaye ni Naibu waziri wa sayansi na teknolojia amekuwa akihusishwa na uhusiano wa karibu na kampuni ya push mobile.

Mahusiano haya yalianza kuibuliwa wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 ambapo walituhumiwa kuiibia CCM Tsh. bilioni 8 za uchaguzi, leo hii wameamua kuuainisha wazi ushindi wa January Makamba na uhusiano wake na push mobile.

Kila mtu amechukizwa na usanii uliofanywa na push mobile na waandaaji wa tuzo za jamii na kuhoji kama walikuwa tayari na washindi wao mifukoni kwanini wachukue pesa za watu kupitia njia ya upigaji kura, huu ni ufisadi uliopitiliza kiwango.

Ikumbukwe washindi wa tuzo za jamii wamepatikana kupitia upigwaji kura kupitia huduma ya push mobile lakini mtangazaji wa tukio hilo alisema wazi wazi kuwa washindi hao haamini kama kweli wamepatikana kupitia kura za wadau. Na hili ni kweli kabisa kuwa ushindi ule ni dhahiri ulikuwa wa mezani na si kura za watu.
 
Unajua maana ya mwanasiasa bora?

Kama ni cv na mafanikio yake wangesema "Mtendaji bora" nasio mwanasiasa bora.

Mwanasiasa bora ni yule anayekubalika kwa umma kwa siasa zake bora.
Yeriko, kwanza nikusahihishe kuwa tuzo haikuhusu mwanasiasa bora bali ilihusu Mwanasiasa Mwenye Mafanikio Katika Jamii. Hapo ndipo Muhongo anapowazidi wengine. Mafanikio yake katika jamii yapo dhahiri na kila mtu anajua achilia mbali unafiki wa baadhi ya watu kumhusisha na kashfa ya escrow
 
Nchi hii sasa tumefikia mahari pabaya kila kitu sasa ni cha kuchakachua. Tutarajie hayo pia kwenye urais.Mungu ibariki Tanzania
Team Lowasa mnaweweseka sana. Angeshinda Lowasa hapa akina Ocampo four, sijui funza, sijui minyoo, sijui John Okello, sijui laki si pesa wangejazana humu kushabikia. Sasa wameufyata
 
Siku hizi nikiisha ona uzi umesifiwa na lizabon tu, basi najua hiyo maada au kilichofanyika ni full ujinga, kitendo tu cha kusifia hizo tuzo tayari najua kuna ujinga umefanyika, kwa ufupi humu ndani kipimo changu nachokitumia kwa ujinga ni LIZABONI
Acha kumtusi wa Kunyumba wewe. Kwani kosa la Lizaboni liko wapi?
 
Kwa kuwa mlitaka apewe EL ndiyo maana mapovu yanawatoka, subiri maajabu mengine yanakuja, mtarajiwa wenu nje ya uringo, hata 18 hagusiiii
 
Ndio maajabu ya Firaun haya maana Muhongo hata bungeni kateuliwa na rais hajawahi katika maisha yake kugombea nafasi yoyote ya Kisiasa nchini. Hana uzoefu wa kisiasa ktk uongozi wa chama chochote nchini, hajawahi kusimama jukwaa lolote la kisiasa, sasa hii kupewa tuzo la mwanasiasa bora ni mchezo gani huu ama pengine jamaa ni mwekezaji kwa hisa au kamwaga mifedha hapo Push Mobile....
Hapo mkuu na mi ndo nashangaa, kwanza jamaa alishawahi kusema ye hakugombea ubunge bali aliteuliwa hivyo sio mwanasiasa, labda wamekosea walitaka kusema waziri bora aliyewahi kuongoza wizara ya madini
 
Sina uhakika na January Makamba, lakini kwa uhakika kabisa Prof. Muhongo anastahili kupewa hiyo tuzo. Kashfa ya Escrow haina uhusiano na Muhongo. Wanasiasa wanafiki (ZZK, Ole) na wafanyabiashara (Mng na Mkn) ndiyo waliolazimisha kashfa hiyo kumgusa Muhongo.

Kashfa ya Escrow ilikuwa ni ya kisheria (ilihusu mwanasheria wa Wizara, TANESCO na Mwanasheria Mkuu), taratibu za kifedha (Wizara ya Fedha, TRA na Benki Kuu) na uidhinishaji wa malipo (Ikulu iliridhia). Waziri ni msimamizi wa sera na pia ni msemaji wa Wizara, wakati Katibu Mkuu ni mtendaji wa Wizara. Hakukuwepo na uwezekano wa Prof. Muhongo kukana taarifa na maelezo aliyokuwa akipewa na Mwanasheria Mkuu na Wataalam wa Wizara ambao aliwakuta na ambao walikuwa na uelewa wa muda mrefu kuhusiana na Escrow. Pia siyo Waziri aliyeidhinisha malipo kwa Escrow. Idhinisho lilitoka Bank Kuu, Wizara ya Fedha, Mwanasheria Mkuu na Ikulu. Uhusika wa Muhongo uko wapi?

Tusipelekwe kama taahira bali tuchambue kwa kutumia akili zetu. Tunapopoteza muda na wasio na hatia, tujue tunatoa nafasi kwa wenye hatia kufanya mambo yao bila kuguswa. Wevi wakubwa wa TANESCO ni pamoja na mkn aliyekuwa akilipwa U$2,000 kwa saa (TZS 1,880,000). Huyu alikuwa akilipwa wastani wa U$20,000 kwa siku anaposhughulikia kesi za TANESCO. Muhongo aliwaondoa wevi wa namna hii, nao wakawatumia wanasiasa uchwara kama akina ZZ (ambaye alikiri kupewa gari) kumwondoa Muhongo.

Muhongo japo uliingizwa katika mfumo uliooza lakini uzalendo wako hautapuuzwa na mtu yeyote mwenye akili, uelewa na uzalendo kwa Taifa lake. Mengine yote dhidi yako yanaweza kusema kwa ushabiki au chuki lakini ukweli utasimama daima.
 
Kama ushindi ni wa kura, kuna kampuni/taasisi tofauti iliyohakiki kura hizo?
 
Taifa hili sio la wajinga, mjinga ni wewe peke yako. Tuzo mnatunga wenyewe na mnapeana wenyewe sasa ujinga wa taifa unatoka wapi hapa. Kwanini chuki zenu na wanasiasa wenzenu mtukane watu wote. Tanzania haiwezi kuwa taifa la wajinga kwa sababu ya mjinga wewe mmoja tu.

Hizo ni vitu wanajifurahisha wenyewe haya na wewe umeshinda tuzo ya kutukana taifa zima just it, msitukane wasio husika sababu ya chuki zenu tu.

Taifa la wajinga kwa idhini ya majuha,

Muhongo tangu lini amekuwa mwanasiasa? Alishawahi kushiriki siasa wapi?

Tangu azaliwe hajawahi kuwa mwanasiasa mpaka juzi alipoteuliwa kuwa mbunge, hivi tayari anaitwa mwanasiasa mpaka kupewa uanasiasa bora?

Hizi tafiti za kizandi vyombo vya dola vishughulike nazo kuliko kupoteza mda na watu wema akina Gwajima.
 
Usually I don't quote you...bcoz arguing with stupid it reflects who am I....
👉 But I see ur stupidity, arrogance, hooliganism, foolishness is BEYOND ur dead mind and body, ur useless and being used...👌 scraped..!!!
So I kicked-in to put down ur Irritating puru...!!!

Ur always in a wrong side of the world...pro-membe...
Defending CCM candidates like JM Makamba hawauziki...mbaya zaidi you play ur nasty mind to raise false reports kumchafua Edward Lowassa...

Umekuwa kiherehere...muongo na kumchafua Lowassa ukitumiwa na hao watu wasio uzika CCM...Hakuna situation Lowassa kamsema MEMBE au kumtuhumu yeyote yule...Ila www umekuwa ukitumiwa ktk Miranda ya Jamiii kumtuhumu na kumchafua Lowassa kila kona...ukitumiwa na mabwana zako....

Hiyo tabia ikome...huna adabu ww mtoto....

Aliyeibuka mshindi ni Prof Sospeter Muhongo ambaye licha ya kudumu kwenye siasa kwa muda mfupi, amefanya mambo makubwa sana. Kubwa zaidi ni kusambaza umeme vijijini na kusimamia nidhamu na kuziba mianya ya rushwa kwenye sekta za nishati na madini. Uwekezaji katika gesi umempaisha Muhongo hadi kwenye level ya juu sana na kuwapiku wenzake.

Kwa upande wa Mwanasiasa Kijana mwenye mafanikio katika jamii, aliyeibuka Mshindi ni Januari Makamba. Huyu naye amemudu vema nafasi yake ya Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia. Kawapiku wenzake akina Zitto Kabwe, Mnyika na wengineo. Hongera Makamba.
 
Acha kumtusi wa Kunyumba wewe. Kwani kosa la Lizaboni liko wapi?

You & Lizaboni are dead long ago....unnoticeable...

Ur dead human beings walking...puppets, devils doing evils....ruler of hell...👌👌👌
 
Sina uhakika na January Makamba, lakini kwa uhakika kabisa Prof. Muhongo anastahili kupewa hiyo tuzo. Kashfa ya Escrow haina uhusiano na Muhongo. Wanasiasa wanafiki (ZZK, Ole) na wafanyabiashara (Mng na Mkn) ndiyo waliolazimisha kashfa hiyo kumgusa Muhongo.

Kashfa ya Escrow ilikuwa ni ya kisheria (ilihusu mwanasheria wa Wizara, TANESCO na Mwanasheria Mkuu), taratibu za kifedha (Wizara ya Fedha, TRA na Benki Kuu) na uidhinishaji wa malipo (Ikulu iliridhia). Waziri ni msimamizi wa sera na pia ni msemaji wa Wizara, wakati Katibu Mkuu ni mtendaji wa Wizara. Hakukuwepo na uwezekano wa Prof. Muhongo kukana taarifa na maelezo aliyokuwa akipewa na Mwanasheria Mkuu na Wataalam wa Wizara ambao aliwakuta na ambao walikuwa na uelewa wa muda mrefu kuhusiana na Escrow. Pia siyo Waziri aliyeidhinisha malipo kwa Escrow. Idhinisho lilitoka Bank Kuu, Wizara ya Fedha, Mwanasheria Mkuu na Ikulu. Uhusika wa Muhongo uko wapi?

Tusipelekwe kama taahira bali tuchambue kwa kutumia akili zetu. Tunapopoteza muda na wasio na hatia, tujue tunatoa nafasi kwa wenye hatia kufanya mambo yao bila kuguswa. Wevi wakubwa wa TANESCO ni pamoja na mkn aliyekuwa akilipwa U$2,000 kwa saa (TZS 1,880,000). Huyu alikuwa akilipwa wastani wa U$20,000 kwa siku anaposhughulikia kesi za TANESCO. Muhongo aliwaondoa wevi wa namna hii, nao wakawatumia wanasiasa uchwara kama akina ZZ (ambaye alikiri kupewa gari) kumwondoa Muhongo.

Muhongo japo uliingizwa katika mfumo uliooza lakini uzalendo wako hautapuuzwa na mtu yeyote mwenye akili, uelewa na uzalendo kwa Taifa lake. Mengine yote dhidi yako yanaweza kusema kwa ushabiki au chuki lakini ukweli utasimama daima.
Maneno yako pekee yamedhihirisha hakustahili maana umeshasema WANASIASA ni wanafiki ukimtoa Muhongo kati ya wanasiasa, hivyo sio mwanasiasa na hakustahili tuzo..Maswala ya Muhongo kuondolewa uwaziri ni bunge kutokuwa na imani naye kama waziri baada ya kusema UONGO...You lie you become an accomplice.
 
Hivi wewe mbona mpuuzi sana??

Utasemaje MTU aliyeshika uwaziri ambayo ni nafasi ya kisiasa si mwanasiasa??

Utasemaje Mbunge ambaye naturally ni political position si mwanasiasa??

Siasa lazima ugombee ndo uitwe mwanasiasa??

Na makatibu wakuu walioteuliwa bila kugombea lakini wanaendesha vyama vya siasa utawaita si wanasiasa ??

wenye kadi za vyama kujitambulisha ufuasi wao utasema si wanasiasa??

Wewe Una shida gani kwenye akili yako??
 
Hapana mkuu usiwe mkali sana twende kwa kituo, jazba ya nini?. Sio wabunge wote ni wanasiasa na lengo haswa la wabunge ni wawakilishi wa wananchi katika majimbo yao. Wapo wabunge ambao wametokana na makundi ya walemavu ambavyo sio vyama vya siasa na wapo wawakilishi wa kina mama na wapo waloteuliwa na rais kwa minajiri yake nje ya chama.

Wanasiasa ni wale wabunge walotokana na vyama vya siasa, hawa ndio wanasiasa maana wanawakilisha itikadi na sera za chama kisiasa bungeni katika kutunga sheria, kupitisha bajeti na kuisimamia serikali. Bunge ni sawa na kamati ya harusi tu..Katika mipango ya harusi ya Kiislaam watu kuvaa kanzu na wanawake kujifunga mitandio haina maana watu wote pale ni waislaam.
 
Hapana mkuu usiwe mkali sana twende kwa kituo. Sio wabunge wote ni wanasiasa na lengo haswa la wabunge ni wawakilishi wa wananchi katika majimbo yao. Wapo wabunge ambao wametokana na makundi ya walemavu ambavyo sio vyama vya siasa na wapo wawakilishi wa kina mama na wapo waloteuliwa na rais kwa minajiri yake.
Haya ndio madhara ya kuamini unajua Sana kumbe mweupe!!

Hao wabunge wanaowakilisha makundi maalumu Kama walemavu...vijana...wanawake.....wazee....wasomi n.k n.k wanapitia mchakato gani kupatikana??

Mbona wengi hupendekezwa na vyama vya siasa kwa tume kulingana na idadi maalumu na hao wawakilishi huchujwa kwa kura za maoni ndani ya vyama vyao??

Akina Regia Mtema waliingia bungeni kupitia wapi??

Mbona wabunge wanaoteuliwa na Rais wote hutokana na vyama vya siasa??

Mkuu Kama hujui vitu heri unyamaze tuu

Wanasiasa ni wale wabunge walotokana na vyama vya siasa, hawa ndio wanasiasa maana wanawakilisha itikadi na sera za chama kisiasa bungeni
unaweza orodhesha wabunge wanaowakilisha makundi maalumu (viti maalum) ambao hawakupendekezwa na vyama vyao kwa tume??
katika kutunga sheria, kupitisha bajeti na kuisimamia serikali. Bunge ni sawa na kamati ya harusi tu..Katika mipango ya harusi ya Kiislaam watu kuvaa kanzu na wanawake kujifunga mitandio haina maana watu wote pale ni waislaam.

Waziri ni nafasi ya kisiasa au kitaalam??
 
Back
Top Bottom